Ndoa ya Joseph Mbilinyi (Sugu) yavunjika, mkewe amlilia

Ndoa ya Joseph Mbilinyi (Sugu) yavunjika, mkewe amlilia

Ni yule aliyefanya vituko kwenye Sherehe yake ya kuzaliwa?
 
Hapana sugu alimwambia anatamani mtoto na bint nae alikuwa na hamu ya mtoto ndiyo yakatokea hayo
Cc Emaroli
 
Last edited by a moderator:
Faiza aluolewa lini na sugu????

Mtu mwenyewe alivaa pampaz kwenye bday yake
 
Sugu mvuta bange hawezi tunza mtoto. Ampeleke ustawi wa jamii
 
Fresh acha kuisimanga bangi bwana
 
Last edited by a moderator:
Halafi huyu mwarabu au? Kama mwarabu stoshangaa kuskia kaishia darasa la.7 au form 3 maana wale hupelekwa skuli wakue kisha waolewe. Wanaume hupewa malori waendeshe ndio maisha yao

Bas kashindwa kupata mlanho.kariakoo afanye kama waatabu wenzake aende Maskati na debei akanunue ma dira ya kuuza Dar?

wagalatia hamuishi vituko, sasa wewe ambae sie mwarabu na umefika chuo kikuu mbona kuandika hujui?
 
bora Sugu kampiga chini kama hawezi tofautisha mavazi huko nyumbani ilikuwaje? Leo anaenda kwenye birthday yake na pumpers kesho atavaa bandage nadhani hata kupika wakati mwingine inawezekana alikuwa anapikia chooni ni kimeoooo
 
bora Sugu kampiga chini kama hawezi tofautisha mavazi huko nyumbani ilikuwaje? Leo anaenda kwenye birthday yake na pumpers kesho atavaa bandage nadhani hata kupika wakati mwingine inawezekana alikuwa anapikia chooni ni kimeoooo

mastaa wa bongo muvi hawapiki
 

attachment.php

Hii ni aibu ya kaka sugu bora alivyoachana naye....akili hana huyu
 
Aliyekuwa mke wa mbunge wa Mbeya mjini Faiza Ally amelalamika
kuwa Mheshimiwa Mbunge Sugu ametelekeza mwanae hatoi huduma
yoyote ile kwa muda wa mwaka mmoja sasa.

Akiongea kwa uchungu mkubwa kupitia kipindi cha Take One cha Clouds Tv
amedai kuwa Sugu amekuwa hataki kupokea simu yake, kipindi cha nyuma
alikuwa akitumiwa simu alikuwa anaijibu labda baada ya siku mbili.

Akitumiwa picha za mtoto wake ili aone maendeleo yake alikuwa hajibu lolote,
akazidi kueleza kuwa wanaosema kuwa ameachana nae sababu ya mavazi
yake ni uongo kwani Sugu alimfahamu yeye kupitia FACEBOOK.

Yaani mh. mbunge alimuona Faiza kwenye facebook ndipo alipomtongozea
na kumuoa. Inaonyesha huyu mbunge wa Mbeya ni tabia yake kutongoza
wanawake kwenye facebook na hivi sasa atakuwa ametongoza mwingine.

Sugu ameshindwa kulea mwanae wa kumzaa, je? wananchi ataweza?

BY: SUPU YA MAWE

Na atakae muoa mwingine nahisi atatokea humu jf...hhahhaaaaaaaa
 
Last edited by a moderator:
“Asante sana Naibu Spika, naomba
nitoe maelezo binafsi jana tarehe 25
June 2015, Mbunge Martha Mlata
alidai kuwa kuna Mbunge wa
CHADEMA amempora mwanamke
mmoja mtoto mdogo wa miaka miwili
na amempora wakati Mbunge huyo
amekuwa hatoi matunzo kwa mama
yake… Mlata aliwataka Wabunge wote
wanawake kuungana kukemea kitendo
alichodai kimefanywa na Mbunge
huyo”
“Hakutaja jina la Mbunge
aliyemhusisha na madai yake ila alidai
kuwa ni msanii mwenzake… hata
hivyo alitaja jina la mwanamke
anayedaiwa kunyang’anywa mtoto
kuwa ni Faiza. Mbunge aliyelengwa na
mashambulizi ni mimi Joseph Osmond
Mbilinyi, mimi ndiye baba wa mtoto
Sasha Desderia Mbilinyi anaedaiwa
kuporwa kwa mama yake, na Faiza
aliyetajwa ni Faiza Abdallah Ally
ambaye ni mzazi mwenzangu na
mama mzazi wa Sasha Desderia“
“Watu wazima hawapendelei
kuzungumzia mambo binafsi
hadharani… Nadhani sitakosea kusema
hata Mheshimiwa Martha mwenyewe
asingependa kuzungumzia matatizo
yaliyopelekea ndoa yake kuvunjika“

“Mimi ni mmoja wa watu wazima
wenye akili timamu ndio maana
sijazungumzia hadharani kuhusu
uhusiano wangu na mzazi mwenzangu
Faiza Ally na mtoto wetu Sasha…
Sasha ameishi na mama yake tangu
alipozaliwa mwaka 2012, katika kipindi
chote nimempelekea mama yake laki
tano kila mwezi, nimemlipia ada ya
shule Milioni 3 kila mwaka
.. Mlata
kama angekuwa anataka kujua
angeniuliza ningempatia taarifa hizi
kabla hajarusha tuhuma nzito“
“Mwanamke anayedaiwa kuwa
mnyonge anajulikana katika kumbi za
starehe nchi nzima, picha zake
zilisambazwa katika Mitandao ya
Kijamii na kuleta fedheha kubwa kwa
watu wanaojali maadili ya mavazi,
picha zake nyingine akiwa amevaa
diapers zilisambaa mitandaoni na
Martha Mlata angeweza kupata ukweli
wa mambo haya kabla hajarusha
tuhuma mbele ya Bunge“
“Nilienda Mahakama ya Mwanzo
Manzese, niliwasilisha ushahidi
kwamba mzazi mwenzangu
asingeweza kumlea mtoto.. Mahakama
ilimwita akajitetea, June 23 Mahakama
iliridhika na ushahidi wangu, ikaamua
mtoto akabidhiwe kwangu ili nimlee.
Kilichodaiwa kuwa ni uporaji wa mtoto
kiukweli ni amri ya Mahakama, Mlata
hakuwahi kuonekana Mahakamani,
nina mashaka hata kama
anamfahamu mtoto mwenyewe au
mama anayemwita mwanamke
mnyonge“
“Mashauri haya hayakupaswa
kuwekwa hadharani kama alivyofanya
Martha Mlata… Nimesikitishwa na
Martha Mlata kuzungumza mambo
binafsi. Pamoja na Mahakama kunipa
haki, mtoto bado yuko kwa mama
yake kwa sababu mimi ni mstaarabu…
nimetoa nafasi ili Majadiliano ya
kifamilia yafanyike… Naomba mjadala
huu usiendelee zaidi ya hapa” .
Mbunge Joseph Mbilinyi alimaliza.
 
Back
Top Bottom