Ndoto inayojirudia ya kuokota pesa za sarafu ina maana gani?

Ndoto inayojirudia ya kuokota pesa za sarafu ina maana gani?

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Habari. Kuna hii ndoto ambayo karibu Kila wiki lazima niiote. Ninakuwa naokota pesa za sarafu mpaka za mataifa mengine na zinakuwa nyingi kiasi kwamba naweza kutembea hata kilomita Moja na Kila mahali naokota hizi pesa. Nimeanza kuiota kitambo sana.

Usiku wa kuamkia Leo pia nimeiota Sasa nilikuwa na mdogo wangu wa kike akaniona naokota na yeye akaanza kuokota ila akawa ananilaumu Kwa nini Huwa naokota mwenyewe Kwa Siri na yeye simwambii.

Wenye ujuzi wa fasiri za ndoto msaada tafadhali maana nimeipuuzia sana lakini inabidi sasa nipate jawabu.
 
Habari. Kuna hii ndoto ambayo karibu Kila wiki lazima niiote. Ninakuwa naokota pesa za sarafu mpaka za mataifa mengine na zinakuwa nyingi kiasi kwamba naweza kutembea hata kilomita Moja na Kila mahali naokota hizi pesa. Nimeanza kuiota kitambo sana. Usiku wa kuamkia Leo pia nimeiota Sasa nilikuwa na mdogo wangu wa like akaniona naokota na yeye akaanza kuokota ila akawa ananilaumu Kwa nini Huwa naokota mwenyewe Kwa Siri na yeye simwambii. Wenye ujuzi wa fasiri za ndoto msaada tafadhali maana nimeipuuzia sana lakini inabidi sasa nipate jawabu.
Sijui imanani hako lakini ndoto yako iko halisi kiroho.

Mara nyingi ni roho ya umasikini inakuwa inakufata, ndio maana unaokota sarafu pekee na sio noti. Tafuta msaada wa kiroho kulingana na imani yako.
 
Sijui imanani hako lakini ndoto yako iko halisi kiroho.

Tuchukulie katika hali ya kawaida. Je ukiwa unatembea ukaona hera njiani, kwa mfano 10,000 Tshs utaichukua au utaicha?

Jibu ni INATEGEMEA. Kabla hujaichukua lazima uhakikishe Roho Mtakatifu amekuruhusu uichukue. Unaweza kuchukua pesa kumbe ni sadaka ilitolewa kwenye kafara au ni sadaka imewekwa kwa ajili ya mapepo. Hivyo ukiichukua kuna kitu kitakupata.

Hivyo hata kwenye suala la ndoto za pesa ni hivyo hivyo. Ndoto ya pesa inategemea. Kwa mfano: watu wengine wanaenda kwa waganga wakienyeji halafu wanatoa sadaka. Halafu mganga anaweza kuchimba na kuzika zile pesa kama ishara ya kuzitoa kwa miungu.

Katika ulimwengu wa roho, zile pesa zinakuwepo kule. Sasa wewe kwenye ndoto unaota unachimba hera then unazichukua halafu zinakuwa haziishi.

Mara nyingi ni roho ya umasikini inakuwa inakufata, ndio maana unaokota sarafu pekee na sio noti. Tafuta msaada wa kiroho kulingana na imani yako.
Asante. Mimi ni mkristo. Nitawasiliana na washauri wa kiroho nisikie maoni yao
 
Habari. Kuna hii ndoto ambayo karibu Kila wiki lazima niiote. Ninakuwa naokota pesa za sarafu mpaka za mataifa mengine na zinakuwa nyingi kiasi kwamba naweza kutembea hata kilomita Moja na Kila mahali naokota hizi pesa. Nimeanza kuiota kitambo sana. Usiku wa kuamkia Leo pia nimeiota Sasa nilikuwa na mdogo wangu wa kike akaniona naokota na yeye akaanza kuokota ila akawa ananilaumu Kwa nini Huwa naokota mwenyewe Kwa Siri na yeye simwambii. Wenye ujuzi wa fasiri za ndoto msaada tafadhali maana nimeipuuzia sana lakini inabidi sasa nipate jawabu.
Illusions

Fanya kazi hakuna pesa za bure bure[emoji23]
 
Back
Top Bottom