Willima
Member
- Jul 27, 2022
- 26
- 39
Watafiti wamezungumzia suala la ndoa kwa vijana wa kike, kasikazini mwa Tanzania, wameonyesha sababu za kupamba moto kwa matukio hayo na athari zake kwa waathirika wa mitazamo na mawazo hayo (wanawake).
Sababu za kupamba moto kwa matukio haya ni ukosefu wa elimu ya kutosha juu ya masala ya ndoa kwa vijana wa kike, kufikiri kuwa ndoa ndio heshima kwa mwanamke, pia ndoa imechukuliwa kama kitega uchumi kwa wazazi wa watoto wa kike, na pia masala ya ndoa yanajitokeza sana kwasababu ya kutokuona umuhimu wa kumsomesha mtoto wa kike hivyo akifanikiwa kuhitimu elimu yake ya msingi hulazimika kuingia kwenye ndoa katika umri mdogo kwakuangalia kigezo cha kupevuka kwa mtoto huyo wakike na kutozingatia umri wake.
Athari za ndoa za utotoni kwa watoto wa kike, ndoa za utotoni hupunguza upatikanaji wa elimu kwa wasichana, pia ndoa za utotoni husababisha mimba za utotoni na husababisha matatizo wakati wa kujifungua na hata kusababisha kifo kwa mama na mtoto.