Ndugai acha kuwaona watanzania ni wajinga. Kama Hayati Magufuli alipotoshwa, wewe kama Spika kwanini haukumshauri?

Hapa umegongelea msumari.
 
Mtu anajiita jiwe yeye anajua kila kitu na hashauriki ungekua wewe spika ungefanya nini na watoto wanakutegemea... Uliona kilichomkuta CAG ASAD kwa sasa kusimamia ukweli akakosa kiti chake
Hatutaki viongozi wa Aina hi.
Hawatufai hata kidogo..
 
Ndugai ni mnafiki mkubwa hafai kuwa kiongozi hata kwa nusu dak
 
Hawa watu ni wapumbavu sn
 
Ndungai kama aliona Rais amepotoshwa na yeye anajua ukweli, alipaswa kujiuzulu! Sasa hakujiuzuru wakati huo, hivyo hana sababu ya kuanza kutoa lawama. Anajipendekeza tu na kukumbatia ufisadi.
 
DHAIFU=6
NDUGAI=6


[emoji3578]..... ASSAD
 

Mkuu umemaliza. Sijui uko wapi nikununulie soda duh.

Matokeo ya uhuru wa kila Mtu kuongea anachojisikia na kukiona ndio kama huu sasa wa Ndugai yaani ni aibu kuu kwa taifa kusema kua walifanyiwa presentation ya mradi na kuona uko vizuri bila kusoma mkataba unatakaje ni aibu kubwa kwa Taifa.

Ndio maana hata katika familia zetu ili uendelee kuna mda lazima uzibe masikio otherwise ukisikia la kila mtu hupigi hatuna.

Ila kwa mwendo huu kila Mtu atamkumbuka JPM soon as possible
 
Mh.Ndugai na naibu wake ilitakiwa waachie madaraka kwa kutoishauri serikali vizuri...hilo lilikua la lazima wakina Tundu walipoishauri Serikali walikatwa hadi posho kisa kumfurahisha Mkuu leo anataka kuja upande wetu sio kweli kabisaa...
 
HUYU NDUGAI AJIBU HOJA ZA WATANZANIA KUHUSU HIYO BANDARI ILIYOPO MJI WENYE HISTORIA YA BIASHARA YA UTUMWA

1. JE, MIKATABA ILISHASAINIWA NA KAMA JIBU NI NDIO ILIPITIA MICHAKAYO GANI

2. ANASEMA ALIKUTANA NA WADAU CHINA WAKAMBRIEF JUU YA HUO MRADI, ILIKUWA NI KWA BAHATI MBAYA AU KWA MIADI?

3.KWA KUWA HUU MRADI UNA MASLAHI MAPANA YA TAIFA, ANAWEZA HATA KWA KIFUPI KUTUELEZEA NAMNA TAIFA LITAKAKAVYONUFAIKA?


4. NI NANI ALIMSHAURI RAIS VIBAYA? KWA UBAYA UPI?

5. KAMA MRADI UNA MASLAHI MAPANA KWA TAIFA NA YEYE ALILIJUA HILO NA KUAMUA KULINYAMAZIA HAONI NI MUDA MUAFAKA WA KUKIRI KWAMBA TAASISI ANAYOIONGOZA NI DHAIFU?

KAMA NDUGAI ULITAFUTA KIKI TUNAANZA NA WEWE
 
HIVI MWENYEWE YULE ALIKUWA ANASHAURIKA? NAKUMBUKA ALIKWAMBIA WAZI KABISA KWAMBA UKIMSHAURI NDIO UMEHARIBU KABISA! AU NASEMA UONGO NDUGU ZANGU?
 
Kumkumbuka ndio hapana haitokuja kutokea kikundi cha wahuni sijui utekaji na maugomvi ya kijinga ya kuchomeana vifaranga yasingeisha huku unakuja kusikia Ndugai kaongeza Kodi kisa mradi wa umeme na report tamu tamu ya CAG ya Atcl kupata faida na kutoa gawio kumbe wanachechemea...
 
Kwa jinsi alivyo kuwa huyo mungu mtu wenu unadhani angeanzia wapi kumshauri wakayi yeye anajua kila kitu yaani, walio taka kumshauri aliwambia wanawashwa washwa awamu zao zilisha pita wamuache,

Na ukijifanya unazidi kumshauri kesho tutasikio umeokotwa ununio aisee huyu bwana ashukuriwe mungu kwa kumchukua kaondoa adha kubwa sana tanzania na mipango yake ya kutaka kubaki madarakani
 
Ndugai ni kichaa tu. Hata Magufuli kalisema kwenye hii clip
Kwa jinsi alivyo kuwa huyo mungu mtu wenu unadhani angeanzia wapi kumshauri wakayi yeye anajua kila kitu yaani, walio taka kumshauri aliwambia wanawashwa washwa awamu zao zilisha pita wamuache,

Na ukijifanya unazidi kumshauri kesho tutasikio umeokotwa ununio aisee huyu bwana ashukuriwe mungu kwa kumchukua kaondoa adha kubwa sana tanzania na mipango yake ya kutaka kubaki madarakani
 
Wachina wamempima korona kwa kile kipimo chao kipya kafuraaahi anataka aje atufanye wajinga akipendezwa yeye mradi uendelee? Waweke wazi mkataba na hiyo presentation na sisi tuione
eti kwa vile wao ni wabunge anadhani ndio wana akiili kubwa kuliko watz wengine, kumbe kiuhalisi ni kinyume chake!.
 
Katiba yetu inahitaji kurekebeshwa kulifanya bunge kuwa huru. Ndugai anaweza kuondolewa kuwa spika kwa kuondolewa uanachama na mwenyekiti wake wa chama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…