Ndoto za Chato kuwa mkoa zayeyuka baada ya mikoa jirani kugoma kuachia maeneo yao

Ndoto za Chato kuwa mkoa zayeyuka baada ya mikoa jirani kugoma kuachia maeneo yao

Ndio unastahili. Mbona mikoa ya Njombe na Katavi ilianzishwa ilistahili ? Hadi leo hii Njombe ina watu laki nane tu na Rukwa ulikuwa mkoa mchanga ulioanzishwa 1974 mbona uligawanywa na kuzaa Katavi ? Hayo yote yalifanywa na Magufuri ?
Nani alikuambia kuwa kigezo kikubwa cha mkoa kugawanywa ni idadi ya watu? Kigezo kikubwa ni ukubwa wa eneo husika ambalo huelezea umbali wa wananchi kupata huduma za kiutawala. Na kigezo kingine ni uwingi na ukubwa wa shughuli za kiuchumi. Utambue kuwa mkoa wa Njombe ni miongoni mwa mikoa 6 yenye highest per capita income kwa Tanzania, mingine ni Dar, Iringa, Mbeya, Ruvuma na Kilimanjaro.

Rais Magufuli: Mkoa wa Njombe hasa mji wa Makambako ndio mji wenye nyumba na Makazi bora Tanzania
 
Hakuna mkoa nisiofika nchi hii wewe ndio unakurupuka. Unaujua umbali wa kutoka Ngara hadi makao makuu ya mkoa Bukoba ? Unajua umbali wa kutoka Kakonko hadi Makao makuu ya mkoa Kigoma ? Wewe ndio hujui kitu. Ukweli ni kwamba mikoa ya Njombe na Katavi ilianzishwa kwa sababu ya ushawishi ya viongozi wazawa waliokuwa huko kama spika wa bunge na waziri mkuu lakini haikustahili kabisa. Knachokusumbua ni chuki wala hujui chochote.
Hujui kitu. Kabla ya mkoa wa Njombe kuanzishwa, umbali kutoka Iringa mpaka Songea ilikuwa 460km, wakati umbali toka Mwanza mpaka Shinyanga ni 152km. Umbali kutoka ni 422km. Kutoka Sumbawabga hadi Kigoma ni 408km. Umbali toka Geita mpaka Bukoba ni 300km.

Kulikuwa na sababu za msingi za kuanzishwa mkoa wa Njombe, Geita na Katavi.

Vigezo vikubwa:

1) ukubwa na umbali mpaka makao makuu ya mkoa

2) ukubwa na uwingi wa shughuli za kiuchumi

3) Idadi ya watu

Hata kama kutakuwa na haja ya kuongeza mkoa utakaopunguza umbali wa umbali kati ya Geita na Bujoba, basi makao makuu hayatakuwa Chato. Chato ni karibu sana na Geita.

Yaani Njombe iliyo ya pili kwa per capita income, unasema haikuwa na vigezo! Lazima utakuwa huna uelewa wa vitu vingi.
 
Morogoro,Lindi na Tabora hiyo ndiyo mikoa yenye uhitaji wa kugawanywa.........huko Chato ilikuwa usumbufu tu
Kote huko wala hakuna haja ya kugawa,hata zilizokwusha gawanywa wala hakukuwa na sababu ya kufanya hivyo.

Kinachotakiwa ni ugatuzi kamili wa madaraka. Maana hata Mwanza au Arusha au Katavi au Rukwa kwa ukubwa wa maeneo yao itakapokuwa populated na very dense kama Dar,bado wazo la kugawa mikoa hiyo litakuja tena mezani muda utakapofika,vivyo hivyo na mikoa mingine ambayo bado haijagawanywa.

Tutakuwa na mikoa mingapi kwenye nchi moya?
Sioni kwamba ni afya kugawagawa mikoa.
 
Unaijua Njombe? Ujue Njombe ni ya pili kwa per capita baada ya Dar. Chato ni ya ngapi? Unafahamu umali wa kutoka Iringa mpaka Njombe (230km), Mbeya mpaka Njombe (236km), Songea mpaka Njombe (228km), Morogoro mpaka Njombe (525km)? Haya niambie umbali wa kutoka Geita mpaka Chato, Bukoba mpaka Chato.

