NDOA: Zamani vs Siku hizi

Mkuu mi nipo ila nahisi we ndo umeadimika na una siku special za kujitokeza humu.

Usasa hauna faida na kwa upande mwingine una faida pia,unaweza kufanya nini kama mtu amechoka kukaa na wewe
na ana uhuru wa kukuacha?na kwa upande mwingine amekupunguzia mzigo,ila tunakoelekea ndoa za kufunga kwa
mkataba wa miaka kadhaa itakuwa na nguvu zaidi kuliko zakufunga forever.
Mi nadhani tunakoelekea ndoa hazifungwi,na zikifungwa hazitadumu mana watu hawapendi kubughudiwa.
Mi namfahamu mama mmoja anatembea na rafiki wa mwanae,sasa hapo unategemea nini,hakuna malalamiko na
maisha bado yanasonga.
 
Reactions: Mbu

...Nakubaliana nawe Mkuu DC. Pia uvumilivu ambao ni muhimu sana katika kudumisha ndoa kama uliokuwepo miaka ile sasa hivi hakuna kabisa.

...Shauri yako Mkuu...bora utemee mate chini 🙂🙂 bucha nyingine nyama zao huwa ni vigumu sana kusahaulika....safi, laini na ladha yake huwa ni tamu sana...kamwe huwezi kusahau lol!

hahahahaha...............mabucha mengine utumbo tupu baada ya muda unaanza kuchacha humu duniani raha tele
 
HEKIMA na BUSARA za babu ,DAIMA NITAZINGATIA.....thnks alot babu DC ,nikioa kwa maadili nitakayokuwa nayo kwa wife ,akiniuliza chanzo sitasita kumhabarisha kuhusu ww.:flypig:
 
Hao vijana wenu wa dot com wanayajua hayo?? Au wao wanamind kumwagiwa misitu ya maua, vocha za kumwaga, simu na sms kila sekunde, ..... na vidume kupewa ngono hadi wavimbiwe??

hahahaha...naam, naam, ....haya ndio ma Egoli aliyoyaandika mwj1....
yaani usipomnunulia mke maua valentine day, sijui birthday card, au ukasahau kum wish happy anniversary...yote mazuri uliyomfanyia yanageuka "ajua!".....aisee 'mapenzi' ya kisasa ni usanii wa gharama acha bana!
 
Kulikuwa na lecturer wangu mmoja ye ni mtu wa makamo sana alikuwa na msemo wake pale tulipokuwa tukichemka kazi zake, utamsikia "Vijana mna mbwembwe sana, na mtakwama sana"
Mara nyingi nikiangalia mambo mengi yanayotutokea katika hili varangati lamaisha na mahusiano nadhani nakubali kauli ya yule mzee....
"TUNA MBWEMBWE SANA"

Ila kwa upande wa pili naweza kuongezea kidogo kuwa (labda kwa kufafanua hizo mbwembwe), kuna tofauti za msingi zinazomfanya MWANAUME awe Mwanaume na MWANAMKE awe Mwanamke.....
Lifestyle ya zamani hasa huku kwetu afrika (sijui kuhusu mazingira mengine japo kwa hili) ilizingatia sana huu ukweli na hizi tofauti katika mgawanyo wa majukumu ya kijamii, kifamilia hadi kimapenzi yaani mahusiano ya hizo jinsia.
Sasa mbwembwe za kisiku hizi zimemomonyoa yote haya na kuyaweka kwenye kapu moja, matokeo yake leo kuna "MADUMEJIKE"...
Binti anajiona kaolewa kumbe hilo ni jike kwa maana ya mtazamo na uwezo wa ku-handle family na majukumu ya kiume, vilevile..
Kijana anajiona kuoa kumbe hilo ni Dume kwa maana hiyohiyo.
Kweli tunakwama sana sasa.
 
Mkuu suala la kuishi kwenye ndoa linatakiwa liwepo tu pale panapokuwa na maelewano na amani. Hili ni jambo la muhimu sana.

Enzi zile, jamiii nzima ilihakikisha ndoa inapewa msaada mkubwa ili idumu. Lakini kama ilionekana kuwa haiwezekani, basi wahusika walipewa pia msaada ili waachane salama!!

Hadi sasa principle ni hiyo hiyo ila kinachokosena ni social system ya kusaidia wanandoa pale ambapo wanahisi hawawezi kuishi pamoja. Kwa mfano, sababu zinazotolewa na baadhi ya watu wanaochana ni za ajabu ajabu ukilinganisha na huko nyuma!

