NDOA: Zamani vs Siku hizi

sread nzuri sana ngoja nipike nikimaliza na mie nije kujaribu kuchanganua miaka yangu minne ya ndoa na miaka 36 ya mamaangu na babaangu ya ndoa yao

Halafu nitaomba uje na mawazo yako juu ya hii dhana,

Je onja onja inayofanyika sana kabla ya ndoa siku hizi ina madhara yoyote kwenye ndoa??

Naamini wadau watatoa msaada wao pia!
 
Asante ila nitakuwa peke yangu ndo hivo

Pole sana AD,

Sasa, kwa nini unadhani wazee wetu walifanikiwa kwenye haya mambo ya malavi davi na sie tunafeli??

Please tupe mawazo yako...Not a case study!!
 
Sijui kwanini unanichanganya na Afrodenzi? Au hangover?

Naomba nisiombe hata msamaha kwa sababu kila ninapojaribu kuwa makini ndivyo ninavyozidi kukosea!!

Anyway,

Tupe basi uzoefu wako dada!
 
Nionavyo mie ni tabia ya watu kutothamini umuhimu wa ndoa au maisha ya kuwa na mwenza wa kudumu.kuishi na mtu kweli kazi, lakini kama unathamini uwepo wake utajitahidi kufanya vitu mnavyokubaliana ili msiachane.mfano zamani baba kutokula nyumbani lilikuwa kosa kubwa anatozwa faini.sasa vijana anapita baa anakula mbuzi akija home anabeuwa kweli jamani.mwanamke kwenda kwao kusalimia mpaka ruhusa na mume anacommunicate na wazee wife atakaa siku ngapi.siku hizi mtu anaaga akiwa airport au stendi.na akiwa huko mume au mke hapigi simu hata kusalimia wazee.matokeo yake mama anaaga anaenda kigoma anaishia Sinza.
 

Kweli ndugu,

Kukosa uvumilivu, heshima na ubinafsi ni hatari sana!!
 
Reactions: Mbu
Marriage is no longer linked to comfortable life mkuu! Ndo haswaa maana ya moskwito! Walio kwenye ndoa wanalalamika kila kukicha, hadi walioko single hawatamani kuingia ndoani tena! Ukiskia dunia hadaa ulimwengu shujaa ndo hii sasa!
kweli king...

that is why nimeiweka kama option... maana yake ni kwamba if it is not comfortable people have other options na kuiacha katikati, so rather than an opt in bad stuff, it has become kinda like opt to stay in if it is comfortable

kwa kiswahili labda, ndoa imekua kitu kingine ambacho unabaki ndani tu pale inapokua comfortable, au unaingia tu ili uwe comfortable na mtazamo wako au wa jamii .... we are searching for comfort so if ndoa makes you comfortable unaingia au unabaki, kama inaboa unaiacha zake na ku-move on to other comfortable options
 

Sure,

That's my very basic and simple principle....

Huwezi kung'ang'ania kuishi na mtu ambaye inaonekana kabisa mambo yamekwama. Mmekutana mkiwa wazima na kwa hiyo ni upuuzi kufikiria kuwa huwezi kuishi bila yeye!!
 


....nimeipenda hiyo swahiba! ...hivi kuna mtu atayekubishia kweli hapa?
tofauti ya zamani kwamba ndoa ilikuwa mtu anaoa/olewa kwenda kuanzisha mji/familia yake...sasa hivi
panaangaliwa wapi penye unafuu wa maisha bila kuangaliwa athari za maisha ya pamoja na sacrifices zake.

safi sana mkuu... umeliweka sawa kabisa kamanda
.


...dahhh, kwahiyo Lizzy wadhani ile miongozo ya vitabu vya kiimani iliyowaongoza wazee wetu karne na karne na kwa kiwango kikubwa ilisaidia kusimamia misingi ya familia weye waiona haifai kwa kizazi hiki? Hapa kwa makusudi kabisa nimekuunga mkono zile mila potofu zilizokuwa zinamkandamiza mtoto wa kike na mwanamke, lakini hata maandiko ya kidini yamesisitiza uongozi wa mwanaume na jinsi mwanamke anavyotakiwa aishi kwenye ndoa...


Marriage is no longer linked to comfortable life mkuu! Ndo haswaa maana ya moskwito! Walio kwenye ndoa wanalalamika kila kukicha, hadi walioko single hawatamani kuingia ndoani tena! Ukiskia dunia hadaa ulimwengu shujaa ndo hii sasa!

