Ndoa ya Mrema ni batili, Mjane ana ndoa nyingine halali

Hata kama nia ilikuwa mali kumbukeni kamsaidia sana Mrema siku zake za mwisho, ugonjwa na uzee, nyie mlikuwa wapi kupinga hiyo ndoa wakati Mrema akiwa hai? malizaneni kistaarabu, tumieni court itawapa haki zenu na yake sio kuchafuana
Unajuaje alimsaidia sana? Leta evidence zako
 
Ndoa ya Doreen mbona ilikuwa ya public kila mtu aliijua. Na pia mara kadhaa alikuwa akihojiwa na mahojiano yake yaliwekwa wazi mitandaoni.

Sasa huyo mume wake alikuwa wapi siku zote mpaka ajitokeze leo baada ya Mrema kufariki?
Raia mwema wanasema mume wa huyo Doreen hakujua anaolewa mpaka siku aliyoolewa na alijua kama mimi na wewe kwenye media ndoa imefungwa.

Hapa nahisi issue ni je kisheria na kwa imani ya katoliki je ndoa ipo au haipo?
 
yule ni mwanamke mrembo na anahisia kama wengine ni mzuri wa sura na ukimuangalia vizuri anaonekana ni mtamu sana! Kwa hiyo mtoa mada ulitaka asipendwe? Changamoto alizopitia kwenye ndoa yake ya kwanza unazijua? Habar ya majina yake wewe ndio baba yake?hata mm nampenda akinikubalia nitafunga nae ndoa!
 


Wewe ni mtoto wa Mrema ama Ndugu wa Mrema. Mbona huyu mke wa Mrema unamwanzishia uzi nyingi sana
 
Wapi nimesema kuwa nina uhakika? Kama nyie mlikuwa na uhakika kuwa alikuwa anamtesa mngempeleka ustawi wa jamii au mahakamani. Hilo la kujutia ndoa ni la kawaida tu. Sio uthibitisho wa kuteswa. Huo unaoona kuwa ni ushahidi wako hauna uzito maana haujathibitisha kuwa mjane wa Mrema ndio huyo unayemtuhumu kuwa aliwahi kuolewa kabla. Mpaka sasa ulichoweka ni umbea tu.

Amandla...
 

Unampenda una hela za uhakika? Usijihaibishe kaka
 
Itabidi muachane kwa kufuata tarat8bu xa kuvunja mkataba wenu mlioingia msikitini au kanisani. Ila kwa kanisa katoliki sahau kuhusu kukubaliwa na kupewa hati ya talaka. Hiyo contract ni until death not otherwise...
 
Kwamba huyo mwanamke anayeonekana hapo kazaliwa mwaka 1984, mmmh!!
 
Unataka ushahidi gani kama mume halali anasema ni mke wake na cheti kipo registered RITA.

Na kanisa waliofunga ndoa linatambua ndoa yao?

Wewe utakuwa Doreen wewe si Bure.
 
Doreen asichafuliwe. Apewe haki zake kama mke/mjane halali wa Mrema. K yake imetumiwa na Mrema hivyo ni shururuti apate mgawo wa mali za Mrema
 
Doreen asichafuliwe. Apewe haki zake kama mke/mjane halali wa Mrema
Sheria inatambua vipi mke/mjane halali?

Na je bwana Fredrick Mushi akifa pia Doreen atakuwa mjane?
 
Unataka ushahidi gani kama mume halali anasema ni mke wake na cheti kipo registered RITA.

Na kanisa waliofunga ndoa linatambua ndoa yao?

Wewe utakuwa Doreen wewe si Bure.
Ndoa imetangazwa kila mahali na picha ya Doreen zimewekwa wazi. Huyo Fredrick alishindwa nini kwenda Mahakamani kumdai huyo unaesema alikuwa mke wake? Kwa nini hakwenda hata kwenye kanisa walikofungia ndoa na kuwaambia kuwa huyo waliyemfungisha ndoa alikuwa mke wake? Mtu amekufa ndio mnaleta za kuleta.

Na unaonekana una chuki binafsi na huyu Doreen. Tangu lini umesikia mali ya marehemu anarithi mke ambae alimuacha au aliishafariki? Mali zote za marehemu alizokuta Doreen ni haki yake pamoja na watoto wote wa marehemu. Mngekuwa mnampenda sana marehemu mngemshauri waingie na mkataba wa prenup na Doreen kabla ya ndoa. Au aandike kabisa will yake mapema.

Kwa hivi ilivyo imekula kwenu. Na msipoangalia mtafunguliwa mashtaka ya kumchafua Doreen.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…