NDOA: Zamani vs Siku hizi


Swahiba/.... wakati wewe unajiandaa kuwasha mshumaa,

Mie nawasha tochi kabisa kuupa heshima yote mwaka 2011... A YEAR THAT WAS/IS, which has been the most exciting year in my life, positively, negatively and every between

My response to this (yet another platinum release) thread of your ni kama ifuatavyo;
Ndoa za zamani hazikua na mikito ya sasa, lakini nazo zilikua na misukosuko yao... waweza pata hayo kuanzia nyimbo za enzi ya shingo ya upanga, moyo wangu, dereva fanya upesi, nalia na moyo, usiondoke you name it; whatever we experience now, ilikuwepo but in a different density
tuonacho sasa ni kuendana tu na kukua kwa technology na knowledge among us (of course with unfortunate muanguko wa wisdom kidogo

KUFUPISHA... MPOROMOKO WA KISASA UNACHANGIWA NA YAFUATAYO
akina mama kujua haki zao zaidi
power of knowledge and alternative life style ambazo zamani zilikua hakuna
public flexibility
Mwisho kabisa ni ile necha ya binadamu kuendelea kuvumbua alternatives, tunaona haki za ndoa za jinsia moja, sayansi hasa IT ilivyoweza kufumua mambo ya tabia na vichocheo vya mwili ambavyo havikuwepo, utundu wa asili wa binadamu na pia ile nafasi ya mwanaume kuwa neutralized na vitu kama ajira, shule, sinema, redio nk... (i guess zamani mume/mke alikua ndio source primary ya habari, mbinu mpya na kila kitu

sometimes huwa nawaza, je Yesu au Mtume Muhammad (SAW) wangekuwepo enzi hizi za twitter, facebook, JF, satellite nk wangekua wana hali gani??? kwani hata akipiga ushuzi tu, dunia itajua

In short current world is dynamics and people have more options than just a MARRIAGE.... AND MARRIAGE IS SLOWLY TURNING INTO "JUST ANOTHER OPTIONS FOR LIVING A COMFORTABLE LIFE"

nakuacha na swali: Kama sio uchoyo wa watawala wa mwazo (werevu) ndoa ingekuwa nucleus ya human reproduction?
 
mkuu hapo umewaza,na sio kujua haki zao tu,pia wanatetewa
 
women empowerment ndo inawatetea na kutukandamiza sisi wanaume

Hahahahhaha!!Eti mnakandamizwa!!
Mnakandamizwa vipi vile?Na kama kweli mnakandamizwa na hamfurahii, kwanini mnataka nyie ndio muwakandamize wanawake?Ina maana wanawake wao ndio wanaona raha kukandamizwa? Kama wote tungekua tayari kutendea upande wa pili haki ni kiasi cha kutafuta balance hapo katikati badala ya kuwa na mawazo ya "haki za mwanamke zinanikandamiza mimi".

Kitu kikubwa kinachotakiwa na hizo haki ni HESHIMA KWA MWANAMKE.Wewe kama mwanaume ukiwa tayari kumheshimu mkeo kama mkeo, kumpa nafasi ya kua mke/mpenzi na rafiki badala ya kumtreat kama mtoto au kijakazi matatizo mengi yangeepukika. Sema sasa kaka zangu naona hizo haki mmezitilia maanani, mmeziongeza na ukubwa alimradi tu muonekane haziwatendei nyie haki.

Binafsi sizilaumu hizi haki isipokua pale mwanamke anapokua limbukeni about it. Nyie jaribuni kuwa reasonable (kama umempata ambae sio limbukeni) uone maisha yatakavyonoga.
 

Hivi Mbu hizo sheria zinamsaidia mwanamke kwasababu tu ni mwanamke au kwasababu anakua anastahili?

Kwanini mnalalamika sana kwamba hizi mpya zinawanyanyasa nyie wakati za zamani ziliwanyanyasa wanawake zaidi? Kwanini msikae chini na kutafuta balance badala ya kutaka nyie ndio muwe wanyanyasaji? Usipompa mtu sababu, hatokua na sababu.Huwezi kuwa mwanaume mnyanyasaji alafu mke akaamua kukuacha na sheria ikamuunga mkono alafu wa kulalamika ukawa wewe.Heshimu uheshimiwe, tenda haki utendewe haki. Hapa naona ubinafsi ndio unaotawala zaidi, ile dhana ya "kwanini mimi ndio ninyanyasike" ndio inayochangia ndoa kutofika popote.Anzeni kufikiria "kwanini tunyanyasane" muone kama hakutakua na mabadiliko.
 
