Hapa ishu ni kwamba kwao ni karibu sana na sehemu yake ya kazi ndugu yangu,kuepusha usumbufu niliona ni vyema akae kwao kwa mda.mimi kwetu ni mkuranga.sasa kutoka mkuranga mpa UDSM ni mtihan
Anaingia kazini saa ngapi?mimi naishi mkuranga na familia yangu,mwanangu anafanya kazi masaki kila siku ananenda kazini kutokea nyumbani mkuranga.Najua anachoka sana lakini kumruhusu mkeo basi siku mbili alale mjini kwao sidhani angesema anachoka.
Kuhamia mkeo Dar akaishi kwao ndio kaburi la ndoa yako.Ndugu,wakwe na bwanazake wa ujanani wakashona sanda.Wanawake wakiwa na kipato kumshinda mwanaume wanakuona kama mnyonyaji na huijali familia.Wazazi wa mke kama wako wanaoona wewe ni mzigo kwa mtoto wao,lakini ingekuwa mke anakutegemea wewe kama housewife wangeitisha vikao vya kukusema unaharibu ndoa ujirekebishe,lakini hapa inaonekana wao wanaona ni sahihi na baba yako hawezi kuitisha kikao cha usenge kama huo.
Hata tukushauri nini,u r the decision maker,na hapa u will have to make a very tough decision.Ningekuwa mimi ningekubali alichosema na kukaa pembeni,mapenzi hayalazimishwi hata kidogo.Kuna Muda huwa tunadhani kulipigania penzi ndio ukamilifu wa mahusiano,lakini ninasema kuna muda wa kuliachia penzi hata kama kuliachia kuna maumivu makubwa kiasi gani.Ukimuacha mtu unayempenda kwa dhati aende huwa unahisi a part of your heart is being torn out lakini kumbe ukiendelea kumng'ang'ania mtu huyu your whole heart will be ripped open sooner or later.
Ushauri wangu kwako, la kwanza kwa vile unaumwa angalia afya yako ili uiimarishe then ndani ya muda wa kujiimarisha kiafya digest the news za kuachana. mwisho umuulize hatma ya watoto wenu,Imagine mpenzi wako akuambie muachane alafu umpe jibu la straight kuwa nimekubali kuachana!Tafakari ndugu.
Mwisho,mlifunga ndoa au sogea tuishi?Kama mlifunga ndoa ni kwa dini gani?
Pole kwa kuumwa,pole kwa kupitia unayopitia lakini hakuna refu lisilokuwa na mwisho,Muda kupita ni tiba ya matatizo kama haya.