Tusishabikie mambo ya kijinga. Fikra za Chato kuwa mkoa zilikuwa za kijinga kabisa. Hayo ni kati ya mambo ambayo yalisababishia kutilia mashaka juu ya utimamu wa akili ya marehemu.

Chato kama yalivyo maeneo mengine ya nchi, ina haki ya kuwa na huduma za kijamii, lakini huduma za kiutawala lazima zifuate vigezo vya kitaifa. In short, he was not a leader. Ameligharimu sana Taifa katika mambo mengi kuanzia uwekezaji, ajira, utawala wa kisheria, demokrasia, n.k. Tunashukuru utawala wake ulidumu kwa muda mfupi, japo hatufurahii kifo chake, kama ambavyo hatuwezi kufurahia kifo cha binadamu mwingine yeyote.
Narudia kugawa mikoa hapa TZ ni siasa tu
 
Kote huko wala hakuna haja ya kugawa,hata zilizokwusha gawanywa wala hakukuwa na sababu ya kufanya hivyo.

Kinachotakiwa ni ugatuzi kamili wa madaraka. Maana hata Mwanza au Arusha au Katavi au Rukwa kwa ukubwa wa maeneo yao itakapokuwa populated na very dense kama Dar,bado wazo la kugawa mikoa hiyo litakuja tena mezani muda utakapofika,vivyo hivyo na mikoa mingine ambayo bado haijagawanywa.

Tutakuwa na mikoa mingapi kwenye nchi moya?
Sioni kwamba ni afya kugawagawa mikoa.
Badala ya kugawa afadhali tuunganishe na kugatua.
 
Kote huko wala hakuna haja ya kugawa,hata zilizokwusha gawanywa wala hakukuwa na sababu ya kufanya hivyo.

Kinachotakiwa ni ugatuzi kamili wa madaraka. Maana hata Mwanza au Arusha au Katavi au Rukwa kwa ukubwa wa maeneo yao itakapokuwa populated na very dense kama Dar,bado wazo la kugawa mikoa hiyo litakuja tena mezani muda utakapofika,vivyo hivyo na mikoa mingine ambayo bado haijagawanywa.

Tutakuwa na mikoa mingapi kwenye nchi moya?
Sioni kwamba ni afya kugawagawa mikoa.
Kuna umuhimu wake mkuu,binafsi nimeona impact ya kuugawa mkoa wa Mbeya na kuupata Songwe......kuna baadhi ya wilaya zilisahaulika kama Ileje,now angalau zimefikiwa na maendeleo
 
Kuna umuhimu wake mkuu,binafsi nimeona impact ya kuugawa mkoa wa Mbeya na kuupata Songwe......kuna baadhi ya wilaya zilisahaulika kama Ileje,now angalau zimefikiwa na maendeleo
Mkuu chato haina ukubwa huo wa kufanywa kuwa mkoa zaidi ya siasa tu
 
Wewe ndio unapayuka, Chato Haina vigezo vya kuwa mkoa hata kuwa wilaya peke yake yalikuwa ni makosa kutokana na uhuni wa Magufuli kupitia kwa shoga yake mkapa kama walivyouza nyumba za serikali! Uwili wa kishetani na kifisadi! Nyau we!
nyau ni mamaako,kahaba wa kiume wee
 
Ndoto ya wananchi wa Wilaya ya Chato kuwa Mkoa imegonga mwamba baada ya mikoa jirani ya Kigoma, Kagera na Mwanza kutokuwa tayari kuachia maeneo yake ili kuunda mkoa mpya wa Chato.

Wazo la Wilaya ya Chato kuwa Mkoa liliibuka tangu enzi za utawala wa awamu ya tano ya Hayati Rais John Magufuli, hata hivyo limekuwa likijadiliwa katika ngazi mbalimbali kabla ya leo kukataliwa rasmi.

Akiwa wilayani Chato Oktoba 14, 2021 kwenye kilele cha mbio za Mwenge, Rais Samia Suluhu Hassan alisema Serikali inaangalia vigezo vitakavyo ruhusu Chato kuwa Mkoa.

