Ndoto za Chato kuwa mkoa zayeyuka baada ya mikoa jirani kugoma kuachia maeneo yao

Ndio unastahili. Mbona mikoa ya Njombe na Katavi ilianzishwa ilistahili ? Hadi leo hii Njombe ina watu laki nane tu na Rukwa ulikuwa mkoa mchanga ulioanzishwa 1974 mbona uligawanywa na kuzaa Katavi ? Hayo yote yalifanywa na Magufuri ?
Nani alikuambia kuwa kigezo kikubwa cha mkoa kugawanywa ni idadi ya watu? Kigezo kikubwa ni ukubwa wa eneo husika ambalo huelezea umbali wa wananchi kupata huduma za kiutawala. Na kigezo kingine ni uwingi na ukubwa wa shughuli za kiuchumi. Utambue kuwa mkoa wa Njombe ni miongoni mwa mikoa 6 yenye highest per capita income kwa Tanzania, mingine ni Dar, Iringa, Mbeya, Ruvuma na Kilimanjaro.

Rais Magufuli: Mkoa wa Njombe hasa mji wa Makambako ndio mji wenye nyumba na Makazi bora Tanzania
 
Hujui kitu. Kabla ya mkoa wa Njombe kuanzishwa, umbali kutoka Iringa mpaka Songea ilikuwa 460km, wakati umbali toka Mwanza mpaka Shinyanga ni 152km. Umbali kutoka ni 422km. Kutoka Sumbawabga hadi Kigoma ni 408km. Umbali toka Geita mpaka Bukoba ni 300km.

Kulikuwa na sababu za msingi za kuanzishwa mkoa wa Njombe, Geita na Katavi.

Vigezo vikubwa:

1) ukubwa na umbali mpaka makao makuu ya mkoa

2) ukubwa na uwingi wa shughuli za kiuchumi

3) Idadi ya watu

Hata kama kutakuwa na haja ya kuongeza mkoa utakaopunguza umbali wa umbali kati ya Geita na Bujoba, basi makao makuu hayatakuwa Chato. Chato ni karibu sana na Geita.

Yaani Njombe iliyo ya pili kwa per capita income, unasema haikuwa na vigezo! Lazima utakuwa huna uelewa wa vitu vingi.
 
Morogoro,Lindi na Tabora hiyo ndiyo mikoa yenye uhitaji wa kugawanywa.........huko Chato ilikuwa usumbufu tu
Kote huko wala hakuna haja ya kugawa,hata zilizokwusha gawanywa wala hakukuwa na sababu ya kufanya hivyo.

Kinachotakiwa ni ugatuzi kamili wa madaraka. Maana hata Mwanza au Arusha au Katavi au Rukwa kwa ukubwa wa maeneo yao itakapokuwa populated na very dense kama Dar,bado wazo la kugawa mikoa hiyo litakuja tena mezani muda utakapofika,vivyo hivyo na mikoa mingine ambayo bado haijagawanywa.

Tutakuwa na mikoa mingapi kwenye nchi moya?
Sioni kwamba ni afya kugawagawa mikoa.
 
Narudia kugawa mikoa hapa TZ ni siasa tu
 
Badala ya kugawa afadhali tuunganishe na kugatua.
 
Kuna umuhimu wake mkuu,binafsi nimeona impact ya kuugawa mkoa wa Mbeya na kuupata Songwe......kuna baadhi ya wilaya zilisahaulika kama Ileje,now angalau zimefikiwa na maendeleo
 
Kuna umuhimu wake mkuu,binafsi nimeona impact ya kuugawa mkoa wa Mbeya na kuupata Songwe......kuna baadhi ya wilaya zilisahaulika kama Ileje,now angalau zimefikiwa na maendeleo
Mkuu chato haina ukubwa huo wa kufanywa kuwa mkoa zaidi ya siasa tu
 
Wewe ndio unapayuka, Chato Haina vigezo vya kuwa mkoa hata kuwa wilaya peke yake yalikuwa ni makosa kutokana na uhuni wa Magufuli kupitia kwa shoga yake mkapa kama walivyouza nyumba za serikali! Uwili wa kishetani na kifisadi! Nyau we!
nyau ni mamaako,kahaba wa kiume wee
 
nadhani ni busara kwa chato kupewa mkoa.hebu fkiria mwananchi atoke kakonko kwenda kufuata huduma kigoma mjini hii si sawa.nadhani imegwe biharamulo,kakonko,mbogwe ziende kuunda mkoa mpya wa chato.wanaokataa chato kuwa mkoa ni wanasiasa na sababu kubwa watapoteza majimbo ndo maana wanang'ang'ania chato isiwe mkoa.kwa ushauri na mawazo yangu wanasiasa wangeweka maslahi mapama kwa wananchi wao.kutoka kibondo kwenda kigoma ni zaidi ya masaa saba sasa huku si kuwaumiza wananchi?
 
Hakuna tena huo upuuzi wa matakwa ya jiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…