Ndoto za Chato kuwa mkoa zayeyuka baada ya mikoa jirani kugoma kuachia maeneo yao

Kote huko wala hakuna haja ya kugawa,hata zilizokwusha gawanywa wala hakukuwa na sababu ya kufanya hivyo.

Kinachotakiwa ni ugatuzi kamili wa madaraka. Maana hata Mwanza au Arusha au Katavi au Rukwa kwa ukubwa wa maeneo yao itakapokuwa populated na very dense kama Dar,bado wazo la kugawa mikoa hiyo litakuja tena mezani muda utakapofika,vivyo hivyo na mikoa mingine ambayo bado haijagawanywa.

Tutakuwa na mikoa mingapi kwenye nchi moya?
Sioni kwamba ni afya kugawagawa mikoa.
Uko sahihi mkuu, hakuna tija ya kugawa mikoa, ingebaki ile ile
 
Ndoto ya wananchi wa Wilaya ya Chato kuwa Mkoa imegonga mwamba baada ya mikoa jirani ya Kigoma, Kagera na Mwanza kutokuwa tayari kuachia maeneo yake ili kuunda mkoa mpya wa Chato.

Wazo la Wilaya ya Chato kuwa Mkoa liliibuka tangu enzi za utawala wa awamu ya tano ya Hayati Rais John Magufuli, hata hivyo limekuwa likijadiliwa katika ngazi mbalimbali kabla ya leo kukataliwa rasmi.

Akiwa wilayani Chato Oktoba 14, 2021 kwenye kilele cha mbio za Mwenge, Rais Samia Suluhu Hassan alisema Serikali inaangalia vigezo vitakavyo ruhusu Chato kuwa Mkoa.

“Bado Chato haijawa mkoa kuna vigezo kadhaa bado tunaviangalia vigezo hivi vikikidhi basi tunakwenda kulimaliza jaambo hilo,” alisema.

Hata hivyo, Januari 10, 2023 imeelezwa kuwa Chato haina vigezo vya kuwa mkoa.

Hayo yamebainishwa katika Kikao cha Ushauri wa Mkoa (RCC) wa Geita, wakati Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu wa Mkoa wa Geita, Frank Mashauri aliposoma majibu ya barua ya Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) yenye kumbukumbu namba CBD.132/503/01B/26 ya Oktoba 2022.

Akifafanua kuhusu kukwama huko, Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amesema nia ya kuanzisha mkoa ilikuwepo na vikao vimefanyika na kupeleka mapendekezo kwenye mamlaka za juu.

Amesema Tamisemi imeandika barua kwenda kwenye mikoa jirani na mikoa hiyo imesema haipo tayari wilaya zake kwenda kuanzisha mkoa mpya wa Chato na kwa maana hiyo maombi ya Geita yamekataliwa.

“Mngeniambia mkoa ni kubwa tugawe inge- make sense (ingeeleweka), lakini mkoa huu haugawiki.

“Wakati mwingine unaweza kuwapa matumaini watu ambayo hayapo, sitaki kuwa muongo kuwapa watu matumaini ambayo hayapo nitakuwa mkuu wa mkoa wa ajabu sana,” amesema Shigela.

Shigela amesema akiwa mkuu wa Mkoa wa Tanga aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli alipinga masuala ya kugawa maeneo na hakuna mkoa wowote uliopendekeza kugawa maeneo yao na kuwataka viongozi kutojenga matumaini ambayo muda wake haujafika.

Amesema mkoa mwingine mkubwa ni Morogoro wenye halmashauri tisa kata 214 ukiwa na ukubwa wa eneo lenye urefu wa mita za mraba 73.

Awali akizungumza katika mkutano huo, Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma aliwataka wadau kutumia busara kupatikana kwa mkoa mpya wa Chato kwa kuwa hata kupatikana kwa mkoa mpya wa Geita haikuwa rahisi na kwamba kilichopo sasa ni kupingana wenywewe kwa wenyewe.

“Tusishikane uchawi na tusikatishane tamaa kuwaliza mikoa haitakubali kwakuwa kuna rasilimali lakini kama kweli mkoa upo sisi Geita tumeshatoa mapendelkezo na Tamisemi wasitutege wakiona inapendeza wataugawa,” amesema Msukuma.

