Ndoto ya Marekani kuivamia Urusi sasa yatimia

Ndoto ya Marekani kuivamia Urusi sasa yatimia

Akilihuru

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2022
Posts
1,512
Reaction score
2,980
Vipi wakuu,

Wakati vita hii ya Rusia na Ukraine inaanza...

1. Kuna watu walihisi kwamba vita hii ni ya Ukraine na Rusia peke yake, na kwamba kwa vile Ukraine ni kanchi kaunyonge basi Rusia anakwenda kumtandika M-ukraine kwa muda mfupi na kuichukua nchi yote ili iwe Jamhuri ya Rusia hapo baadae.

2. Kuna watu walihisi vita hii alievamiwa ni M-Ukraine peke yake, hivyo basi lolote linalotokea lipo juu ya kichwa chake mwenyewe (m-ukraine)

3. Wengine walihisi kwamba pamoja na kwamba M-Ukraine anapata support fulan ya silaha kutoka kwa wakubwa wakiongozwa na mtemi wa dunia (USA) ila hatokuwa na uwezo wa kufika mbali maana ngoma ya mtoto siku zote huwa haikeshi nk.

Sasa ndugu zangu niwambie tu kwamba hii vita ya Ukraine sio ya Ukraine tu kama wengi wanavyofikiria, bali ni vita ya Rusia na nchi bandia ya Marekani ambapo hilo jina la nchi ya Ukraine na ardhi yake vinatumika kama kichaka tu ili kuhalalisha kile kinachokwenda kufanywa na Marekani siku za usoni.

Putin analijua hili ndio maana anatumia nguvu kubwa kujaribu kupambana na kinvuli hicho cha Marekani, huku Marekani yenyewe original ikimchora na kuendelea kumchosha ili mwisho wa siku wamalize mchezo kiulaini kama vile mlevi anaeangushwa na ganda la ndizi.

Wakati Mmarekani anapanga mikakati yake kupitia Ukraine (Marekani bandia) kuna ndugu zetu warashia wa kwamtogole na mwanarumango walikuwa wakipanua midogo yao kumsifia Putin na jeshi lake, huku wengine wakiamini kwamba hakuna siku ambayo M-Ukraine ataweza kuifikia ardhi ya Putin kirahisi.

Sasa Mungu sio Athumani leo hii kila kitu kipo wazi kwamba Mmarekani anapoamua lake hakuna pa kwenda kujificha. Namaanisha hata ukiwa umejificha katika mji uliozungukwa na mitambo ya namna gani bado atakutumia mizinga huko huko ikufukunyue.

Hapa tunapoongea tayari Marekani ameshaingia hadi chumbani kwa Putin (Moscow) na kufanya maangamizi, huku kwao Marekani kina 50Cent na Jay Z wakiendelea kula mziki bila bughuza yoyote ya mabomu au rocket.

Kwa sasa inasemekana Putin anaishi pangoni kama ilivyokuwa kwa Sadam, lkn nakuhakikishieni, kama hajajitokeza mapema kuomba msamaha au kukimbilia China kuomba hifadhi basi ajiandae kukutana na yale aliyokutana nayo Saddam, Gadafi.

Picha ndio kwanza linaanza. Marekani original na NATO yake bado hawajaingia kazini.

Time will tell...
View attachment 2640177View attachment 2640178

Screenshot_20230530-165743.jpg
Screenshot_20230530-112018.jpg
Screenshot_20230530-170033.jpg
 
Umeandika kama uko Shimo la Tewa hujui lolote..Kwani mara ngapi watu wanauawawa Washngton hata watu 100 hata wanafunzi??? Hujawahi kuona?

Magaidi waliipiga hiyo marekani hapo hapo kwao na inapigwa mpaka leo hivyo usiseme mambo kama unahara...tulia..Putin yuko hapo na anaendelea na kazi hata leo asbh ameingia ofisni..Russia sio Zimbabwe subiri uone kinachofuata...
 
Boss, Umechambua kishabiki mno. Tunakosa la kujifunza kupitia uzi wako.
Funzo ni kwamba usije kumvamia jirani yako na kumtwanga mangumi bila sababu eti kwa vile wewe ni mkubwa na una nguvu kumshinda, huwezi jua alie nyuma ya huyo jirani yako.

Pengine ana undugu na mandinga, so akijua itakula kwako.
 
Back
Top Bottom