Ndoto inayojirudia ya kuokota pesa za sarafu ina maana gani?

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Habari. Kuna hii ndoto ambayo karibu Kila wiki lazima niiote. Ninakuwa naokota pesa za sarafu mpaka za mataifa mengine na zinakuwa nyingi kiasi kwamba naweza kutembea hata kilomita Moja na Kila mahali naokota hizi pesa. Nimeanza kuiota kitambo sana.

Usiku wa kuamkia Leo pia nimeiota Sasa nilikuwa na mdogo wangu wa kike akaniona naokota na yeye akaanza kuokota ila akawa ananilaumu Kwa nini Huwa naokota mwenyewe Kwa Siri na yeye simwambii.

Wenye ujuzi wa fasiri za ndoto msaada tafadhali maana nimeipuuzia sana lakini inabidi sasa nipate jawabu.
 
Sijui imanani hako lakini ndoto yako iko halisi kiroho.

Mara nyingi ni roho ya umasikini inakuwa inakufata, ndio maana unaokota sarafu pekee na sio noti. Tafuta msaada wa kiroho kulingana na imani yako.
 
Asante. Mimi ni mkristo. Nitawasiliana na washauri wa kiroho nisikie maoni yao
 
Illusions

Fanya kazi hakuna pesa za bure bure[emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…