Ndoto za usiku zinazo husiana na kuota nyoka ukiwa umelala

Ndoto za usiku zinazo husiana na kuota nyoka ukiwa umelala

Binadamu anapolala basi Ubongo wenyewe unaendelea na kazi yake kwa hiyo bado unahitaji oxygeni tena kwa wingi... unapokosa au kupata pungufu ndiyo unaanza kuota unapanda milima na mabonde ama kukimbizwa na Simba, Chatu nk.

Na ndiyo maana ukishtuka ni lazima uvute hewa kwa fujo sana kufidia... Pia namna ya kulala ndiyo husababisha what called Jinamizi... ukitaka kupata ndoto za ajabu lala chali uone moto wake.. unaweza kuhama nyumba ukasema wanakuchawia.
 
Nje ya mada;

Mara nyingi sana naota nikiwa napaa, kuna anayepatwa na hili pia?

Tafsiri?
 
ndugu yangu mwanamke ameota kakabwa na nyoka wawili wakubwa na wanamuingilia kimwili, hii ina maana gani?
 
Nimeota nyoka mdogo sn km mnyoo ameniingia kwenye kidole changu cha mkono ila nikiwa ndotoni bado nikapata hofu kuwa nyoka huyo mdg atakuwa mkubwa sana badae itakuwajee sasa wkt Yupo kidoleni mwangu, hii ndoto ina maana gani mkuu ?
Mi nimeota nyoka black alikuwa katika mti pembeni ya nyumba kisha akaingia ndani nikaanza kumfukuza. Akachomoka mbio akaingia nyumba ya jirani nako akafukuzwa akaingia shimoni.

Niliporudi nikakuta katika mti ule ule jirani na ninapoishi kuna nyoka wa kijani nikaanza kumfurusha tena akaanza kupiga kelele vibaya mno. Alipodondoka chini ya mti tu nikastuka. MziziMkavu naomba tafsiri mkuu
Noma sana!
 
Ndoto za Nyoka zinaashiria mtoto wa kiume, mtu asiyekuwa na heshima, Adui, mali iliyofichwa, ushirikina, mabadiliko, uwezo, kiongozi mbaya, na mwanamke.

Nyoka katika ndoto anawakilisha mtu anayeishi Bondeni, vilevile

Nyoka katika ndoto ni ishara ya uadui kutoka kwa wakwe zako au watoto au ni ishara ya uovu na wivu kutoka kwa majirani zako.

Ukiota unamuona nyoka maana yake ni kwamba utadanganywa na mkeo au mumeo.
Sasa sisi wengine siyo kuota tu tunaamka asubuhi wako uvunguni mwa vitanda na wakati mwingine tumejifunika nao shuka
 
Unaandamwa na maaduwi zako kwa ubaya wa uchawi jihadhari sana.
Mkuu mimi nimeota nimeng'atwa na nyoka wa kijani kichwani yule green mamba tukapambana tukamua. Alafu nikakimbizwa hospitalini kupewa huduma ndio nikashtuka . Sijui hii ndoto inamaana gani ?
 
kua makini hapo ulipo usije ukaanguka
Mkuu mimi nimeota nimeng'atwa na nyoka wa kijani kichwani yule green mamba tukapambana tukamua. Alafu nikakimbizwa hospitalini kupewa huduma ndio nikashtuka . Sijui hii ndoto inamaana gani
 
Back
Top Bottom