Ndoto za Chato kuwa mkoa zayeyuka baada ya mikoa jirani kugoma kuachia maeneo yao

Ndoto za Chato kuwa mkoa zayeyuka baada ya mikoa jirani kugoma kuachia maeneo yao

Yani uache kuigawa mikoa Kama Morogoro na Tabora ukaugawe Mkoa wa juzi Geita anyway tuache tu.
Wakati mnaigawa Rukwa Magufuri alikuwa Rais ? Au wakati mnaifanya Njombe yenye watu laki nane kuwa mkoa ni Magifuri ndiye aliyeidhinisha ?
 
Wakati mnaigawa Rukwa Magufuri alikuwa Rais ? Au wakati mnaifanya Njombe yenye watu laki nane kuwa mkoa ni Magifuri ndiye aliyeidhinisha ?
Umeshafika hayo maeneo uliyoyataja na kujionea jiografia yake na ugumu uliokuwepo katika kuyaongoza mpk kufikia hatua ya kuanzisha mikoa ya njombe, katavi, manyara, simiyu na Geita ambayo bado ikawa inalazimishwa kuchukua maeneo mengine kuanzisha huo Mkoa mpya? Kama hujawahi kufika hayo maeneo usikurupuke siku nyingine
 
Mzee unazijua requirements na uhalali wa kugawa mkoa?

Deep ndani kabisa ya moyo wako unaona ilikuwa haki kuanzisha mkoa wa Chato? Yaani mkiwa wawili tu na Mwenyezi Mungu mnatazamana face to face akakuuliza unadhani ilikuwa halali kuanzisha mkoa wa chato utajibu ndio?
Ndio unastahili. Mbona mikoa ya Njombe na Katavi ilianzishwa ilistahili ? Hadi leo hii Njombe ina watu laki nane tu na Rukwa ulikuwa mkoa mchanga ulioanzishwa 1974 mbona uligawanywa na kuzaa Katavi ? Hayo yote yalifanywa na Magufuri ?
 
Angalia mkoa wa geita na wilaya ya chato? Utengeneze chato kwa kutumia wilaya gani? Kuna vigezo hasa ukubwa wa eneo na vyanzo vya mapato..
Ushindwe kuigawa morogoro, dodoma na tabora uigawe chato? Kuwa serious jamaa
Morogoro na Tabora kuna mapato gani kuzidi Geita ?
 
Kwani chato ikiwa Mkoa kuna shida gani ? ,Akili za kujua wenyewe wanazo viongozi wa CCM wote ambao wameruhusu wakuu wa mikoa,mawaziri nk kutembelea Land cruiser za bei ghali hii ndio sababu nchi yenu ni masikini, matumizi ni makubwa mno

Hiyo Hospital ya Chato ambayo watu wengi hasa humu JF wanaipinga,imetusaidia wengine
Basi Nenda
 
Sasa asili na utamaduni vinakisaidia nini kwenye Sayansi na teconorojia ya Sasahivi?kutenga mikoa ni kulaisha uduma za jamii baada ya kutumia Siku mbili unafatilia uduma,utumie masaa tu,nimekutolea mfano kutoka Biaramulo mpaka Bukoba ambapo ni makao makuu ya mkoa ni zaidi ya masaa 8 hapo haujatokea vijiji vya mpakani,lakini kuja Chato inaweza kuwa masaa 3,sasa mtu kama huyu asili inamsadia nini?
Akikujibu nitag
 
Unapokuwa unajaribu kutoa hoja jaribu kusema ukweli, pia ukumbuke humu JF ni taifa kamili yaani kila kitu au kila taarifa ni rahisi kupatikana kuliko sehemu yoyote ile. Ukitoka Bukoba to Biharamulo hayajawahi kufika masaa nane , sanasana ni masaa matatu yakiwa mengi hadi nne tena hapo una gari za abiria.........kwa kukusaidia ni kwamba hayo
masaa nane unakuwa Nzega na kwendelea. Ukiitaka kujua sehemu zenye uhitaji mkubwa wa kumegwa nenda Tabora na Morogoro alafu urudi hapa
Tabora eneo kubwa ni mapori tu. Na uchumi mdogo.
 
Umeshafika hayo maeneo uliyoyataja na kujionea jiografia yake na ugumu uliokuwepo katika kuyaongoza mpk kufikia hatua ya kuanzisha mikoa ya njombe, katavi, manyara, simiyu na Geita ambayo bado ikawa inalazimishwa kuchukua maeneo mengine kuanzisha huo Mkoa mpya? Kama hujawahi kufika hayo maeneo usikurupuke siku nyingine
Hakuna mkoa nisiofika nchi hii wewe ndio unakurupuka. Unaujua umbali wa kutoka Ngara hadi makao makuu ya mkoa Bukoba ? Unajua umbali wa kutoka Kakonko hadi Makao makuu ya mkoa Kigoma ? Wewe ndio hujui kitu. Ukweli ni kwamba mikoa ya Njombe na Katavi ilianzishwa kwa sababu ya ushawishi ya viongozi wazawa waliokuwa huko kama spika wa bunge na waziri mkuu lakini haikustahili kabisa. Knachokusumbua ni chuki wala hujui chochote.
 