Kwa upande wake Mwenyekiti halmashauri ya Mbogwe, Vicent Busigwa amesema mvutano uliopo ni wa viongozi na sio wa wananchi.

Busigwa alisema Tamisemi ishauriwe kuliangalia upya jambo hili ili kupeleka huduma za wanachi karibu.

Naye Mbunge wa Mbogwe, Nicodemas Maganga, amesema, “Mwenyekiti Kanda hii ya Ziwa wananchi wote wanasubiri Chato kutangazwa kuwa mkoa na ukumbuke, Rais akizima mwenge Chato wananchi walikua wakisubiri mkoa kutangazwa jambo hili limekuwa siku nyingi.”

Chanzo: Mwananchi
Mods unganisha huu uzi
 
nadhani ni busara kwa chato kupewa mkoa.hebu fkiria mwananchi atoke kakonko kwenda kufuata huduma kigoma mjini hii si sawa.nadhani imegwe biharamulo,kakonko,mbogwe ziende kuunda mkoa mpya wa chato.wanaokataa chato kuwa mkoa ni wanasiasa na sababu kubwa watapoteza majimbo ndo maana wanang'ang'ania chato isiwe mkoa.kwa ushauri na mawazo yangu wanasiasa wangeweka maslahi mapama kwa wananchi wao.kutoka kibondo kwenda kigoma ni zaidi ya masaa saba sasa huku si kuwaumiza wananchi?
Mkuu kwani hizo huduma zikisogezwa bila kufanya Chato kuwa mkoa kuna tatizo gani? Mana mimi siyo mtaalamu kwenye mambo ya utawala
 
Kwani chato ina umaaarufu gani hapa nchini?
 
HONGERA SAMIA KWA KUWANYIMA CHATO MKOA, SASA WATU WA CHATO WAFIE KWENYE UMASIKINI KABISA. UNGEWAPA WANGEJIDAI.. HUKU BUKOBA, KIGOMA TUNAFIURHIA SANA KWA KUWAKOMESHA HASA HUYO JIWE
 
Kuna watu wa Mlimba ,Mahenge utazani wanaenda Kigoma masaa wanayotumia kusafiri ndani ya Mkoa

Kuna sehemu huko Mahenge mpaka jua liwake watu ndio wapatikane kwenye Simu..ni leo hii 2023.
Mkoa wa Morogoro ni mkubwa sana
 
Ndoto ya wananchi wa Wilaya ya Chato kuwa Mkoa imegonga mwamba baada ya mikoa jirani ya Kigoma, Kagera na Mwanza kutokuwa tayari kuachia maeneo yake ili kuunda mkoa mpya wa Chato.

Wazo la Wilaya ya Chato kuwa Mkoa liliibuka tangu enzi za utawala wa awamu ya tano ya Hayati Rais John Magufuli, hata hivyo limekuwa likijadiliwa katika ngazi mbalimbali kabla ya leo kukataliwa rasmi.

Akiwa wilayani Chato Oktoba 14, 2021 kwenye kilele cha mbio za Mwenge, Rais Samia Suluhu Hassan alisema Serikali inaangalia vigezo vitakavyo ruhusu Chato kuwa Mkoa.

“Bado Chato haijawa mkoa kuna vigezo kadhaa bado tunaviangalia vigezo hivi vikikidhi basi tunakwenda kulimaliza jaambo hilo,” alisema.

Hata hivyo, Januari 10, 2023 imeelezwa kuwa Chato haina vigezo vya kuwa mkoa.

Hayo yamebainishwa katika Kikao cha Ushauri wa Mkoa (RCC) wa Geita, wakati Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu wa Mkoa wa Geita, Frank Mashauri aliposoma majibu ya barua ya Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) yenye kumbukumbu namba CBD.132/503/01B/26 ya Oktoba 2022.

Akifafanua kuhusu kukwama huko, Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amesema nia ya kuanzisha mkoa ilikuwepo na vikao vimefanyika na kupeleka mapendekezo kwenye mamlaka za juu.

