Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Tuendelee na sehemu ya pili na ya mwisho.
Kupanda kwa Prince Fumimaro Konoe kuelekea kilele cha mamlaka hakukuwa matokeo ya mapinduzi, bali mwendelezo wa urithi wa kifalme uliovaa suti ya siasa. Sasa mwezi Juni 1937, kwa mapendekezo na maneno mazuri kutoka kwa mlezi wake Saionji Kinmochi, Konoe aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Japani. tusisahau kuwa bwana mdogo alikuwa chini ya uangalizi wa Saionji Kinmochi walivyokwenda kwenye ujumbe wa amani kule Paris, ni kama kazi aliyopewa enzi yupo naye Paris ilikuwa ni kazi ya mafanikio.
Wengi walimwona kama mtu wa kuleta uwiano kati ya serikali ya kiraia na jeshi lililokuwa linaongezeka nguvu kwa kasi ya kutisha katika maisha ya watu, kwa ufupi ndani ya Japan viongozi wengi wa kijeshi walishika nafasu za umma. Mfano, Hideki Tojo ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu alikuwa pia ni Jenerali wa Jeshi, Sadao Araki ambaye aliwahi kuwa Ndalichako wa Japani, mwamba alikuwa ni Jenerali wa Jeshi. Kantaro Suzuki ambaye huyu alikuwa Waziri Mkuu mwaka 1945, Janja alikuwa ni Admiral.
Lakini historia haikumpa muda wa kupumzika hata kidogo. Tukio la Marco Polo Bridge Incident lilitokea mwezi mmoja baadaye, kwa lugha ya watoto wa Nyerere, ilikuwa siku ya saba saba, na Japani ikaingia katika vita kamili dhidi ya China. Badala ya kuzuia upanuzi wa vita, serikali ya Konoe iliruhusu jeshi liingie China na kuzichapa, ikiamini ushindi wa haraka ungefuta matatizo ya ndani. Hii ilikuwa hesabu mbaya ya kihistoria ya kivita duniani.
Chini ya uongozi wake, Japani ilipata ushindi wa kijeshi lakini ikapoteza uhalali wa kimaadili. Mauaji ya Nanjing, mateso ya raia, na uhalifu wa kivita vilitokea katika kipindi chake. Konoe hakutoa amri moja kwa moja ya mauaji, lakini alihusika kwa kukaa kimya, jambo ambalo historia haijasahau. Marco Polo Bridge Incident ikampatia kichwa sana Mjapani na kuongeza moto huku akikumbushia tukio la Mukden Incident la mwaka 1931.
Mwaka 1938, Konoe alipitisha sheria yake ya kwanza kabsa, sheria ya State General Mobilization Law, sheria iliyogeuza Japani kuwa dola yenye udhibiti kamili. Serikali ilipata mamlaka ya kudhibiti viwanda, vyombo vya habari, ajira, mishahara, na hata mawazo ya raia wa Japani. Kwa jina la vita, uhuru wa kiraia ulifutwa kabsa, hapa ndipo Konoe alipobatizwa jina jipya la mbunifu mkuu wa Japani ya kiimla.
Baada ya kushindwa kupata ushindi wa haraka nchini China, alijiuzulu mwaka 1939, lakini alirudi tena madarakani mwaka 1940. Kipindi hiki kilikuwa hatari zaidi. Alianzisha Imperial Rule Assistance Association, chama kimoja kilichozika demokrasia ya Japani, lengo la mwamba likiwa ni kusimamia new order ambayo aliipatia jina la Shintaisei, dogo alikuwa amevurugwa balaa kwani pia alisaini Mkataba wa Tripartite na Ujerumani ya Nazi na Italia ya Benitto Mussolini, akiiunganisha Japani na nguvu za uharibifu wa dunia.
Lakini ndani ya Konoe, hofu ilianza kukua taratibu. Aliona wazi kwamba jeshi, hasa Jeshi la nchi kavu, lilikuwa limeiteka serikali na hakukuw na namna ya kulishauri, kwani walikuwa wamejaa watu wa jeshi kama majenerali, na admirals wa kutosha kwenye wizara. Mazungumzo yake na Marekani yalivunjwa na ratiba kali ya kijeshi.
