Ndoto ya usiku wa leo imenitisha, msaada kwa anayejua tafsiri au maana

Niliona kama nipo sehemu ambayo sio mazingira yangu ya kila siku, chini niliona mandhari ya kijani na magorofa marefu sana.
Kitendo cha kuona umepaa angani hio inamaanisha umevuka level uliokuepo mwanzo umeenda level ya juu.

Na ile level uliokua mwanzo, maadui zako walikua wanakumudu ila sasa upo level ya juu sio level zao (hawakuwezi).

Kwa tukio lililo mbele yako watachemka ila wanaweza wasikate tamaa wakaangalia wamejikwaa wapi wakaenda kujirekebisha na kukurudia tena siku nyingine... Sasa ili uendelee kua imara inabidi uimarishe imani yako muda wote.
 
Asante kwa ushauri na ufafanuzi huo na nimegundua napaswa kuimarisha imani yangu pamoja na kuepuka kukosana na watu bila sababu.
 
Punguza viazi kwenye daku na futari yako, ipo siku itakuua.

Anyway, kuna mjomba wangu nae alipata ndoto kama hiyo, hakumaliza wiki tukamuimbia parapanda na mashada juu.
 
Punguza viazi kwenye daku na futari yako, ipo siku itakuua.
Mimi huku nilipo ni mwaka sasa sijawahi hata kuona kiazi kwa macho.
Anyway, kuna mjomba wangu nae alipata ndoto kama hiyo, hakumaliza wiki tukamuimbia parapanda na mashada juu.
Kama ni hivyo sina budi kukubaliana na hali yoyote iliyo mbele yangu kwani sote ni wa Mungu na kwake tutarejea
 
kama ulivyoandika ni Kweli ipo hivi Roho zinaweza chukua sura ya mtu wa karbu au usyemjua hivyo una vita ya kichawi, unayo au inakujia hivyo unapaswa kuwa karbu na Mungu ndio maana ulifika mawinguni na hapo tafuta msaada wa maombi kwa watumishi wa kweli wanao Tumia Jina la Yesu vizuri , Maana Kuna uweze kano ukaondoka kwenye earth ๐ŸŒ ndio maana ulifika mawinguni ni suala la muda jitahid kuzingatia.
 
Ukiota unaingia maliwato usije ukajaribu kujisaidia tu...๐Ÿคฃ
 
Ulivyosema ni kweli kwamba napaswa kuongeza ibada na maombi kwasababu ni muda sasa nipo mbali na maswala ya kiimani. Ila kama kweli kuna maadui wananiwinda basi naamini hawataweza Mungu yupo.
 
Kama ni kweli ulipaa angani mpaka ukafika kilele cha juu mbona hujalowa maana usiku mzima mvua ilikuwa inanyesha
 
Kwanza mshukuru sana Mungu kwa hiyo ndoto.
Adui yako au mshindani wako hatakuweza.
Watafanya wawezalo kukuangusha lakini utawashinda.
Kupaa kwako ni kninuliwa juu yao katika ulimwengu wa roho.
Muombe Mungu aitimize hiyo ndoto katika ulimwengu wa damu na nyama.
 
Japo tafsiri ni nyingi na tofauti lakini nimegundua ndoto hii sio ya bure, kama ina matokeo yaliyo negative basi nipo katika wakati mbaya, ila kama ni positive basi kweli Mungu anilinde na kuniongoza wakati wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