Ndugai amefuata utaratibu wa kujiuzulu Uspika kwa mujibu wa Katiba. Mbatia hayupo sahihi na kesi yake haina mashiko

Mkuu una hoja tena hoja mujarab kabisa ila kidogo imetoka nje ya mada. Hoja ya msingi kwenye mnakasha huu as per mleta mada ni; "Je, Bunge limepata taarifa ya kujiuzulu kwa Spika au halijapata?". According to mleta mada ni kwamba Katiba inaeleza tu Bunge lipewe taarifa ila kwa utaratibu upi, Katiba iko kimya.

Sasa kuna hoja mbili tu za kujibu ku-prove wrong kwamba "Spika hajajizulu"; mosi, Bunge halijapata taarifa; na/au pili, Bunge limepata taarifa ila utaratibu haukuwa sahihi. Tujikite kwenye hoja mbil hizo.
 
Kwamba Bunge ndo' lilipelekewa copy, ila 'orijino' alipewa katibu mkuu wa CCM[emoji848]
... sidhani kama kuna tatizo kwa sababu unapoletewa copy ni kwa ajili ya nini? "KWA TAARIFA"; so Bunge lina taarifa.
 
Mbatia anatembelea matukio kutafuta kiki,
Katiba imekanyagwa mara nyingi sana huko nyuma,hakuwahi kujitokeza kufungua kesi,
Leo hii ameona Nini?
Kipi ni Bora , kuendelea katika makosa au kuanzia upya bila makosa , au mtu akikosea njia huko nyuma hatakiwi kurudi kwenye njia sahihi , Bali aendelee katika makosa ? Hakuna mtu sahihi duniani kote, hata mbinguni wapo wa kuhesabu
 
Toa taarifa na si nakala ya taarifa, sijui unatumia kiswahili cha wapi!
 
Kipi ni Bora , kuendelea katika makosa au kuanzia upya bila makosa , au mtu akikosea njia huko nyuma hatakiwi kurudi kwenye njia sahihi , Bali aendelee katika makosa ? Hakuna mtu sahihi duniani kote, hata mbinguni wapo wa kuhesabu
Sorry uliwahi kuishi Mbinguni?
 
Mbatia anatembelea matukio kutafuta kiki,
Katiba imekanyagwa mara nyingi sana huko nyuma,hakuwahi kujitokeza kufungua kesi,
Leo hii ameona Nini?
Ni kweli kabisa.Ndugai amenajisi katiba kwa kuwakumbatia wabunge 19 walio jichagua bila ridhaa ya chama Chao.Mbatia atuambie kama taratibu zimefuatwa,kama Sheria, kanuni na taratibu hazikufuatwa, nadhani hapa ndiyo angeshitaki kwa kutofuata Sheria.Kinyume Cha hapo ni usanii tu.
 
Asante Sana Mkuu. Umefunga kazi
 
Watu wanasema lile sio bunge la CCM ni bunge la wananchi sasa kwanini Ndugai amwandikie Chongolo.


Umeelewa au bado?
Alimwandikia Chongolo lakini pia alimpa nakala katibu wa bunge, kwanini? Kwasababu alitaka pia katibu wa bunge ajue.
 
Kikubwa ni Bunge kupata taarifa ya kujiuzulu kwake.

