Pongezi kwa wananchi wa mikoa ya Kagera na Kigoma.
Inabidi suala la mikoa, wilaya na maeneobunge (majimbo) kugawanywa yasifanywe na Rais bali wananchi wahusishwe kwa maoni yao huru huku Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi ikihusishwa kama ilivyo nchini Kenya IEBC
Majukumu ya IEBC Kenya :
(5) Mipaka ya kila eneobunge italinganishwa kwa, inakaribiana sana, sawa na idadi ya wakazi katika eneobunge hilo, lakini idadi ya wakazi wa eneobunge inaweza kuwa kubwa au ndogo kuliko idadi ya kiasi cha watu kwa namna ambayo imetajwa katika Ibara ya (6) ili kuzingatia–
- (a) hali ya kijiografia na maeneo ya miji;
- (b) jamii ya eneo lile, kihistoria, kiuchumi na mshikamano wake wa kitamaduni; na
- (c) mbinu za mawasiliano.
(6) Idadi ya wakazi wa eneobunge au wadi inaweza kuwa kubwa au ndogo zaidi ya idadi ya watu kwenye eneo hilo kwa kiwango kisichozidi–
- (a) asilimia arubaini kwa majiji na maeneo yaliyo na idadi ya watu iliyotawanyika; na
- (b) asilimia thelathini kwa sehemu nyingine.
(7) Katika kurekebisha mipaka ya maeneobunge na wadi, Tume–
- (a) itashauriana na makundi yote husika; na
- (b) itandelea kufanya kazi kwa lengo la kuhakikisha kwamba idadi ya watu katika kila eneobunge na wadi, inakaribiana, sawa na idadi ya watu wa eneo hilo iliyokadiriwa.
(8) Ikiwezekana, Tume hii itabadilisha majina na mipaka ya maeneobunge na wadi, na idadi, majina na mipaka ya wadi.
(9) Kulingana na Ibara ya (1) (2),(3) na (4), majina na maelezo ya kina kuhusu mipaka ya maeneobunge na wadi iliyobuniwa na Tume, itachapishwa kwenye Gazeti Rasmi la Serikali, na itatekelezwa baada ya kuvunjwa kwanza kwa Bunge, kufuatia kuchapishwa kwake.
Source :
www.iebc.or.ke
Kutakuwa na maeneobunge mia mbili tisini kwa lengo la uchaguzi wa wabunge wa Baraza la Kitaifa.
afrocave.com