Ndoto ya usiku wa leo imenitisha, msaada kwa anayejua tafsiri au maana

Ndoto ya usiku wa leo imenitisha, msaada kwa anayejua tafsiri au maana

Uadui mkubwa na WA karibu utakaoushinda kwa karama kubwa zilizo ndani yako.Na chanzo ni UKUU wa kimaisha na kiroho uliozawadiwa na Mungu,au asili.
 
Uadui mkubwa na WA karibu utakaoushinda kwa karama kubwa zilizo ndani yako.Na chanzo ni UKUU wa kimaisha na kiroho uliozawadiwa na Mungu,au asili.
Mkuu lakini mbona mimi sina uadui wowote na mtu yeyote, ila kuhusu UKUU wa kimaisha na kiroho yaweza ikawa kweli maana ni mengi nimepitia na kuongoza wengine na hata kutegemewa katika baadhi ya mambo.
 
Ulivyosema ni kweli kwamba napaswa kuongeza ibada na maombi kwasababu ni muda sasa nipo mbali na maswala ya kiimani. Ila kama kweli kuna maadui wananiwinda basi naamini hawataweza Mungu yupo.
Sawa kama umelitambua hilo hivyo nenda ukaombewe hapo ulipo ni kama betri iliyo Isha chaji haiwezi kujichaji yenyewe Tena lazima ikachajiwe ndipo iwe na nguvu upya.
 
Kitendo cha kuona umepaa angani hio inamaanisha umevuka level uliokuepo mwanzo umeenda level ya juu.

Na ile level uliokua mwanzo, maadui zako walikua wanakumudu ila sasa upo level ya juu sio level zao (hawakuwezi).

Kwa tukio lililo mbele yako watachemka ila wanaweza wasikate tamaa wakaangalia wamejikwaa wapi wakaenda kujirekebisha na kukurudia tena siku nyingine... Sasa ili uendelee kua imara inabidi uimarishe imani yako muda wote.
Kuna rafiki yangu mmoja aliota akipambwa na kusifiwa na Mwijaku.

Sasa sijui na hii ina maana gani?
 
Milele amina....

Pia nakusalimu tena..... Assalamualaikum ndugu
Wewe ni Mtumishi wa Mungu Ndugu kama ulikua huna Taarifa chukua hiyo....! Ni Watu wawili tu wenye Hatima zao kwenye Ulimwengu wa Roho ambao huota Ndoto za Kupaa hewani, Mchawi na Mtumishi wa Mungu ndo maana nikakusalimia Bwana Yesu asifiwe.
 
Iyo ni kisaikolojia zaidi... inasababishwa na kumbukumbu ya matukio aliyopitia mchana kabla ya kulala.
Nilijaribu kumuuliza akadai hata sio mfuatiliaji wa huyo mtu wala hana muda wa kumfikiria.

Nikajaribu kutafakari labda ujumbe umejikita kwenye “Sifa” ya muotaji katika jamii.
 
Usiku wa leo nimeota ndoto ya ajabu sana, nimeota kuna mtu ninaye mfahamu ananikimbiza na kutaka kunidhuru.

Nikaanza kumkemea kwa maombi huku namnyooshea kidole, ghafla nikaanza kupaa angani mpaka nikafika kilele cha juu mawinguni, chini nikawa naona mazingira tofauti kabisa ambayo sijawahi kuyaona.

Wajuzi wa mambo ya ndoto naombeni mnijuze ndoto hii itakuwa na maana au tafsiri gani kwasababu imenitisha sana kwakweli.
wahi kwa mganga kama wewe ni mshirikina au jiweke kwenye maombi kama imani yako inaamini katika nguvu kubwa iliyoko kwenye maombi, uko katika vita ya kichawi
 
Back
Top Bottom