Aliyekuwa mke wa mbunge wa Mbeya mjini Faiza Ally amelalamika
kuwa Mheshimiwa Mbunge Sugu ametelekeza mwanae hatoi huduma
yoyote ile kwa muda wa mwaka mmoja sasa.
Akiongea kwa uchungu mkubwa kupitia kipindi cha Take One cha Clouds Tv
amedai kuwa Sugu amekuwa hataki kupokea simu yake, kipindi cha nyuma
alikuwa akitumiwa simu alikuwa anaijibu labda baada ya siku mbili.
Akitumiwa picha za mtoto wake ili aone maendeleo yake alikuwa hajibu lolote,
akazidi kueleza kuwa wanaosema kuwa ameachana nae sababu ya mavazi
yake ni uongo kwani Sugu alimfahamu yeye kupitia FACEBOOK.
Yaani mh. mbunge alimuona Faiza kwenye facebook ndipo alipomtongozea
na kumuoa. Inaonyesha huyu mbunge wa Mbeya ni tabia yake kutongoza
wanawake kwenye facebook na hivi sasa atakuwa ametongoza mwingine.
Sugu ameshindwa kulea mwanae wa kumzaa, je? wananchi ataweza?
BY:
SUPU YA MAWE