Ndoto inayojirudia sana

Ndoto inayojirudia sana

Ndoto yako inaweza kuwa na tafsiri hii: inaonekana Kuna namna ulitakiwa kuwa umefika level flan lkn bado unaweza ukajua Hilo kwa kuangalia wenzako mliokua na uwezo sawa wako wapi.
Au pia inaweza kuwa ni ishara kwamba ujiandae kwa changamoto mpya ili uweze kuvuka na kuinuliwa zaidi.
Kwa namna fulani ilibidi niwe sehemu fulani kitaaluma. Doctorate or more japo sikufika na sina tena mpango wa kufika huko. Infact I derailed and now fighting back to tracks- the standards was supposed to be
 
Dah mkuu kumbe inatukuta wengi? Ila mimi huwa inatokea mara nyingi nachelewa mtihani yaani naweza hisi naenda kabisa ila nkifika mtihani huwa ushaisha au unakuta msimamizi ananicheleweshea tu mtihani mwisho wa siku siandiki chochote kwenye mtihani huo.

Ndoto mara nyingi huwa ni mtihani wa chuo ila location huwa ni sehemu ambayo nimesoma advenced level.
Aisee...😄 Mi location zote hunijia. Primary, secondary, hata university. Utakuta primary mara niko na jamaa tuliomaliza chuo
 
Hii inamaanisha kuwa hapo ulipo upo idol. Yaani ni kama haujatimiza ndoto yako ulivyotaka uwe. Upo katika situation ambayo ni low kuliko ulivyotakiwa kuwa. So pambana tafuta njia ya kutoka hapo kwenye hilo shimo ulipostuck.
🙏 Kweli Victoire. Iam not living my supposed life
 
Pole sana mkuu me ndoto kama hizi huwa zinanitokea na hii za mitihani huwa zinanitokea kweli najikuta nipo katika kipindi cha kufanya mitihani na sijasoma nk,ila nilitamani kuuliza kwa wa2 lakini nikashindwa ila sikujua kwa nini nilishindwa kuuliza,kwenye pita pita zangu mitandaoni nikakuta kuna m2 kauliza swali hilo hilo kwa mtu mwenye uelewa wa elimu hiyo husika na moja wapo ya jibu alilotoa ni kuwa ndoto hiyo si nzuri sana kwa m2 kuiota kwani inaelekea mtu kupata shida, changamoto,matatizo,wakati mgumu na vitu vinavyofanana na hivyo nilivyo vielezea,ila ili upate jibu kamili ingia hata youtube search juu ya hiyo ndoto na jibu utapata.
Ila yote kwa yote Akili ya kuambiwa changanya na yako
 
Kumbe tuko wengi. Basi kuna kaukweli katika hizo tafsiri za watu mbalimbali. La msingi ni kupambana hadi mitihani ifanyike na kufaulu pia nadhani ndio ndoto hizi zitakoma 😀
 
Kama title inavyosema, nimekuwa nikiota niko shule na ni kipindi cha kumaliza. Kipindi cha mitihani.

Sasa huwa najikuta sijasoma kabisa na mtihani ndio huo! Basi huwa naweweseka sana na kuwa na hofu. Wakati wengine wanajiandaa mi huwa sijui niko bize na nini. Mwisho wa siku huwa napata ahueni kuwa ni ndoto.

Kubwa kuliko ni usiku uliopita. Mitihani mingine japo sikuwa nimesoma niliifanya kiaina, kama kingereza (sikumbuki ilikuwa level gani-sec or primary). Sasa mtihani wa mwisho ilikuwa namba.

Yani kila nikiwaza sioni natoboa vipi. Sikumbuki fomula wala nini. Kila ninayemfuata japo animumbushie longolongo nyingi. Wakawa wananiambia nikae karibu na mtaalam ili nidese. Bado simutaka iwe hivyo.

Ikawa imebaki masaa machache pepa kuanza. Hapo ni alhamis. Kumbe bana mi ndio nilikuwa sijui kuwa kuwa pepa itafanyika next week jumanne.

Yani ni kama niliona nyota ya jaha kwa furaha na ahueni. Ningepata muda wa kutosha kureview na angalau kujibu baadhi ya maswali.

Nilifurahi zaidi nilipogundua kuwa ni ndoto.