...shabaash!....

huu nao ni mtazamo mwingine unaokinzana na wa MTM, yaani ni sawa na muono wa bilauri kama ni half full, au half empty...kamanda alitaja ndoa kama an option ya comfortable life, nawe wasema not linked anymore....nyote mko sawa kabisa... NDOA IMEPOTEZA MAANA YAKE!
 

...yanafanyika sana tu haya majumbani, ila ndio kama wachangiaji wengine waliopita walivyotanabahisha, utandawazi nao umeleta athari zake kubwa tu kwenye jamii yetu hii ambayo inatupelekea kutafuta maisha kwa kwa majibu rahisi...mzazi akiwa mtu wa kukemea sana kwa mujibu wa maandiko matukufu ataambiwa ni old fashioned!
...ni wangapi miongoni mwetu tunaozingatia kuhudhuria nyumba za ibada angalau mara moja kila wiki? hofu ya Mwenyezi Mungu imepungua....
nini kifanyike sasa? .....



....sasa mkuu hiyo manual book si ndio hivi vitabu vya kiimani vinavyopigwa vumbi makabatini bana? misahafu, biblia, nk...nk...ila kwa sie kujifanya twajua sana, tunajaribu ku link tafsiri za maazimio ya Beijing katika maisha yetu ya kila siku kuzitafsiri haki za mwanamke...au ni wanaume wamepoteza uwezo wao wa kuwa kichwa cha familia kama mafundisho yalivyotaka?

nani alaumiwe?



...umezungumzia ya maana sana sana, heshima na uthamani wa taasisi hii....no wonder leo hii kuna hata malalamiko ati kuna baadhi ya wake majumbani wameacha kabisa majukumu yao na kuyakabidhisha kwa wasaidizi wa ndani (house girls)....lakini pamoja na hayo, je? ni wanawake tu wanaohusika katika kuporomosha maadili ya taasisi hii???
 
Sure,

That's my very basic and simple principle....

Huwezi kung'ang'ania kuishi na mtu ambaye inaonekana kabisa mambo yamekwama. Mmekutana mkiwa wazima na kwa hiyo ni upuuzi kufikiria kuwa huwezi kuishi bila yeye!!

...sasa mkuu kishindo kinakuja je?

kama ndoa zilikuwa ndio mhimili madhubuti wa familia, leo hii ndoa zinapuuziwa as if ni optional tu?
vipi athari zake kwa watoto na vizazi vijavyo? tunatengeneza taifa na watu wa aina gani, maana ikumbukwe... hapo zamani za kale, ndoa ilihusisha FAMILIA.
 
Aiseee hii mada tamu sana, ila wanaume wa siku hizi kwanza anaona kukuoa ni kama favour flan anakupa, ndo maana hata akiwa anatongoza tu anatanguliza ntakuoa, na akisha kuoa anategemea so much from you (to replace his mother) wakati huo yeye hayupo prepared to do anything hata vile vidogo anavyotakiwa kufanya.

Pili anaona amekupa favour kukubebesha minba, kwani anauwezo wa kuwapa wanawake wengine. now imagine living with a man with this kind of mindset ndo maana watu hawadumu na hizo ndoa,
 
Sababu ya ndoa za leo kutokudumu: This age we have a lot of negotiations. From the morning to the evening, from the sitting room to the bedroom, every where! Ni kwa wale tu ambao wako tayari kwa havoc hii ndo watadumu na ndoa.Ndoa za zamani wamama walikuwa kama ilivyo kwenye kile kipande cha movie la Eddy Murphy," COMING TO AMERICA". Mwambie mama kubweka atabweka,lakini leo thubutu yako,utashangaa una Asha ngedere ndani mwako. Let's go with the era!
 
Reactions: Mbu


na hii ya kuanza na sex, mbona mara nyingi huwa zinafell tena hazifiki kabisa kwenye ndoa, na wanajamii watakwambia usingemvulia kwanza mpaka akuoe, nadhani kudumu kwa ndoa au mahusiano yeyote ni mpaka ukutane na mtu mnaendana, mnasikilizana
 
na hii ya kuanza na sex, mbona mara nyingi huwa zinafell tena hazifiki kabisa kwenye ndoa, na wanajamii watakwambia usingemvulia kwanza mpaka akuoe, nadhani kudumu kwa ndoa au mahusiano yeyote ni mpaka ukutane na mtu mnaendana, mnasikilizana
Kama mnaendana hata mkikutana leo na kuona kesho mtadumu, kama hamuendani hata mkikutana wote ni bikra, mkakaa kwenye uchumba muda mnaodhani unatosha na ndugu wote wakawaunga mkono bado kudumu kwenu kutakua kwa mashaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…