Hahahahaha, kwahiyo tatizo lipo kwenye kuolewa tu?Kama haolewi anaweza kwenda nae?

Uzuri hapo sheria ipo upande wa mtoto zaidi (sio mwanamke) na inampendelea kwa kumwacha aishi na mama yake ikiwa mama yake ni capable. Sasa wewe akikuachia utamnyonyesha?Utaacha kazi ukae nae nyumbani au unamtafutia mama wa kambo /hausigeli afanye kazi ya mama mzazi wakati mama mzazi yupo hai and capable?
 
Ndoa is a two way street, ila kwa ubinafsi (bora ninyanyase mimi kuliko ninyanyaswe) baadhi ya watu wanataka kuifanya one way street.Mwenzi atangulie mbele wao nyuma kufuatilia na kumuendesha. Hata ikimbidi kugeuka na kurudi nyuma unamzuia kwasababu uko kwenye nafasi ya kufanya hivyo. Badala ya kumlazimisha mtu aendelee kuwepo kwanini nguvu msiweke kwenye kumshawishi taratibu na kumpa sababu za kuendelea kuwepo? Msipobadilika nyie kama wanaume inabidi tuandike hasara linapokuja swala zima la ndoa, kubalini mabadiliko and make the best of it badala ya kuona hamtendewi haki kwakua mmenyang'anywa haki ya kunyanyasa.

Yani kwa vyovyote vile, mmoja akifikia kujiona bora kuliko mwenzake, akaona yeye ana haki kuliko mwenzake kiwango cha kufanikiwa pamoja nacho kinashuka.
 
Marriage is no longer linked to comfortable life mkuu! Ndo haswaa maana ya moskwito! Walio kwenye ndoa wanalalamika kila kukicha, hadi walioko single hawatamani kuingia ndoani tena! Ukiskia dunia hadaa ulimwengu shujaa ndo hii sasa!
AND MARRIAGE IS SLOWLY TURNING INTO "JUST ANOTHER OPTIONS FOR LIVING A COMFORTABLE LIFE"
 
Mbu,
Mostly sababu za mambo kuwa kama yalivyo nadhani zimejadiliwa sana (nakiri sijapitia uzi, unakimbia ka nshale!). In my opinion:
1 wanawake wanajitambua. Haki mnazolalamikia wanapewa zimewasaidia kujitofautisha na wanyama kazi na punching bag (japo nna jirani anapigwa na bf kila siku, nimemshawishi amuache nimechoka. Ntamleta jf,kha!)
2 woga wa unyanyapaa umetuisha. Zamani zile ilikuwa ukiachika unakuwa najisi kwenye jamii nzima. Siku hizi hata mwanaume akikukuta bikira anakudharau manake anataka mwanamke mzoefu. I guess mwanamke aliyeachana na mume ni better candidate (source: The Boss)
3 uwezo wa kifedha.. Hatuogopi tena maisha. Kuna wanawake wana-support familia mume included! Kuna mwanaume miaka nenda miaka rudi anaishi na mke na wanae kama yuko gesti hausi isiyo na hata kodi ya pango. Sasa mke akiona tu mambo ndivyo sivyo anakufukuza kwanza manake waishi kwake.
4 hali halisi: kuna magonjwa ya kuambukiza kama ukimwi, so cheating is unacceptable. Lifestyle diseases nazo kama presha na visukari zinatufanya tuepuke stress zisizo za msingi.
5 options nyingi: MTM ameongelea source za habari enzi hizo. Mume aende kilabuni, mama aende sokoni warudi wapige umbea wote kama Al-jazeera! Tuongelee mfumo uliopo hata wa sex! Mume ana-cheat, mke ana-cheat! Smile anapewa kila atakacho kuanzia ridhiko la mwili, la fedha, kampani na ana hadi miscellaneous bf! Sasa inakua shida juu ya nini? Sijui kama nimeeleweka!
6 lack of responsibility kwa wanaume: niseme tu wanaume wa siku hizi hawana nidhamu ya ndoa aisee! Jitu haliwezi hata kutunza wanae, kutwa kukimbizana na wanawake wa nje, halafu ndo show full time na dharau nyumbani. Anatoka small house anarudi kwake na kisirani (huku anadai anapewa faraja, sasa sijui uchachu wa nini?!).
Ntaishia hapa kwa sasa, ila just stressing on last point, matatizo ya ndoa yalikuwepo toka enzi. I know a couple baba ana watoto nje, mama ana watoto nje (lol, manake sio wa ndani ya ndoa). Wamepishana uzuri kama matawi ya mwembe! Lakini ndoa wanaiendeleza mwanawani manake ndo mfumo waliochagua. Ila wanaume wetu siku hizi, anazaa nje kwa mbwembwe, halafu akikuta sms ya ku-flirt tu kama sio kipigo ni talaka!
 