Amesema Tamisemi imeandika barua kwenda kwenye mikoa jirani na mikoa hiyo imesema haipo tayari wilaya zake kwenda kuanzisha mkoa mpya wa Chato na kwa maana hiyo maombi ya Geita yamekataliwa.

“Mngeniambia mkoa ni kubwa tugawe inge- make sense (ingeeleweka), lakini mkoa huu haugawiki.

“Wakati mwingine unaweza kuwapa matumaini watu ambayo hayapo, sitaki kuwa muongo kuwapa watu matumaini ambayo hayapo nitakuwa mkuu wa mkoa wa ajabu sana,” amesema Shigela.

Shigela amesema akiwa mkuu wa Mkoa wa Tanga aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli alipinga masuala ya kugawa maeneo na hakuna mkoa wowote uliopendekeza kugawa maeneo yao na kuwataka viongozi kutojenga matumaini ambayo muda wake haujafika.

Amesema mkoa mwingine mkubwa ni Morogoro wenye halmashauri tisa kata 214 ukiwa na ukubwa wa eneo lenye urefu wa mita za mraba 73.

Awali akizungumza katika mkutano huo, Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma aliwataka wadau kutumia busara kupatikana kwa mkoa mpya wa Chato kwa kuwa hata kupatikana kwa mkoa mpya wa Geita haikuwa rahisi na kwamba kilichopo sasa ni kupingana wenywewe kwa wenyewe.

“Tusishikane uchawi na tusikatishane tamaa kuwaliza mikoa haitakubali kwakuwa kuna rasilimali lakini kama kweli mkoa upo sisi Geita tumeshatoa mapendelkezo na Tamisemi wasitutege wakiona inapendeza wataugawa,” amesema Msukuma.

Kwa upande wake Mwenyekiti halmashauri ya Mbogwe, Vicent Busigwa amesema mvutano uliopo ni wa viongozi na sio wa wananchi.

Busigwa alisema Tamisemi ishauriwe kuliangalia upya jambo hili ili kupeleka huduma za wanachi karibu.

Naye Mbunge wa Mbogwe, Nicodemas Maganga, amesema, “Mwenyekiti Kanda hii ya Ziwa wananchi wote wanasubiri Chato kutangazwa kuwa mkoa na ukumbuke, Rais akizima mwenge Chato wananchi walikua wakisubiri mkoa kutangazwa jambo hili limekuwa siku nyingi.”

Chanzo: Mwananchi
ulikuwa upuuzi mkubwa sana, matakwa ya kikabila kugawa nchi kama chapati:
Ni ujinga tu hata kugawa mikoa kwa kisingizio cha huduma, kwani say mkoa wa Arusha usinge gawanywa na Manyara, hao wa Babati na kiteto wakajengewa hospitali kama mount meru, huduma za mkoani wakaafikishiwa wilayani kwao ingekuwa shida?
Nchi ina wapuuzi sana sometimes bora mkoloni angebaki tu
 
Hivi wewe kazi yako kutukana wasukuma tu? Kwanza tuoneshe sehemu ambayo Magufuli alisema anataka kuanzisha mkoa wa chato?
wacha watu wateme nyongo, watu kwa miaka 60 utumwani utafikiri miaka 400 ya waisreaeli Jangwani
 
Lkn bado kulikuwa na watu wanalifanya kama ni jambo la lazima hasa kipindi Magufuli yupo madarakani.
Yule jamaa angeendelea kuwepo NHC wangejenga magorofa mengi Chato

Wizara ya Utalii ingejenga hotel nyingi.

Ndege zingelazimishwa kutua kule
 
Asante Mungu kwa kutuondolea yule Ibilisi mfitini, mbinafsi, muuaji , fisadi kubwa na lichawi likubwa lililoharibu akili za wananchi wengi ambao mpaka sasa hawawezi kukaa kutwa bila kumtaja
Ndio ujue sometimes tunaishi na shetani bila kujua, damu za watu zinalia sana, Mama samia Mungu akupe maisha marefu , yani hutaki damu ya mtu mikononi mwako.
 
Back
Top Bottom