Ndoa za ndugu kwa ndugu kama hii ya Waarabu wa Tanga, ni sahihi ama si sahihi?

Ndoa za ndugu kwa ndugu kama hii ya Waarabu wa Tanga, ni sahihi ama si sahihi?

MKATA KIU

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
3,410
Reaction score
8,184
baa1bb0ca5874d05b45c5e0976a51856.jpg
 
Hapo wewe ndio huelewi.Hiyo Mgeituf ni kabila sio jina la ukoo.Waarabu huwa wanatumia sana mwisho wa majina yao,kuandika kabila la kiarabu,wengi hawafahamu kuwa waarabu ni kusema kama mwafrika,halafu hao waarabu wana makabila ,kama msukuma,mchaga,mdigo,msambaa,ni kama kuamdika Hemed Ali Shemfuko,huyo ni.
msambaa,kwa hiyo inakuwa wepesi kujua ni wa kabila gani.Kwa waarabu unaweza kuona wanatunia Bahoza,Bakheresa nk,unajuwa hawa ni kabila lipi.Mwaweza kuwa kabila moja lakini msiwe ndugu.Ni sawa wakabila la msambaa,wote wawe wasambaa na majina yafanane,lakini sio ndugu.
 
Hapo wewe ndio huelewi.Hiyo Mgeituf ni kabila sio jina la ukoo.Waarabu huwa wanatumia sana mwisho wa majina yao,kuandika kabila la kiarabu,wengi hawafahamu kuwa waarabu ni kusema kama mwafrika,halafu hao waarabu wana makabila ,kama msukuma,mchaga,mdogo,msambaa,ni kama kuamdika Hemed Ali Shemfuko,huyo ni.msambaa,kwa hiyo inakuwa wepesi kujua ni wa kabila gani.Kwa waarabu unaweza kuona wanatunia Bahoza,Bakheresa nk,unajuwa hawa ni kabila lipi.
Waarabu kama wapare .
Wapare nao huchukua ubini ktoka eneo wanalotoka.Mfano Msangi ninwanaotokea Usangi,Mgweno anayetokea Ugweno, Mchome anayetokea Chome nk

Hivyo waweza shangaa kijana wa kiume Msangi anao binti meenye la ukoo Msangi pia

Kifupi Waarabu na wapare akili kichwani hamna
 
Hilo sio swala la waarabu bali ni UISLAM ndio umeelekeza hivyo.

Haramu ni mama yako, watoto wa dada/kaka yako, shangazi zako,bibi yako, mama zako wadogo na wakubwa.

Nje ya hapo ni halali, watoto wa baba mkubwa na mdogo unaoa bila ya shida yoyote, mtoto wa mjomba ako (binamu) unaoa vizuri tu.
 
Waarabu kama wapare .
Wapare nao huchukua ubini ktoka eneo wanalotoka.Mfano Msangi ninwanaotokea Usangi,Mgweno anayetokea Ugweno, Mchome anayetokea Chome nk

Hivyo waweza shangaa kijana wa kiume Msangi anao binti meenye la ukoo Msangi pia

Kifupi Waarabu na wapare akili kichwani hamna
UISLAM ndio umehalalisha
 
MUNGU AJAACHA KITU KATIKA QURAN..ameelezea kuhusu hili jambo

Maharimu ni wanawake na wanaume walioharamishwa kuoana kutokana na ukaribu wa nasaba kama ilivyobainishwa katika Qur-an na Sunnah. Wanaume wa Kiislamu wameharamishiwa kuwaoa wanawake wanaobainishwa katika aya zifuatazo:


"Wala msiwaoe wake waliowaoa baba zenu; isipokuwa yale yaliyokwishapita. Bila shaka jambo hili ni uovu na chukizo na ni njia mbaya (kabisa). Mmeharamishiwa (kuoa) mama zenu, watoto wenu, dada zenu, shangazi zenu, ndugu za mama zenu, watoto wa ndugu zenu, watoto wa dada zenu, na mama zenu waliowanyonyesheni, na dada zenu wa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu, walio zaliwa na wake zenu mliowaingilia. Lakini kama nyinyi hamjawaingilia basi si vibaya kwenu (kuwaoa). Na mmeharamishiwa wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu. Na (mmeharamishiwa) kuwaoa madada wawili wakati mmoja, isipokuwa yale yaliyokwisha pita. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kurehemu na Mwenye kusamehe. (4:22-23)


"Na pia mmeharamishiwa wanawake wenye (waume zao) isipokuwa wale iliyowamiliki mikono yenu ya kuume. Ndiyo Sheria ya Mwenyezi Mungu juu yenu. Na mmehalalishiwa (kuoa wanawake) minghairiya hawa..." (4:-24)
 
Quran 4:22-24

Aya hizi zinabainisha wanawake walioharamishwa kuwaoa kuwa ni hawa wafuatao:

1. Mwanamke aliyepata kuolewa na baba yako, (babu yako, baba wa baba yako - wa kuumeni na kikeni).
2. Mama aliyekuzaa (babu aliyezaa waliokuzaa, mama wa bibi aliyezaa aliokuzaa...).
3. Binti yako uliyemzaa (au binti aliyezaliwa na uliyemzaa...). Pia binti wa kunyonya na mwanao (na kikazi chake...).
4. Dada yako khalisa au wa kwa baba au wa kwa mama.
5. Shangazi yako- dada wa baba yako,(na dada wa babu yako...).
6. Mama mdogo; ndugu wa mama yako (au ndugu wa bibi yako...).
7. Binti wa ndugu yako mwanamume, khalisa au wa kwa baba au kwa mama (na kila aliyezaliwa naye).
8. Binti wa dada yako khalisa au wa kwa baba au kwa mama
9. Mama wa kukunyonyesha (na mama zake wa kumzaa au wa kumnyonyesha).
1O. Dada yako wa kunyonya naye (aliyenyonyeshwa na aliyekunyonyesha).
11. Mama yake mkeo wa kumzaa au wa kumnyonyesha (na bibi yake pia wa kumzaa mama yake au wa kumnyonyesha Ama ndugu yake mama yake mkeo yaani mama mdogo wake au shangazi yake wa kuzaliwa au kunyonya; unaweza kumuoa akifa mkeo au utakapomuacha na eda ikaisha.
12. Binti wa mkeo uliyemuingilia (na mjukuu wake...).
13. Mke aliyeolewa na mwanao wa kumzaa au wa kunyonyeshwa na mkeo (na kizazi chake); si mke wa mtoto wa kupanga au mtoto wa kulea.
14. Mtu na ndugu yake pamoja (au) mtu na shangazi yake au mtu na mama yake mdogo pamoja. Akifa mke au ukimuacha na eda ikaisha unaweza kumuoa dada yake, au shangazi yake, au mama yake mdogo.
15. Mke wa mtu, bado mwenyewe hajafa wala hajamuacha ni Haram kumuoa. Wanawake hao wameharamishwa kuolewa na wanaume wanaofanana na hawa kwa upande wa kiumeni.
 
Back
Top Bottom