Umeshafika hayo maeneo uliyoyataja na kujionea jiografia yake na ugumu uliokuwepo katika kuyaongoza mpk kufikia hatua ya kuanzisha mikoa ya njombe, katavi, manyara, simiyu na Geita ambayo bado ikawa inalazimishwa kuchukua maeneo mengine kuanzisha huo Mkoa mpya? Kama hujawahi kufika hayo maeneo usikurupuke siku nyingine
Geita ilikua na jiografia gani ngumu kwenda Mwanza mkoani ? Hujui kitu. Nakuambia hivi mikoa hapa Tanzania hugawanywa kisiasa na si uhalisia.
 
Kwani Magufuli ndiye alikuwa Rais wakwanza aliyeanza kugawa mikoa mie nakumbuka mpaka nakuwa na uelewa nilkuta mikoa 20, Sasahivi kuna mikoa zaidi ya 25, Mkapa pamoja na Kikwete aligawa hatukuwahi kusikia makelele.Kwa Magufuli kwanini iwe nongwa? Nyinyi mnaopiga makelele ndio mashetani kwani ukiwepo mkoa wa Geita utapungukiwa nanini kama sio roho mbaya tu.
Hebu jaribu kusoma ulichoandika tena. Mkoa wa Geita uko toka wakati wa Kikwette? Unaongea nini wewe mpumbavu?

Tunachokataa ni kulazimisha mkoa ambao utaipunguza Kakonko, Muleba na Geita ili kuvihamishia Chato.
 
Ndoto ya wananchi wa Wilaya ya Chato kuwa Mkoa imegonga mwamba baada ya mikoa jirani ya Kigoma, Kagera na Mwanza kutokuwa tayari kuachia maeneo yake ili kuunda mkoa mpya wa Chato.

Wazo la Wilaya ya Chato kuwa Mkoa liliibuka tangu enzi za utawala wa awamu ya tano ya Hayati Rais John Magufuli, hata hivyo limekuwa likijadiliwa katika ngazi mbalimbali kabla ya leo kukataliwa rasmi.

Akiwa wilayani Chato Oktoba 14, 2021 kwenye kilele cha mbio za Mwenge, Rais Samia Suluhu Hassan alisema Serikali inaangalia vigezo vitakavyo ruhusu Chato kuwa Mkoa.

“Bado Chato haijawa mkoa kuna vigezo kadhaa bado tunaviangalia vigezo hivi vikikidhi basi tunakwenda kulimaliza jaambo hilo,” alisema.

Hata hivyo, Januari 10, 2023 imeelezwa kuwa Chato haina vigezo vya kuwa mkoa.

Hayo yamebainishwa katika Kikao cha Ushauri wa Mkoa (RCC) wa Geita, wakati Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu wa Mkoa wa Geita, Frank Mashauri aliposoma majibu ya barua ya Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) yenye kumbukumbu namba CBD.132/503/01B/26 ya Oktoba 2022.

Akifafanua kuhusu kukwama huko, Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amesema nia ya kuanzisha mkoa ilikuwepo na vikao vimefanyika na kupeleka mapendekezo kwenye mamlaka za juu.

Amesema Tamisemi imeandika barua kwenda kwenye mikoa jirani na mikoa hiyo imesema haipo tayari wilaya zake kwenda kuanzisha mkoa mpya wa Chato na kwa maana hiyo maombi ya Geita yamekataliwa.

“Mngeniambia mkoa ni kubwa tugawe inge- make sense (ingeeleweka), lakini mkoa huu haugawiki.

“Wakati mwingine unaweza kuwapa matumaini watu ambayo hayapo, sitaki kuwa muongo kuwapa watu matumaini ambayo hayapo nitakuwa mkuu wa mkoa wa ajabu sana,” amesema Shigela.

Shigela amesema akiwa mkuu wa Mkoa wa Tanga aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli alipinga masuala ya kugawa maeneo na hakuna mkoa wowote uliopendekeza kugawa maeneo yao na kuwataka viongozi kutojenga matumaini ambayo muda wake haujafika.

Amesema mkoa mwingine mkubwa ni Morogoro wenye halmashauri tisa kata 214 ukiwa na ukubwa wa eneo lenye urefu wa mita za mraba 73.

Awali akizungumza katika mkutano huo, Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma aliwataka wadau kutumia busara kupatikana kwa mkoa mpya wa Chato kwa kuwa hata kupatikana kwa mkoa mpya wa Geita haikuwa rahisi na kwamba kilichopo sasa ni kupingana wenywewe kwa wenyewe.

“Tusishikane uchawi na tusikatishane tamaa kuwaliza mikoa haitakubali kwakuwa kuna rasilimali lakini kama kweli mkoa upo sisi Geita tumeshatoa mapendelkezo na Tamisemi wasitutege wakiona inapendeza wataugawa,” amesema Msukuma.

Kwa upande wake Mwenyekiti halmashauri ya Mbogwe, Vicent Busigwa amesema mvutano uliopo ni wa viongozi na sio wa wananchi.

Busigwa alisema Tamisemi ishauriwe kuliangalia upya jambo hili ili kupeleka huduma za wanachi karibu.

Naye Mbunge wa Mbogwe, Nicodemas Maganga, amesema, “Mwenyekiti Kanda hii ya Ziwa wananchi wote wanasubiri Chato kutangazwa kuwa mkoa na ukumbuke, Rais akizima mwenge Chato wananchi walikua wakisubiri mkoa kutangazwa jambo hili limekuwa siku nyingi.”

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom