Ndoto inayojirudia ya kuokota pesa za sarafu ina maana gani?

Hii ndoto ya umasiki mkuu! Unatakiwa uwokote noti nyekundu zile
Hizo za noti nyekundu za TZ au noti zingine Euro au USD hunijia mara chache na mara nyingi hizi za Euro na USD Huwa siziokoti inakuwa labda Kuna kazi nimepiga ndio nalipwa Kwa hizo currencies
 
Sijui imanani hako lakini ndoto yako iko halisi kiroho.

Mara nyingi ni roho ya umasikini inakuwa inakufata, ndio maana unaokota sarafu pekee na sio noti. Tafuta msaada wa kiroho kulingana na imani yako.
Niliota nimepata mibunda mingi sana ya hela yaani hazibebeki.
Nikapanga mipango kibao.
Duh, kuashtuka ndotoni nikamakia kitandani kwangu palepale kazakamba.
Nikalaani kwanini ndoto ile imeisha mapema.
 
Pole sana mkuu😂😂 ulitamani iendelee
 
Kiufupi mkuu unafanya kazi inayokupatia kipato kidogo na ni kwa muda mrefu sasa, na means ya kukuza kipato hujapata, na ndipo watu wako wa karibu wanakulaumu kwanini unafanya kuokota hizo hela ndogo hvo na humwambii kiasi anakutegemea akijua mambo supa kumbe hela mbuzi,

Buni vipato vipya japo ulicho nacho sasa usikiache, buni kipato baada ya kazi zako za kawaida, badili mfumo wa maisha, kama ulikua ukitoka job unapita kwa masela kutia stor badilisha ratiba, wafanye washkaji wawe mtaji wako kwa kubuni bidhaa ambayo watakua wanakuungisha mara kwa mara, usiruhusu mikopo, vaa mavazi nadhifu na safi, fanya usafi unapoishi na unapolala, fanya usafi wa roho na akili kwa kusoma Vitabu Vitakatifu na makala za ujasiriamali, badilisha mazungumzo/kauli zko kati yako na wote wanaokuzunguka ziwe nadhifu na zisizo na hasira, stor zako zisiwe za past events hard time bali ziwe za invensions..usisimange watu walioshindwa kimaendeleo wala usiwatolee mfano ktk stor zako isipokua wale wenye mafanikio ya kawaida unayoyaona na yaliyokuzunguka...pitia youtube handworks mbalimbali za kawaida hata mbili tatu kila siku, sikiliza gospal music mbili tatu kabla ya kulala kila siku

Hutaota tena hizo ndoto..baada ya kufanya haya.
 
Habari. Kuna hii ndoto ambayo karibu Kila wiki lazima niiote. Ninakuwa naokota pesa za sarafu mpaka za mataifa mengine na zinakuwa nyingi kiasi kwamba naweza kutembea hata kilomita Moja na Kila mahali naokota hizi pesa. Nimeanza kuiota kitambo sana.

Usiku wa kuamkia Leo pia nimeiota Sasa nilikuwa na mdogo wangu wa kike akaniona naokota na yeye akaanza kuokota ila akawa ananilaumu Kwa nini Huwa naokota mwenyewe Kwa Siri na yeye simwambii.

Wenye ujuzi wa fasiri za ndoto msaada tafadhali maana nimeipuuzia sana lakini inabidi sasa nipate jawabu.
Tawaza na maji ya moto uondoe kutu....maana sarafu huwa inashika kutu....na sarafu ni umaskini ondoa kutu kwenye maisha yako kwa kutawaza na maji ya moto.
 
