Ndoa ndiyo taasisi hatari kuundwa duniani kwa lengo kutesa maisha ya binadamu

Ndoa ndiyo taasisi hatari kuundwa duniani kwa lengo kutesa maisha ya binadamu

Uzi umejibiwa vizuri na ni vyema uishie hapa.

Inamaana hata ndege wanamzidi maarifa na akili kwa kuwa wawili wawili mleta mada?

Hujui Binadamu ni kiumbe dhaifu ambaye ukamilifu wake unahitaji jinsi pinzani(Ke/Me) ili ukamilike kimaisha ktk hii dunia kwa kusaidiana?

Au kila jinsi inahitaji uwepo wa jinsi nyingine kimahusiano ili iweze kuwa na amani kimaisha?

Huitaji ndoa achana nayo isikupotezee muda, sababu Mungu hajalazimisha Binadamu awe na mwenzi wa ndoa bali ni hiyari, isipokuwa unatakiwa uishi kiuaminifu bila ya kujihusisha na uzinzi wala uasherati ili yasije kukukuta madhara ya kutokuwa na ndoa kama umaskini, magonjwa, ubakaji, ulawiti, malezi mabovu ya watoto ukampatia Mungu lawama zisizo na mashiko.
kwan ndoa inamaliza matatizo haya. jiondoe kwenye matumaini. ishi kiualisia
 
Ila ukweli nikwamba pikipiki hazifai kupandwa na binadamu ila ugumu wa maisha tu ndo chanzo cha kuzipada ndugu yangu
Wapo Wana maisha Safi na wanapanda pikipiki. Je wale wazungu wanaopita hapa Tanzania na mipikipiki Yao BMW kutoka Cairo mpaka Cape Town Wana maisha magumu?
Kuna mjerumani nimeishi naye hapahapa aliporudi kwao akachukua pikipiki kutoka Ujerumani mpaka Mongolia kwa ajili ya utalii. Pikipiki ni chombo, ni maamuzi yako kuamua unakitumiaje.
 
True nakubaliana nawe. Mwanamke na mwanaume wakikaa pamoja ugeuka kuwa maadui.Hii ni nature. Thus unashauriwa kama huna akili usioe.
Kama una hasira usioe/olewa bora ukawe sister au padri ndoa inataka akili na hasira ni kipimo cha mtu asiye na akili.
 
Ndoa ni taasisi bora kama nyote mnaakili yaani hekima.
 
MWANAMKE MPUMBAVU HUPIGA KELELE.

Kabla hatujatafuta mchawi wa mahusiano yetu, tunapaswa kujichunguza sisi wenyewe kwanza tupo sawa au tuna shida mahali ila hatujui kama hilo ndilo linatufanya tushindwe kuwa na amani kwenye mahusiano yetu.

Ukiwa kama binti, unaweza usiwe na tabia zingine mbovu unazojua wewe kama vile zinaa ila ukawa na kitu hichi, "kelele/makelele" unashangaa kila baada ya muda fulani mahusiano yako ya urafiki/uchumba yakikaa huwa yanavunjika.

Unaweza ukapata bahati ya kuambiwa shida yako na aliyekuacha, baada ya kukuonya mara nyingi huko nyuma, ama unaweza kuachwa kimya kimya bila kuambiwa shida yako ni nini.

Ukiwa kama mke, unaweza kuharibu ndoa yako kwa sababu hii, "kelele/makelele" kwa mume wako. Hasa ukiwa umeolewa na mwanaume ambaye hajasimama vizuri kwenye imani, na ambaye hajaokoka.

Ni rahisi sana mwanaume kuchoshwa na mke mwenye makelele/kelele, na kutoka nje ya ndoa yake. Sio njia ya kumaliza tatizo ila kwa mwanaume ambaye hajaokoka kwake haiwezi kuwa tabu kufanya hivyo.

Tunaweza kulalamika sana kuhusu waume zetu wanaochelewa sana kurudi nyumbani ila ukweli ni kwamba, kelele zetu ndio zinawafanya waume zetu waone ni heri kuchelewa nyumbani, kuliko kuwahi nyumbani ukakutana na kelele zisizo na mwisho.

Japo kuchelewa nyumbani hakuwezi kuondoa tatizo, wanaume wengi huona njia hiyo inawasaidia wao kuepuka kelele za wake zao. Sasa huko nje huwezi kujua huyu mwanaume anashindia wapi.

Ndio maana wanawake wengi huanza kuhisi vibaya waume zao, kwa kuwaambia wana wanawake wengine nje. Si unajua kusingiziwa kila siku kitu ambacho hukifanyagi huwa inauma na mtu mwingine inaweza kumwathiri. Na kuamua kufanya kweli, hasa kwa yule asiye na hofu ya Mungu ndani yake.

Kelele zisizoisha ndani ya ndoa zinaweza kuharibu kabisa ndoa ile, wawili hawa wanaweza kuonekana kwa nje wapo pamoja ila ukweli humo ndani hawapo pamoja.

Hebu tuangalie maandiko matakatifu yanasemaje kuhusu hili, huenda umepata ukakasi wa hili fundisho kutokana na kichwa cha somo hapo juu.

Rejea: Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu.MIT. 9:13 SUV.

Mwanamke yeyote anayepiga sana kelele ni mpumbavu, na ni Mjinga, yaani ana sifa zote mbili, ya upumbavu na ya ujinga. Tena andiko likaongeza mkazo zaidi, HAJUI KITU.

Kwa lugha nyingine mwanamke wa namna hii, huwa mjuaji sana, kila kitu yeye anajua, yupo juu kwa kila kitu, kujishusha kwake ni hakuna. Mume wake hakuna anachoweza kuzungumza akaeleweka, yeye ni anachojua sana ni kelele.

Wanawake wa namna hii, huwa wanakimbilia wapewe haki SAWA, yaani 50 kwa 50, si unakumbuka ni kwa sababu HAWAJUI KITU! Ni andiko limesema hivyo, wanaojua kitu hawezi kupigizana hizo kelele.

Rejea: Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.1 KOR. 11:3 SUV.

Kichwa cha mwanamke ni mwanaume, na sio kichwa cha mwanaume ni mwanamke... huu sio ukabila. Maana kuna watu hawachelewi kusema huo ni ukabila/utamaduni wa watu fulani, hili ni andiko ndani ya Biblia.

Wanawake mtaponya ndoa zenu wenyewe, acheni kelele ndani ya nyumba zenu, ndoa inajengwa kwa hekima ya kiMungu iliyo ndani yako. Si kwa kelele zako ndani ya nyumba.

Rejea: Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe. MIT.14:1 SUV.

Wasiosikia, endeleeni kuzibomoa ndoa zenu wenyewe huku mkilalamikia wanaume, utasema wewe hujui tu ninayoyapata, kwani wakati unaolewa naye hukujua hayo. Si hadi kuna watu walikuja kukunasua ukaona wanakufuatilia maisha yako! Basi tulia, acha kelele.

Tena tabia yake mbaya ulikuwa unaiona kwake ukasema Mungu atambadilisha akiwa ndani ya ndoa, kwa hiyo Mungu ameshindwa hiyo kazi? Jibu ni kwamba, ujuaji wako, upumbavu wako, Ujinga wako, na kutokujua kwako ndio kulikuingiza kwenye mahusiano yasiyo yako. Acha kelele.

Turejee kwa Mungu.
Samson Ernest.
+255759808081.
 
Back
Top Bottom