Ndoa inanishinda, naomba mnishauri kisheria

Mkeo kabila gan, tuanzie apo
 
Well said, it's over
 
Kwa ndoa ya Kikristo kuachana ina kaugumu kake kidogo
Mmezaa watoto 2, its obvious mnaweza kuamua kuachana na mkafanikiwa lakini after 2 years nyote mtakuwa kwenye majuto nikimaanisha Wakwe ambao wamelianzisha, Wewe, Mkeo na Watoto

Ni wazi kwamba tatizo liko kwa Wazazi wa mkeo, na ni wazi vile vile kwamba Mkeo aidha ni mdogo kwa umri au hajapevuka kiakili na yeye ndiye ataejuta zaidi mambo yakishaharibika. Kuisaidia ndoa yako ni jinsi gani unamfanya mkeo anazinduka ktk lindi la tashwishi za Wazazi(hasa Mama)
1. Unaweza fanya kikao na Baba Mkwe tu akiwa na Mzee mwingine ambaye ni Rafiki yake wa karibu umuelezee dukuduku zako na usistize kwamba huna lengo la kumuacha mkeo. Kama Baba nimuelewa wa maisha na hajashikwa na mkewe na yeye ndiye Breadwinner pale nyumbani una nafasi kubwa ya kuiokoa ndoa yako kwa kumtumia yeye. Kaa naye karibu, jinyenyekeze atawiwa kuokoa ndoa yenu, wachaga ni waelewa saana ikiwezekana tafuta hata wazee wa kichaga ukae nao kwanza ili wakapambane na mwenzao

2. Tafuta shangazi yake muelewa, shosti, au Mama mwenye hekima katika Jumuiya(for catholics) au jamii, ampe mwanga wa maisha, amwonyeshe vile jinsi gani anavyopeleka maisha yake shimoni ampe na case studies

3. Viongozi wa Dini nao ni muhimu, kama mtakuwa na vikao ambavyo vinahusisha familia zote mbili. Watanzania bado tunaithamini dini hivyo kuwepo kwa watu wa dini kunaweza rudisha nyuma nia ovu.

4. Tengeni Muda na Mahali
Wakati mwingine mazingira yanaweza kuwa kikwazo hebu tafuta muda muende mbali na mlikozoeaga kwenda. Mnaweza kwenda Magoroto, Zanzibar au Mafia au popote kulingana na uwezo wenu. Lengo ni kuonyesha thamani ya umoja wenu ukilinganisha na hasara ya utengano wenu

5. Acha Kuchepuka

6. Mtafutie shughuli ya kufanya, fuatilia kila mara anaendeleaje. Ni kawaida kwa wamama wa Nyumbani(most of them) kuona pesa huwa zinapatikana kiurahisi hivyo unaposhindwa kutimiza matakwa fulani anajua unafanya makusudi

7. Hamad Kibindoni, Silaha Mkononi
Usikae kiboya, seek legal advice kwa Mwanasheria ikibidi ulipie kabisa sio humu JF, ili silaha za kidiplomasia zikishindikana uwe unajua muelekeo

8. Muombe Mungu kikombe kikuepuke. Nguvu ya kuamka usiku na kuomba Mungu ni kubwa sana, ikiwezekana hata kufunga ufunge, hasa hasa linapokuja suala la watoto
 
Ushauri makini!💪💪
 
wazazi wa huyo mwanamke ni mapopoma na ndio source ya huo mgogoro.
 
Asante saaana,,tumeshakaa saaana lakin now tupo huku kwetu mbeya,,baba mkwe ndio kaanza mambo yake kunipigia simu akinitishia,ndio maana niliomba ushaur kisheria ikiwa atakuja kweli kumchukua binti yao n sheria au utaratibu gan naweza kuitumia kuzuia wanangu labda tu itapoamuliwa na mahakama
 
Pole sana mkuu.

Baba mkwe ni katika watu ambao wanatakiwa wakuheshimu sana.
Sijui mkweo ni mtu wa aina gani.

Ikifikia hatua kama hiyo kwamba baba wa mke hana busara,ni tafrani.

