Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,438
Kila mtu anapenda kufunga ndoa na kuwa na familia. Bahati mbaya kwetu wanawake ni mwanaume anaefanya maamuzi kuwa huyu ndiye ananifaa katika safari ya maisha.
Hapa hakuna formular wengine watapenda binti mzuri, wengine wanapenda kwasababu ni kabila moja, wengine wanapenda msomi ni mambo mengi.
Unakuta dada amemuona mkaka na amempenda, anajiwekea kabisa huyu lazima anioe . Anaanza kumfulia nguo, kusafisha nyumba yake kumpigia. Ukiwa unafanya yote hayo pia angalia uhusiano wenu una afya gani. Usiwe wewe wa kufua na kupiga pasi wakati hata kwa marafiki zake hakutambulishi.
Basi kuna mmoja wakati amemaliza kupiga pasi nguo za ‘honey wake’ anaziweka kabatini alikutana na engagement ring. Akijua hii nitavalishwa mimi, acha ajiongeze kwa mwanaume Yule.
Kumbe pete ile jamaa aliinunua amvishe mpenzi wake aliyepanga kumuoa huko siku za badae. Pale alikuwa anapoteza muda tu akimsubiri mtarajiwa wake.