Kiufupi mkuu unafanya kazi inayokupatia kipato kidogo na ni kwa muda mrefu sasa, na means ya kukuza kipato hujapata, na ndipo watu wako wa karibu wanakulaumu kwanini unafanya kuokota hizo hela ndogo hvo na humwambii kiasi anakutegemea akijua mambo supa kumbe hela mbuzi,

Buni vipato vipya japo ulicho nacho sasa usikiache, buni kipato baada ya kazi zako za kawaida, badili mfumo wa maisha, kama ulikua ukitoka job unapita kwa masela kutia stor badilisha ratiba, wafanye washkaji wawe mtaji wako kwa kubuni bidhaa ambayo watakua wanakuungisha mara kwa mara, usiruhusu mikopo, vaa mavazi nadhifu na safi, fanya usafi unapoishi na unapolala, fanya usafi wa roho na akili kwa kusoma Vitabu Vitakatifu na makala za ujasiriamali, badilisha mazungumzo/kauli zko kati yako na wote wanaokuzunguka ziwe nadhifu na zisizo na hasira, stor zako zisiwe za past events hard time bali ziwe za invensions..usisimange watu walioshindwa kimaendeleo wala usiwatolee mfano ktk stor zako isipokua wale wenye mafanikio ya kawaida unayoyaona na yaliyokuzunguka...pitia youtube handworks mbalimbali za kawaida hata mbili tatu kila siku, sikiliza gospal music mbili tatu kabla ya kulala kila siku

Hutaota tena hizo ndoto..baada ya kufanya haya.
Shukrani kwa ushauri mkuu
 
Habari. Kuna hii ndoto ambayo karibu Kila wiki lazima niiote. Ninakuwa naokota pesa za sarafu mpaka za mataifa mengine na zinakuwa nyingi kiasi kwamba naweza kutembea hata kilomita Moja na Kila mahali naokota hizi pesa. Nimeanza kuiota kitambo sana.

Usiku wa kuamkia Leo pia nimeiota Sasa nilikuwa na mdogo wangu wa kike akaniona naokota na yeye akaanza kuokota ila akawa ananilaumu Kwa nini Huwa naokota mwenyewe Kwa Siri na yeye simwambii.

Wenye ujuzi wa fasiri za ndoto msaada tafadhali maana nimeipuuzia sana lakini inabidi sasa nipate jawabu.
Hali yako ya kiuchumi ikoje kwa sasa? Inaendana na matarajio yako?

Kazi unayoifanya inaendana na taaluma yako?
 
Hii ndoto ya umasiki mkuu! Unatakiwa uwokote noti nyekundu zile
Jamani eeh.. nmeona weng wanasema kuhusu kuokota noti ndio ishara nzuri.. mwezi kama wa tatu kama sio wa nne niliota kuokota hayo manoti tena mengne yalikua yananitoka tu mfukoni ila ukata nilio nao kwny real life acha tu.. sasa which is which hapo
 
Mambo ya ndoto ni ubashiri kama tabiri nyingine tu !! Huenda ndoto kweli zina maana lakini kujua yupi anatafsiri ukweli ni ngumu !!😂😂 Utakaa hapa watakupeleka huku na huku mradi tu zinatafsriwa kwa mazoea ! Ooh ukiona rangi nyekundu ni hatari , ukiona mwewe mara ukiota uko darasani blah blah kibao mradi kila mtu atafsiri !! Ukiota omba utafsriwe lakini usiufanye mwongozo wa maisha yako ! Utajijenga hofu au utajipa matumaini yasiyo na msingi 😂😂😂 sasa kama kuokota sarafu ni Umaskini wakati ukweli tunaamin hakuna Billion bila senti moja au Shilingi moja kwanini tusitafsiri kwamba hapo anaiendea step ya mafanikio kutoka chini kwenda juu , "Mbuyu huanza kama mchicha" ila watafsiri ndoto kwa mazoea watakupanga hapa ! Utaondoka na sonona ! Ndoto ni ubongo tu unakua unareharsal shughuli zake !! Ndo maana ndoto hutaota kitu ambacho hakiko kwenye mizunguko yako Daily au mawazo yako !!! We ni mchaga !! Mbona hujawahi kuota unaongea Kijaluo !! Au mbona usiote uko Kwenye Medieval era ! utaota uko shule kwa sababu robo ya maisha yako mara nyingi tunaitumia tukiwa shule , na ndo sehemu kubwa tunapotengeneza moments marafiki wa ukubwani n.k ni mifano tu !!.
 
Back
Top Bottom