Siku chache zilizopita tena nikaota tuko kwenye mitihani. Safari hii ni chuo. Pepa za kumaliza mwaka wa mwisho. Mambo yakawa mengi naingia humu natokea mule.

Basi ikawa mitihani iliyobakia sikufanya. Hiyo ikimaanisha sitagraduate.

Basi ndoto za namna hii zimeshajirudia zaidi ya mara kumi. Hatari sana
Fanyiwa maombi ya deliverance hiyosio ndoto nzuri,niliwahi somam mahalim kwamba ndoto za namna hiyo inaashiria kwamba uko na roho za kucheleweshwa
 
Aisee hii ndoto mm haipiti siku 1 lazima niote tena inajia sana sijui kwanini hapa sio bure kuna namna haiwezekani kila siku mandoto ya shule mara nipo shule ya msingi mara secondary mara chuo
Ila kuna siku ndio iliniacha hoi niliota kuna vita vya dunia sasa likapigwa bomu la nyukilia likaenda juu likawa linakuja maeneo ya chuo chetu na wanafunzi wapo wengi basi wakawa wanakimbia huku na kule kila mtu anaogopa basi mm nikapaaa mpaka juu kuliwahi nikalikamata na kulizima nikiwa huko angani na ndoto ikakakata hapo kuamka hoi
Kabla hujalala..hakikisha umekula ukashiba vzr kisha lala?
 
Dah mkuu kumbe inatukuta wengi? Ila mimi huwa inatokea mara nyingi nachelewa mtihani yaani naweza hisi naenda kabisa ila nkifika mtihani huwa ushaisha au unakuta msimamizi ananicheleweshea tu mtihani mwisho wa siku siandiki chochote kwenye mtihani huo.

Ndoto mara nyingi huwa ni mtihani wa chuo ila location huwa ni sehemu ambayo nimesoma advenced level.
Hii ya kwako unakwamishwa kifursa. Kuna chances zinatokea kwenye maisha yako lakini zinakwamishwa zisikufikie, wakati huo huo unakuwa unapitia kwenye vikwazo lakini ukiwa unataka kutoboa kunatokea vikwazo na unaikosa hiyo fursa.

Ukiota uko shule hasa Msingi na Sekondari huku kiuhalisia ulishamaliza kitambo, ukiwaota marafiki zako wa utotoni jua kwamba maisha yako yamerudishwa nyuma, kuna mkwamo kwenye maendeleo yako.

Unachotakiwa kufanya ni kuanza kujichunguza, ni mipango gani ukiwa unataka kuifanya unapata ugumu na pengine kupelekea kushindwa kabisa kuikamilisha au unaghahirisha pasipo sababu za msingi.

Tafuta msaada wa kiroho ili Mungu akusaidie.
 
Kwa namna fulani ilibidi niwe sehemu fulani kitaaluma. Doctorate or more japo sikufika na sina tena mpango wa kufika huko. Infact I derailed and now fighting back to tracks- the standards was supposed to be
Kama una muda wa kutosha timiza maono yako mkuu huwezi kujua Mungu amekupangia nini kwenye hiyo nafasi. Usikate tamaa.
 
Ha ha ha

Tupo wengi

Mtu unasali, unakemeaa

Lakini bado unalishwa tu na unamkaa mdomo mchunguu.

Pole yetu mweeee.
Hapa inabidi utafute chanzo cha tatizo na siyo kushughulishia tatizo. Hii yako ni madhabahu ndio zinakusumbua na siyo roho unazozikemea. Go deep kujua chanzo cha kulishwa hivyo vyakula.

Ukiota unalishwa vyakula maana yake unaingizwa kwenye maagano ya kichawi kwa kutumia malango ya kwenu. Chunguza ukoo wenu ni wa namna gani, huko nyuma kulikuwa na nini, walifanya nini /waliagana nini na miungu, ulitakiwa kuwa nani kwenye familia (mila),na umevunja makubaliano yao.

Chunguza tu mkuu utaujua ukweli na kupata muongozo jinsi ya kuomba.
 
Dah....ni Kama hawa watu wanaonilisha nyama wamenisikia kwamba nimechoka nyama.....usiku wa leo wamenilisha maharage....Ila mmoja nimemtambua

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Kama umemtambua ndio mwanzo kuanza kujua chanzo chake, utawajua wote na utajua kwanini wanakuingiza kwenye maagano yao.
 
Back
Top Bottom