Alipoona hawezi tena kudhibiti maji ya Tsunami, alijiuzulu Oktoba 1941, miezi michache kabla ya tukio la Pearl Harbor ambalo Mmarekani alitangaza vita ndani ya masaa 24 pekee. Ni kama mwamba aliona mbele kuwa hii ngoma itamuharibia jina lake.
Kuanzia hapo, Prince Konoe alibadilika kutoka kuwa mtendaji wa vita na kuwa mshauri. Alibaki karibu na Mfalme Hirohito na alichangia kuangushwa kwa serikali ya Tojo mwaka 1944. Kufikia 1945, akiwa na taarifa kamili za hali ya kijeshi, alitambua kwamba Japani ilikuwa imefika mwisho.
Alipata taarifa hizo kupitia mashushu wake, ambao walisema kuwa timu ya kijeshi inayoongozwa na CGS Yoshijiro Umezu pamoja na Shunroku Hata, kuwa wameshaingia baridi ile mbaya. Majenerali wawili Tomoyuki Yamashita pamoja na Seishiro Itagaki walikuwa tayari kabsa kukubali kushindwa ili Japani iwe salama.
Mwamba akaona isiwe mbaya akakaa na kuandika barua yake inayoitwa “Konoe Memorial” ya 14 Februari 1945, akimwambia Mfalme kwa lugha ya heshima lakini yenye uzito mkubwa: “kuendelea na vita kungesababisha maangamizi ya taifa na hata mapinduzi ya kikomunisti”.
Hii ni kama Konoe alimuota Matarajin na kuambiwa kuwa Hiroshima pamoja na Nagasaki zinakwenda kupigwa mabomu. Lakini kama ilivyokuwa kwa Shigenori Tōgō na Admiral Mitsumasa Yonai, ushauri wake ulifungwa ndani ya woga wa kumkosea heshima Mfalme Hirohito.
Baada ya kujisalimisha kwa Japani, Konoe alijiunga kwa muda mfupi sana baada ya serikali kuwa chini ya Waziri Mkuu Prince Naruhiko Higashikuni. Lakini kivuli cha vita kilimfuata. Alishukiwa kwa kesi uhalifu wa kivita.
Mwamba aligoma na kukataa kushirikia katika Operation Blacklist – mpango wa Marekani ambao moja ya malengo yake ilikuwa ni kumsafisha Mfalme Hirohito na taasisi ya Kifalme dhidi ya lawama zote – mwamba akaona huu ni ujinga, inawezekanaje mjapani tena aliyepigwa na Mmarekani kuunganisha nguvu na Mmarekani, kwake ilikuwa ni usaliti mwingine.
16 Desemba 1945, siku moja kabla ya kukamatwa kwake, Konoe alikunywa potassium cyanide na kufa. Mwamba aliona kifo ni bora kuliko fedheha ya kesi. Mazungumzo yake ya mwisho na mwanawe Michitaka yalijaa majuto, huku mshua akiongea zaidi kuliko dogo, ni kama vile mshua alikuwa anamuaga dogo.
Je unafahamu kuwa **Mirihiro Hosokawa ni mjukuu wa Konoe na ndiye alikuja kuwa Waziri wa Japani kuanzia mwaka 1993 mpaka 1994.
Prince Fumimaro Konoe alikuwa mjenzi wa mfumo wa vita na pia mwathirika wa mfumo alioutengeneza. Alikuwa na medali za heshima, nafasi za juu, na ukoo wa kifalme, mpaka anaondoka duniani alikuwa na jumla za medali saba, ikiwemo Order of the Rising Sun, 1st Class pamoja na Order of the Sacred Treasure.
Kuna watu huota ndoto na wakikuambia kuwa jambo baya litatokea basi kuwa mpole na sikiliza maneno yao, usiwe mgumu kama Mfalme Hirohito.
MWISHO