Mtu anamwacha mwenzake eti amegundua hakumpenda...Je anafikiria nini kuhusu maisha ya mtu ambaye anamwacha??

Wanataka kula ila wasiliwe...very pathetic!!
 
Reactions: Mbu

Duuuu....kaka hapo umenikumbusha wale maafande wangu wa form 7!!
 
Reactions: Mbu
...Nakubaliana nawe Mkuu DC. Pia uvumilivu ambao ni muhimu sana katika kudumisha ndoa kama uliokuwepo miaka ile sasa hivi hakuna kabisa.

huo uvumilivu mwenzio atakuwa nao?
 
Reactions: BAK
Kuna swala nikuulize hapo kwnye kuoana, nnavojua kwenye usilam kijana wa kiume anapoozeshwa huambiwa " UMEKUBALI KUMUOA FULANI BINTI FULANI and so on" hakuna kitu mnaona, Je hii ibadilike nayo au imekaaje?

...lol...hilo uliloliandika hapo nahisi kama ndio hali iliyopo sasa aisee,...watu wanajichagulia steak tu, dahhh!

...otherwise, mimi nipo sana tu mbona, ila unajua tena...funga mwaka hii kuhesabiwa muhimu hapa, usijekuta kina klorokwini wanapita na vikapu vya michango ya msiba kumbe recession tayari...
 
HEKIMA na BUSARA za babu ,DAIMA NITAZINGATIA.....thnks alot babu DC ,nikioa kwa maadili nitakayokuwa nayo kwa wife ,akiniuliza chanzo sitasita kumhabarisha kuhusu ww.:flypig:

Ahsante sana kaka,

Wewe kaoe tu....Ukiwa tayari kuliwa ili nawe ule naamini utasonga mbele!!

Hawa dada zetu ni wagumu sana kuishi nao but yet very simple kuwamudu.......!!

Kuna dada yangu mmoja alinambia wakati naoa kwamba, jukumu la kuvunja au kulinda ndoa ni la mume!!

Kwa sasa ndo nimeanza kuelewa alikuwa anamaanisha nini!!
 
Kuna swala nikuulize hapo kwnye kuoana, nnavojua kwenye usilam kijana wa kiume anapoozeshwa huambiwa " UMEKUBALI KUMUOA FULANI BINTI FULANI and so on" hakuna kitu mnaona, Je hii ibadilike nayo au imekaaje?

...nahisi kusudio lake hapo ni mume na mke wote kuwa radhi kuoana, maana hata bi harusi huulizwa kabla atoe idhini yake kukubali kuolewa ndipo shekhe muozeshaji anapokuja kwa mume mtarajiwa na swali hilo.
 
i wish muda wangu ukifika niwe on th right boat kwakweli.
 
...Nakubaliana nawe Mkuu DC. Pia uvumilivu ambao ni muhimu sana katika kudumisha ndoa kama uliokuwepo miaka ile sasa hivi hakuna kabisa.

Kaka,

Nasikia vijanza wamechukua chupa zilizojaa uvumilivu wakazi-empty na kujaza ubinafsi!!

Utafika kweli??
 
Reactions: Mbu
Tatizo hizi zinazoitwa Women rights zimeingilia mpaka mambo ya watu ya kidini pia, ndio maana wengine wanazipinga usiseme kuwa hazina tatizo lolote.

Reactions: Mbu
hilo swala la kuishi kwenye ndoa linatakiwa liwepo,ila itawezekana?amegundua kuwa hakupendi na anao uhuru wa kukuacha
utamzuiaje?
 
Hao vijana wenu wa dot com wanayajua hayo?? Au wao wanamind kumwagiwa misitu ya maua, vocha za kumwaga, simu na sms kila sekunde, ..... na vidume kupewa ngono hadi wavimbiwe??
babu DC kwa wtoto wa dotcom ukiwa realistic wanakuona umepitwa na wakati na ni mnoko.
 
Reactions: Mbu
Kuna swala nikuulize hapo kwnye kuoana, nnavojua kwenye usilam kijana wa kiume anapoozeshwa huambiwa " UMEKUBALI KUMUOA FULANI BINTI FULANI and so on" hakuna kitu mnaona, Je hii ibadilike nayo au imekaaje?

Vyovyote vile, mtu anatakiwa kutambua kuwa mmeoana. Wale wanaondekeza kuamini kuwa wameoa au wameolewa hawataweza kuyapita mawimbi haya ya dot com!!

Kwa hiyo pamoja na kuimbishwa hayo wakati wa kufunga ndoa, ni muhimu kuwa mbayu wayu!!
 
Reactions: Mbu
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…