Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
Kama title inavyosema, nimekuwa nikiota niko shule na ni kipindi cha kumaliza. Kipindi cha mitihani.
Sasa huwa najikuta sijasoma kabisa na mtihani ndio huo! Basi huwa naweweseka sana na kuwa na hofu. Wakati wengine wanajiandaa mi huwa sijui niko bize na nini. Mwisho wa siku huwa napata ahueni kuwa ni ndoto.
Kubwa kuliko ni usiku uliopita. Mitihani mingine japo sikuwa nimesoma niliifanya kiaina, kama kingereza (sikumbuki ilikuwa level gani-sec or primary). Sasa mtihani wa mwisho ilikuwa namba.
Yani kila nikiwaza sioni natoboa vipi. Sikumbuki fomula wala nini. Kila ninayemfuata japo animumbushie longolongo nyingi. Wakawa wananiambia nikae karibu na mtaalam ili nidese. Bado simutaka iwe hivyo.
Ikawa imebaki masaa machache pepa kuanza. Hapo ni alhamis. Kumbe bana mi ndio nilikuwa sijui kuwa kuwa pepa itafanyika next week jumanne.
Yani ni kama niliona nyota ya jaha kwa furaha na ahueni. Ningepata muda wa kutosha kureview na angalau kujibu baadhi ya maswali.
Nilifurahi zaidi nilipogundua kuwa ni ndoto.
Siku chache zilizopita tena nikaota tuko kwenye mitihani. Safari hii ni chuo. Pepa za kumaliza mwaka wa mwisho. Mambo yakawa mengi naingia humu natokea mule.
Basi ikawa mitihani iliyobakia sikufanya. Hiyo ikimaanisha sitagraduate.
Basi ndoto za namna hii zimeshajirudia zaidi ya mara kumi. Hatari sana