Hili li uzi limekimbia sana asee,
Na wengi wamesema sidhani kama mheshimiwa moskwito anahitaji notes zaidi....
Labda ODM aongeze hivi:

Pamoja na facts walizozitaja wadau huko juu, ndoa za zamani zilidumu kwa sababu ya kitu "Kuwekeana heshima". Kwamba zamani ili mtu aoe wazazi walihusishwa kikamilifu. Yaani kwamba wazazi wangu wanakuwa wanajuana na wazazi wa Lizzy. Wanaongea na wazazi wa Lizzy. Wanakubaliana Lizzy na ODM waoane. ODM anamuoa Lizzy na kwa sababu ya heshima za wazazi wao, hata kikitokea kutokuelewana basi wanavumilia machungu ili ndoa yao kustawi na kutowavunjia heshima wazazi wao. Uthibitisho wa hili utaliona kwenye namna ya ndoa za zamani zilivyokuwa....asilimia kubwa zilihusisha watu wa kijiji/mji mmoja, kabila moja na dini moja.

Sasa hizi ndoa zetu za sasa.... haiyumkiniki wazazi kutambulishwa mchumba, tayari kibinti kina mimba ya miezi kadhaa. Yaani wazazi wanafanywa kutambulishwa tu si kuhusishwa katika mchakato mzima. Kwa mantiki hii basi, namna ya urahisi wa kufunga ndoa ndivyo ulivyo urahisi wa kuvunjika...who cares?...... Tumekutana kimjini mjini, tuachane kimjinimjini....

Mengine yanayochangia ndoa za kisasa kuwa zimamoto ni kama:
Teknolojia
Ubabe wa wanawake (kutokubali dhana kuwa mwanamme ni kichwa cha familia sababu ya kipato, elimu umri etc)
Inferiority complex (wanaume kutokubali kuzidiwa kipato, elimu etc na mwanamke)
Ulukuki wa vishawishi na sehemu za ufanyiaji ngono (magesti mpaka uchochoroni)
Mungu kugeuzwa mjomba (hofu ya Mungu inazidi kupungua kila uchao)
Wanawake kujitambua (kutokuwa tayari kuvumilia manyanyaso)
Nk
Nk
Nk

Nawatakieni wote heri ya mwaka mpya. Naziombeeni ndoa zenu zidumu na kudumu na kudumu!
 
mimi nadhani wazazi muwaelimishe watoto kuhusu ndoa tusisubiri mpaka kitchen party, na tutumie vitabu vya dini pia kuwaelewesha watoto, tukae nao mara kwa mara na kuwaelewesha maisha jinsi yalivyo including ndoa ili mtoto aone dhamani ya kuwa mke/mume, na nyyie wazazi muache ubusy.
*pia wazazi muwe mifano mizuri kwa watoto wenu vyo mnagombana mpaka watoto wanajua kama mama na baba wanagombana.
 
Ila kuna siku dunia itakuja jua mahali mwanadamu alipoteleza,na itaku too late,kama kweli unataka ulitumie gari vizuri ni lazima usome "manyuo buku"!Kama ukilitumia vile unavyotaka wewe kisa hutaki "utumwa" kubali matokeo yake ambayo lazima yatakua hasi tu!Ukiyakataa lazima kifaa ulichopewa kuchambua mambo(ubongo)kitakua na mushkeli.
 
Ila akija kugundua baba aliyemlea si wake atakutafuta,sema tu atagunduaje?


Mkuu,

Hakuna mtu anayezaa mtoto ili aje amtafute ukubwani, labda hao wa vichochoroni. Baba wa ukweli anaatamani kuishi na mtoto wake na kumpitisha kwenye hatua zote muhimu za maisha....

Hata kama mtoto akikutafuta ukubwani, nafasi yako kama baba inakuwa ilishapotea siku nyingi..The only chance you have is to become just a good friend!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…