Suala la kukitaarifu chama kilichomdhamini ni hiyari yake na wala siyo kosa na haiathiri ukweli kuwa bunge limepewa taarifa ya kujiuzulu kwa spika na bunge lenyewe limekiri
Soma vizuri hiyo ibara ya 149 kifungu kifungu kidogo cha kwanza tangu mwanzo kisha soma hiuo 1(c) na uunganishe. Msharti yaliyoainishwa ya kujiuzulu kwanza ni kuandika barua ya kujiuzulu na kuitilia saini kwa mkono wake, kisha kuipeleka hiyo taarifa / barua kwa bunge. Maana yake ni kuliandikia bunge (barua zote zinazoelekea bungeni huandikwa kwa katibu wa bunge), na si vinginevyo!!
Ndiyo maana pamoja na kupokea nakala ya barua hiyo, katibu wa bunge hawezi kuanzisha mchakato wa kupata spika wa bunge!! Katibu mkuu wa ccm hana mamlaka ya kupokea barua ya kujiuzulu ya spika!! Spika angekuwa amejiuzulu uanachama wa ccm hapo ndipo angepaswa kumwandikia katibu mkuu wa ccm!!
Wala katibu mkuu wa ccm hana mamlaka ya kikatiba kumwandikia katibu wa bunge akimtaarifu juu ya kujiuzulu kwa spika maana barua hiyo lazima iwe na saini ya spika KWA MKONO WAKE!!
Wasipolizingatia hili unaweza kuzuka MGOGORO MKUBWA WA KIKATIBA, iko hivi: Kama wakipuuza utarstibu huu wa kikatiba kama inavyoelekea kutokea, katibu mkuu wa ccm atamwandikia barua katibu wa bunge akimtaarifu kuwa Ndugai kajiuzulu, na katibu wa bunge akaikubali taarifa hiyo na kuanzisha mchakato wa kuchagua spika mpya, KIKATIBA MCHAKATO HUO NI BATILI, NA SPIKA ATAKAYECHAGULIWA NI BATILI, NA VIKAO VYOTE VYA BUNGE NA KAMATI VITAKAVYOKAA CHINI YA SPIKA BATILI. I BATILI PIA, NA MAAMUZI YOTE YATAKAYOFIKIWA CHINI YA SPIKA BATILI NI BATILI PIA!! Mgogoro wa kikatiba utaanzia mtu atakapogoma kutekeleza maamuzi au wito wa spika kwa madai kuwa hayatambui maamuzi ya bunge maana nj BATILI na hautambui wito wa spika maana naye ni SPIKA BATILI!! Mwisho wa siku ngoma ITATUA MAHAKAMA KUU, kwa maana mtu huyo atashitakiwa!! Huko mahakamani atatoa sababu kwa nini maamuzi hayo ni batili!! Kuna uwezekano mtu huyo wataogopa kumshitaki ili kuepusha MGOGORO, lakini watu watajua na maamuzi ya bunge yatapuuzwa na watu wengi mwisho wa siku mgogoro utafika mahakamani tu!! Huko mahakamani ITATAMKWA RASMI SPIKA NDUGAI BADO NI SPIKA HALALI MAANA BADO HAJAMWANDIKIA KATIBU WA BUNGE KIHUSU KUJIUZULU KWAKE NA IKAO VYOTE VYA BUNGE VILIVYOKAA CHINI YA SPIKA BATILI NI BATILI PIA!!!! Ifanyike jitihada ya kuepusha mgogoro huo mkubwa wà kikatiba!! Soma tena ibara hiyo ya katiba kwenye post #1.
 
Mbatia anatembelea matukio kutafuta kiki,
Katiba imekanyagwa mara nyingi sana huko nyuma,hakuwahi kujitokeza kufungua kesi,
Leo hii ameona Nini?
Anachekesha na anasikitisha.
 
Tukisema vyuo vya Tanzania vinatoa Premature mnakasirika. Kwa akili yako Ndugai angeweza kupiga Simu tu ikawa taarifa?
Punguza hasira. Spika ametoa taarifa katika bunge na bunge limekiri kupewa taarifa hiyo; hivyo spika amezingatia matakwa ya kisheria ktk kujiuzulu

Nakutakia makasiriko mema
 
149(1)(c) Mimi nimeelewa kwamba taarifa ya kujiuzulu inatokewa iwasilishwe bungeni, yaani kwenye mkutano/kikao cha Bunge
Kwa hiyo asubiri hadi kikao ndipo ajiuzulu? We uliona wapi?

Kwenye bunge tafsiri yake ni bunge kupewa taarifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…