Ndoa zinavyoteseka na hizi simu hasa kwenye kipengele cha NYWILA(PASSWORD)

Uhuru24

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2015
Posts
4,523
Reaction score
5,159
Mimi fundi simu hapa kariakooo ila mojawapo ya hekaheka ninazokutana nazo kwenye simu ni juu ya nywila a.k.a Password.

Hili jambo limeachisha ndoa nyingi sana,unakuta mtu amechukua simu ya mkewe kwa lengo la kumtengenezea haswa kioo,anapofika kwa fundi mwanaume huomba nywila kwa kisingizio cha fundi anataka kujilidhisha na ubora wa kioo(hapo ndio kwenye hekaheka).

Hapo mwanamke ata taja nywila zaidi ya kumi kana kwamba yeye simu tokea iharibike ina miaka3 kumbe siku mbili tu,hivyo tunamwambia huyo hawezi kukupa hiyo nywila wewe mpelekee tu simu yake.

Mwanaume hushikwa na hasira wengine hufikia hatua ya kuwaambia kabisa kabla sijafika nyumbani nikute ushaondoka kama hutaki kutoa nywila,na kweli mwanamke hatoi.

Kuna siku alikuja jamaa na mkewe huku simu ikiwa imevunjwa kioo,yule mwanamke akaninong'oneza kwamba (WAKATI UNAWEKA KIOO HAKIKISHA FORMAT) nitakupa 20,000 maana itakuwa umeniokoa.

Hivyo basi kuna muda unafanya hivyo ili kuokoa ndoa zao kuna siku nyingine mtu anakuja na dau kubwa anakwambia nina wasiwasi na kwenye WhatsApp basi tunafanya kwakweli.

INAKUWAJE UISHI NA MTU HUKU MKIWEKEANA MIPAKA KWENYE SIMU?
Hapa ndio kwenye chanzo cha yote haiwezekani niishi na mke au uishi na mume wako kwenye simu msivhunguzane,maana kufanya hivi kama umehalalisha uhuni(umalaya)kwa kila mmoja wenu.
 
yule mwanamke akaninong'oneza kwamba (WAKATI UNAWEKA KIOO HAKIKISHA FORMAT) nitakupa 20,000 maana itakuwa umeniokoa.
Mke wa hivyo maana yake hakuachana na ma-ex wake, na ni Chawote..
Hakuna ndoa hapo
 
Mke malayamalaya hugawa namba yake hovyohovyo kwa wahuni. Wahuni humtongoza na kuchepuka nao, huficha uovu wake kwa nywila ili mume wake asigundue kuwa anaishi na mzinzi. Always simu za wanandoa hazipaswi kuwekwa nywila. Kuweka nywila huleta mashaka ya kutokuamiana na huleta ufa katika ndoa
 
Mwanamke umeolewa una mume halafu unaweka nywila kwenye simu huo ni umalaya, ni kwamba unaficha mahusiano ya mchepuko, pumbavu, huwa navunja simu zenye nywila, sipendi mwanandoa malaya
Mimi nimeweka password na sina mchepuko wala mpango wa kando. Kikubwa ni usalama wa simu yangu hata akiichukua mwizi labda akai flash.
Kingine ime limit watoto kuchezea simu yangu. Wataishia kujipiga picha na kupiga simu emergency contacts basi.
 
hiyo nywila aijue mume wako, kama mume hajui utaleta shida kwa mume, simu si yako peke yako na ya ndoa yenu
 
Nywila ni kwa wasiohusika kuweza kuona kilichomo ndani ya simu, wezi, watoto na wengine aside ila mume anatakiwa kuijua hiyo nywila, na kama hujui nywila ya simu ya mke wako basi we ni zoba tu huna sauti kwa mke, unatawaliwa kiboya
 
Nashangaa unakuta mwanaume anaiyogopa kujua nywila ya mkewe kisa anasema tusijekugombana,hapa unahalalisha uovu.
 
Mimi fundi simu hapa kariakooo ila mojawapo ya hekaheka ninazokutana nazo kwenye simu ni juu ya nywila a.k.a Password.

Hili jambo limeachisha ndoa nyingi sana,unakuta mtu amechukua simu ya mkewe kwa lengo la kumtengenezea haswa kioo,anapofika kwa fundi mwanaume huomba nywila kwa kisingizio cha fundi anataka kujilidhisha na ubora wa kioo(hapo ndio kwenye hekaheka).

Hapo mwanamke ata taja nywila zaidi ya kumi kana kwamba yeye simu tokea iharibike ina miaka3 kumbe siku mbili tu,hivyo tunamwambia huyo hawezi kukupa hiyo nywila wewe mpelekee tu simu yake.

Mwanaume hushikwa na hasira wengine hufikia hatua ya kuwaambia kabisa kabla sijafika nyumbani nikute ushaondoka kama hutaki kutoa nywila,na kweli mwanamke hatoi.

Kuna siku alikuja jamaa na mkewe huku simu ikiwa imevunjwa kioo,yule mwanamke akaninong'oneza kwamba (WAKATI UNAWEKA KIOO HAKIKISHA FORMAT) nitakupa 20,000 maana itakuwa umeniokoa.

Hivyo basi kuna muda unafanya hivyo ili kuokoa ndoa zao kuna siku nyingine mtu anakuja na dau kubwa anakwambia nina wasiwasi na kwenye WhatsApp basi tunafanya kwakweli.

INAKUWAJE UISHI NA MTU HUKU MKIWEKEANA MIPAKA KWENYE SIMU?
Hapa ndio kwenye chanzo cha yote haiwezekani niishi na mke au uishi na mume wako kwenye simu msivhunguzane,maana kufanya hivi kama umehalalisha uhuni(umalaya)kwa kila mmoja wenu.

Hakika ni kazi ngumu unayo, lete habari zaidi...
hapo orange sijakuelewa.
kijani 👑:eeveeHappy::eeveeHappy::eeveeHappy:
swali la wakataa ndoa wa humu:DoctorPls::DragonJAM:😂

Ila nafikiria tu ni kwamba hao wanawake inakuwaje wanaume wanawaletea simu zao? kukosa pesa wenyewe au hawawezi kuja mjini na kujua mlipo?

Lazima umepata picha hao waume wanasemaje?

Na wanawake wanaleta simu za waume zao au? 😀 :BULBAROLL:
 
Mwanaume yupo sahihi kutengeneza simu ya mkewe,mwanaume anafanya kazi maeneo ya msimbazi,mnazi mmoja au azikiwe,sas hawezi akaongozana na mkewe amuache karikoo atengeneze simu na yeye aende kazini,ila kwakuwa mwanaume anafanya kazi mazingira haya hamna sababu na mke kuja kutengeneza simu.(mtazamo wa wengi)
 
Back
Top Bottom