Ndoto ni matokeo ya ubongo kupumzika, hazina maana yeyote zipuuzeni

Ndoto ni matokeo ya ubongo kupumzika, hazina maana yeyote zipuuzeni

Hapo unazungumzia hali ya mtu ambaye amesikia usingizi au amechoka na kuamua kujipumzikia kwa maana ya kulala na ndiyo ikatokea kuota ambapo ndio unasema ni matokeo ya ubongo kupumzika, upo sahihi kwa kiasi fulani lakini tukizungumzia kuhusu ndoto unajua kwamba inawezekana kutarajia kuota kuhusu jambo fulani kabla ya kulala?(ubongo kupumzika) yani mtu anataka kujua kuhusu jambo fulani mfano kujua kitu kilichopotea au kujua ukweli wa jambo fulani basi hutumia hiyo hali ya kulala huku akitarajia apate ndoto ambayo itahusu hilo jambo ambalo yeye anataka kulijua.

Je ushawahi kusikia vitu kama hivyo?
Sasa hapo mtu si tayari kashajipangia aote kuhusu nini?, ina maana hiyo sio ndoto ni mawazo/imagination ambazo hutumika hata na wapelelezi mkuu
 
Mtu halisi yupo katika ndoto anazoota.

Kupuuza ndoto ni kujitenga na kivuli chako.

Makinika.
 
Mi sipuuzi ndoto, kuna muda huwa naota vitu na vinatokea vile vile
 
Tatizo la watu wengi hufikiria ndoto ni kuhusu utabiri na maono tu kumbe haipo hivyo, ila kushughulika na ndoto kuna faida nyingi sana.
 
We ngoja siku uote unakula bakora makalioni halafu ukaamka asubuhi ukakuta alama zipo makalioni bila shaka utabadili mtizamo
 
Nimefuatilia ndoto nazoota zaidi ya miaka 10 sasa, zina maana kubwa sanaaa! Siwezi kuacha kufuatilia ndoto..........kuna baadhi ya mambo unaota leo then kesho yanatokea kweli.

Kuna kipindi nilishaota jamaa yangu mmoja anapatwa na janga flani kubwa sana nikapuuzia.......aisee kilichokuja kumtokea nilijuta sana kwanini sikumpa tahadhali mapema. So toka kipindi hiko nimekuwa makini sana na ndoto zote nazoota.
 
Back
Top Bottom