Ndoto inayojirudia ya kuokota pesa za sarafu ina maana gani?

Mhh!! Kinachonishangaza ni huo wingi wa sarafu. Naweza kutembea kutoka Faya mpaka Muhimbili Kila mahali naziokota!!
Bro,unapata mwanamke wa level ya chini,unatongoza tena unapata wa namna hiyohiyo tena,Kuna kupata wa level yako hapo? Si utakuwa ushazeeka....kuziokotz hizohizo tu badala ya noti means hakuna maendeleo
 
Bro,unapata mwanamke wa level ya chini,unatongoza tena unapata wa namna hiyohiyo tena,Kuna kupata wa level yako hapo? Si utakuwa ushazeeka....kuziokotz hizohizo tu badala ya noti means hakuna maendeleo
Huo mfano sasa daah😅
 
Inatakiwa ujue sarafu ni za aina gani, na muda gani. Sarafu za copper au gold ambazo ni za zamani hiyo ni ishara nzuri kwamba kuna jema linakujia ila maadui wapo kuliharibu hivyo mtangulize Mungu kwa kila jambo.
Kama ni sarafu za kisasa mkuu safisha nyota na linda isichafuliwe au usiichafue
 
Shukrani. Huwa naokota zile za zamani pia ambazo hazipo kwenye mzunguko lakini zinakuwa za nchi zingine. Whether ni gold au silver Sina hakika.
 
Mosi : tambua kuwa una majini..... hili utakuja kuliona huko mbeleni.....

Kila BINADAMU ana mapepo...hutegemea tu nguvu ya hayo mapepo na aina ya mapepo....

Umeona jinsi mdogo wako anavyokulaumu kuwa humwambii kama huwa unaokota?!!!

Yeye hana mapepo ya aina uliyonayo....hayo mapepo yamekuletea tu taswira ya kukuonyesha kuwa wewe ndiye mwenye nayo.....

Hakuna NDOTO ya kawaida anayoota mtu kwa kujirudia kila uchao.....

Mkuu umeshawahi kufanya kazi migodini kama nyoka?!!!

Binafsi nimeshawahi....na pamoja na KUWAHI kuota mambo ya Madini ili hazijawahi kunirudia Kama hizo zako ilihali nilikuwa nazama miduarani kila uchao......[emoji1787]

Nasita kuelezea mengi kwa kuwa zinaonekana imani za kishirikina....ila mambo ya aina hiyo yapo....japo si lazima kuhusisha nayo kwa kila kitu......

Peace & Love[emoji120]
 
nyota yako inatumika ndugu. jamaa anapiga pesa huko. kimbilia kwa Yesu ndio suluhisho, hata ukienda kwa mganga anaenda kuishukua na kumuuzia atakayempa pesa nzuri.
 

Hii ndoto ya umasiki mkuu! Unatakiwa uwokote noti nyekundu zile
 
Sijawahi kabisa kufanya kazi mgodini. Kuna wakati nilitaka kujihusisha na madini kama broker nikakata mpaka leseni lakini ikawa longolongo nyingi na mambo ya kazi yakanibana nikashindwa nikashindwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…