at last nitalazimika kufanya ngono na beki-tatu kama ''AHSANTE KWA KUNIJALI''.huyu mwanamke atabak analia lia tu mara mumewe muhuni,mara hausigeli muhuni wakati yeye ndiye chanzo
Geof , that is ur mentality en no body can change that other than urself,
Ila nikirudi kwenye mada Kaka Kilambi yuko sahihi baadhi ya maeneo na maeneo mengine anahitaji kusahihishwa kama alivyotanguliza kusema yeye mwenyewe.
maeneo ambayo mie nadhani yuko sahihi pale mama mwenye nyumba anapomwachia maid afue vyupi or boxers za mumewe, amtayarishie maji ya kuoga mumewe( mie naoga na mume wangu kila siku so sio kwamba ntakuwa namtayarishia maji ya kuoga ni kwamba natayarisha maji ya kuoga sote), ila jambo kubwa zaidi nadhani wanawake wengi tunakosea ni kumuachia maid awe mwangalizi wa mtoto uwepo usiwepo mtoto anaumwa maid ndio akumbuke kumpa dawa kisa wewe uko kazini , ukiondoka asubuhi ukirudi nyumbani jioni mtoto kalala wewe hauko concerned , nadhani hapo tunawakosea sana watoto wetu, tunapoteza mapenzi ya watoto wetu kwetu bila ya kujitambua na khamishia hayo mapenzi ya mtoto kwa maid. kuna wazazi wengine huwa wananchosha pale wanapojisifia mbele za wageni 'mhhh mwanangu mie hata hanitaki anampenda dada yake tu hata nikirudi kazini hanijali' for me i see this mama is stupid coz anajisifia ujinga .
jamani tukubalini ukweli kwamba sometimes nature inatubeat no matter how much we want to try, huuu usawa tunaosema utatoka wapi wakati tumetoka kwenye mbavu zao plus tuanze na kurudisha nusu ya zile mahari ili na wao tuwe tumewalipia mahari kama wahindi wafanyavyo.
Don get me wrong sisemi wanawake tunatakiwa tufanye kila kazi anayofanya maid ila kuna zingine ziko private jamani,
ila linapokuja swala la kupika usafishaji wa nyumba (except ma bedroom) hapo tuwaachieni mameid kwasababu kiukweli huwezi kurudi kazini na kunza kupikia familia kila siku (japo famili yangu ndogo en that is wat i do kila siku unless tunadine out ,coz mie napenda kula vizuri na sio michemsho tuu). lakini ni ngumu na hassa kama mwanamke hana hobby na jiko.
pia akina baba wanatakiwa kuwasaidia wake zao leo nimetenga maji mie kesho watenga wewe, ukiona nimepitiwa kufua hizo boxers basi nisaidie mume wangu sina alama usoni kwamba lazima mie ila nafanya kwasababu ya mapenzi na heshima yangu juu yako, na pia watoto kuwafatilia afya na makuzi yao ni kazi yetu sote japo mimi naplay a big part.
Na hiii mentality ambayo wamama wengi tunayo kuwa hawa wasaidizi wetu wa nyumbani ndio wastahili kuachiwa kazi zote nyumbani bila kuwapa muda wa kupumzika , hiii mentality ni ya kitumwa zaidi . na wao ni binadamu kama sie mbona sisi tukiwa maofisini humu tunadai haki zote za wafanyakazi tena kwa maguvu na makelele? ukifanya kazi zaidi ya muda wa kazi wa kawaida tunadai overtime, tukifanya kazi muda wa mapumziko kama sundays tunadai overtime , mbona hawa wasaidizi wetu hatuwafikiriii hata kuwapa masaa mawili ya kupumzika ? hiiii sio fair kabisa na wao ni binadamu wanahitaji kuhurumiwa, plus na hiyo mishahara tunayowapa ndo kabisaaaaaaaaaaaa