Pole kwa changamoto na hongera kwa kuliweka mezani maana penye wengi hapaharibiki neno. Maelezo uliyoyatoa hayajitoshelezi hivyo itakuwa vigumu kupata ushauri uliojitosheleza. Itakuwa vigumu kukupatia ushauri mzuri kwani inaonekana kuna baadhi ya maelezo hujayaweka wazi. Kila atakayekupa ushauri atakupa ushauri kwa kutegemea taarifa pungufu ulizotoa. Yawezekana una sababu za msingi za kutoweka bayana taarifa zote za chanzo cha tatizo lako.
Haingii akilini mwanamke uliyeoana naye kwa mapenzi na hadi mkapata watoto leo aende kazini kwako kudai mshahara!
Haingii akilini wazazi wanaompenda binti yao ghafla wamshawishi aachane na wewe hadi kufikia kukupeleka mahakamani!
Haingii akilini tena from nowhere mkeo atamke kwamba 'Mama Mkwe wangu ni kama mke mwenza kwangu'
Kauli ya kwamba 'Mama Mkwe ni Kama Mke Mwenza' inaashiria kwamba umeshindwa kuweka usawa kati ya mama yako na mkeo, kila mmoja wao ana nafasi muhimu kwako - mama ana nafasi kwako kama mzazi na mlezi na pia mkeo ana nafasi yake kama mweza wako wa maisha.
Kwa kuwa wewe uko katikati ya sakata hili ambalo upande mmoja ni mkeo, wakwe zako na mama yako wewe ndiwe pekee wa kuliweka sawa jambo hili. Tambua kuna gharama kwa kila maamuzi tuyafanyayo hivyo tafakari kitu ni muhimu kwako na uko tayari kulipa gharama kiasi gani. Chochote unachoamua hakikisha unaweza maslahi ya watoto mbele kwanza kuliko chochote. Ubishi na ushindani kati yako wewe na mkeo au wakwe zako hautakusaidia - angalia maslahi ya watoto yameangukia wapi. Kwa maslahi ya watoto kama inawezekana jaribu kumshawishi mkeo mjaribu kuishi kama zamani. Ukifanikiwa kuishi na mkeo (hata kama amekukera kiasi gani) kuna faida nyingi kwako/kwenu kuliko hasara utakazopata ukiamua mtengane. Achana na epuka kabisa masuala ya kumpeleka mkweo au mkeo mahakamani - EPUKA KWA NGUVU ZOTE.
Kuna mengi lakini muda hautoshi - kama unahitahiji ushauri zaidi njoo pembeni