Mwanamume huyo aliamua kufanyia watoto wake wanne uchunguzi wa DNA baada ya kuanza kumshuku mke wake
- Ripoti ya uchunguzi huo ilionyesha kuwa ni baba halisi ya mtoto mmoja pekee kati ya wanne ambao aliwalea pamoja na mke wake kwa miaka 24
- Mke wake alikiri kuwa bosi wake ndiye baba ya watoto watatu wa kwanza
Tafakari haya, baada ya miaka 24 ya ndoa, unagundua kuwa watoto watatu kati ya wanne ambao umekuwa ukiwalea pamoja na mke wako si wako halisi.
Ndoa ya miaka 24 yavunjika baada ya mume kutambua watoto 3 si wake.
Japo visa hivi hutokea kwenye filamu pekee, jamaa mmoja ambaye alikumbana na hali hii alithibitisha kuwa mambo haya ni ya kweli.
Kupitia kitandazi cha Twitter, Khasakhala almaarufu Julius Mmasi aliwaacha wanamtandao vinywa wazi baada ya kufichua kuwa rafiki wake wa karibu alilazimika kuvunja ndoa yake ya miaka 24 na mke wake baada ya matokeo ya DNA kubainisha kuwa ni baba halisi wa mtoto mmoja pekee kati ya wanne ambao aliwalea pamoja na mke wake.
Jambo la kuhuzunisha zaidi ni kuwa mke wake alikiri kuwa bosi wake ndiye baba ya watoto watatu wa kwanza
Mwanamume huyo aliamua kufanyia watoto wake wanne uchunguzi wa DNA baada ya kuanza kumshuku mke wake.
Kwa uchungu mkubwa, aligundua kuwa mabinti wake watatu ni watoto wa bosi wa mke wake huku kitinda mimba ambaye ni wa kiume ndiye mtoto wake pekee halisi katika ndoa hiyo.
"Watoto watatu wa kwanza wa kike, wawili walishamaliza tayari kidato cha nne mwingine yuko kidato cha nne. Mke wake alikiri kuwa watoto watatu wa kwanza ni wa bosi wake.
Utamshauri nini mtu kama huyu ?"