Mke uliyemuoa hana busara wala heshima.daah mara nyingi inakuwaga ni kwenda kumpumzisha kwao.ikiwa njia zote zimefeliiiiiii mpe talaka usitake kuonekana mstaarabu katika sehemu ambyo hata hawana shida na ustaarabu wako.

Mpe talaka alafu mpotezee kamawezi hivi huku ukimpa mahitaji yake ya kawaida.
Hapo ni nafasi yake kujirudi
 
Suala la mchepuko n kweli nnao lakin hakufanya nishindwe kutimiza majukumu yangu,pia mm kuwa na mchepuko kulichangizwa na yy (sijitetei) akawa hanifulii nguo ,hanipikii kabisa unadhan ningefanyaje?

Duh

Hapa ndio naona ishu

Huu mchepuko anaujua physically?

Ungeficha kabisa asijue lolote whatsoever,kata ,kata,kata!

Huu mchepuko ni Mnyakyusa kama wewe?

Sorry kwa maswali sir!
 

Hapo ndipo penye tatizo lako!

Inaonekana unawapenda sana watoto wako kitu ambacho ni kizuri lakini wao wamechukulia huo kama udhaifu wako na wamepata pa kukukamatia!

Mazingira gani mabovu kama binadamu wengine wanaishi?

Piga moyo konde,
Saingine mtoto akililia wembe mpe!

Waache wakae hata Mwaka watakukumbuka na kutaka kurudi kama ni damu yako haitapotea!
 
Lakini na wewe ujitafakali kama unamicheko ndiyo mara nyingi huleta mifaraka ndani ya ndoa ili uwape Plan B
 

Watoto hadi wafike umri wa miaka 7 ,
Hata hivyo kuna facts huwa zinazingatiwa kabla kufikia uamuzi huo !
Hata kabla ya hapo wawezapewa!
Nenda Uastawi wa jamii!

Yani wanakuona dhaifu sana kwa kuwang’ang’ania duh!

Vinginevyo ujenge hoja kuwa wakuondoka pesa ya kugawa ya matumizi hautakuwa nayo!
 

Uko sahihi wanataka kufanya watoto kuwa kitega uchumi cha yeye na wazazi wake!

Wewe muulize kwa meseji mzee unachotaka nifanye ni nini?

Akisema anamtaka mwanae muulize je na hawa watoto wadogo unawafikiriaje?

Akikujibu vyovyote tunza meseji.

Halafu waache waende zao using’ang’anie
 

Mkuu

Naona wazazi wameingilia ndoa

Kwavile mama yako haelewani na mkeo,basi watenganishe!

Na yeye wazazi wake hawataki kuelewana na wewe,awatenganishe na wewe...

Binafsi sijaona kama huyo dada ni ana tatizo au ukosefu wa adabu sana kua mke

Wala wewe huna shida kabisa,au labda kuna vitu vingine hujatuambia

Naona purely parental relations wa pande zote mbili

Huyo baba wa binti ni kiazi,ila mama yako umegusia kwa mbali sana hujafunguka hua analeteana na mkeo noma gani mpaka hawapendani kiasi hicho!

Clear all these parental rubbish za pande mbili...na mkeo aweke matako chini
 
Umekosea kidogo kijana
Hebu nikuombe utililike yote yaliyopo nyuma ya pazia
Je wewe na mkeo mnaugomvi gani yaani kunatofauti zozote na je ni yepi ambayo tayali mkeo keshayafikisha kwao?
Mama na mkwewe je zinawaka au hawaelewani na je tatizo huwa ni nini wife alishawahi kukulalamikia chochote kuhusu mama?
Kipi kimesababisha wife akaishi na mkwewe ambako ni mbali na unapoishi?
FUNGUKA TUKUSAIDIE KUNUSURU NDOA YAKO
 

Mnaambiwa kila siku oeni kwenu hamsikii

Unachosema kipo kwenye DNA yao,you can never change them!

Sijui kwanini watu wanajikombeleza makabila mengine wakati wana warembo wazuri sana kwao...

Tutumie common sense!
 
Baba mzazi na MUHA...

Sio mchaga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…