“Bado Chato haijawa mkoa kuna vigezo kadhaa bado tunaviangalia vigezo hivi vikikidhi basi tunakwenda kulimaliza jaambo hilo,” alisema.

Hata hivyo, Januari 10, 2023 imeelezwa kuwa Chato haina vigezo vya kuwa mkoa.

Hayo yamebainishwa katika Kikao cha Ushauri wa Mkoa (RCC) wa Geita, wakati Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu wa Mkoa wa Geita, Frank Mashauri aliposoma majibu ya barua ya Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) yenye kumbukumbu namba CBD.132/503/01B/26 ya Oktoba 2022.

Akifafanua kuhusu kukwama huko, Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amesema nia ya kuanzisha mkoa ilikuwepo na vikao vimefanyika na kupeleka mapendekezo kwenye mamlaka za juu.

Amesema Tamisemi imeandika barua kwenda kwenye mikoa jirani na mikoa hiyo imesema haipo tayari wilaya zake kwenda kuanzisha mkoa mpya wa Chato na kwa maana hiyo maombi ya Geita yamekataliwa.

“Mngeniambia mkoa ni kubwa tugawe inge- make sense (ingeeleweka), lakini mkoa huu haugawiki.

“Wakati mwingine unaweza kuwapa matumaini watu ambayo hayapo, sitaki kuwa muongo kuwapa watu matumaini ambayo hayapo nitakuwa mkuu wa mkoa wa ajabu sana,” amesema Shigela.

Shigela amesema akiwa mkuu wa Mkoa wa Tanga aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli alipinga masuala ya kugawa maeneo na hakuna mkoa wowote uliopendekeza kugawa maeneo yao na kuwataka viongozi kutojenga matumaini ambayo muda wake haujafika.

Amesema mkoa mwingine mkubwa ni Morogoro wenye halmashauri tisa kata 214 ukiwa na ukubwa wa eneo lenye urefu wa mita za mraba 73.

Awali akizungumza katika mkutano huo, Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma aliwataka wadau kutumia busara kupatikana kwa mkoa mpya wa Chato kwa kuwa hata kupatikana kwa mkoa mpya wa Geita haikuwa rahisi na kwamba kilichopo sasa ni kupingana wenywewe kwa wenyewe.

“Tusishikane uchawi na tusikatishane tamaa kuwaliza mikoa haitakubali kwakuwa kuna rasilimali lakini kama kweli mkoa upo sisi Geita tumeshatoa mapendelkezo na Tamisemi wasitutege wakiona inapendeza wataugawa,” amesema Msukuma.

Kwa upande wake Mwenyekiti halmashauri ya Mbogwe, Vicent Busigwa amesema mvutano uliopo ni wa viongozi na sio wa wananchi.

Busigwa alisema Tamisemi ishauriwe kuliangalia upya jambo hili ili kupeleka huduma za wanachi karibu.

Naye Mbunge wa Mbogwe, Nicodemas Maganga, amesema, “Mwenyekiti Kanda hii ya Ziwa wananchi wote wanasubiri Chato kutangazwa kuwa mkoa na ukumbuke, Rais akizima mwenge Chato wananchi walikua wakisubiri mkoa kutangazwa jambo hili limekuwa siku nyingi.”

Chanzo: Mwananchi
nadhani ni busara kwa chato kupewa mkoa.hebu fkiria mwananchi atoke kakonko kwenda kufuata huduma kigoma mjini hii si sawa.nadhani imegwe biharamulo,kakonko,mbogwe ziende kuunda mkoa mpya wa chato.wanaokataa chato kuwa mkoa ni wanasiasa na sababu kubwa watapoteza majimbo ndo maana wanang'ang'ania chato isiwe mkoa.kwa ushauri na mawazo yangu wanasiasa wangeweka maslahi mapama kwa wananchi wao.kutoka kibondo kwenda kigoma ni zaidi ya masaa saba sasa huku si kuwaumiza wananchi?
 
Hakuna tena huo upuuzi wa matakwa ya jiwe
 
Back
Top Bottom