Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu una hoja tena hoja mujarab kabisa ila kidogo imetoka nje ya mada. Hoja ya msingi kwenye mnakasha huu as per mleta mada ni; "Je, Bunge limepata taarifa ya kujiuzulu kwa Spika au halijapata?". According to mleta mada ni kwamba Katiba inaeleza tu Bunge lipewe taarifa ila kwa utaratibu upi, Katiba iko kimya.Nafasi ya U spika inahudumia Watanzania regardless tofauti zetu za kiitikadi,means hawezi akawa anawajibika katika system's za kichama ,speaker alitakiwa awasiliane na Bunge sio political party ndio maana halipwi na political party,tatizo ni KATIBA na mbaya zaidi ccm wamejimilikisha nchi yetu,yaani wanaiona ni sehemu ya Lumumba na wengineo wote ni wakimbizi,Tanzania it belongs to all of us na wote tunawajibika kwa ustawi wake.
... sidhani kama kuna tatizo kwa sababu unapoletewa copy ni kwa ajili ya nini? "KWA TAARIFA"; so Bunge lina taarifa.Kwamba Bunge ndo' lilipelekewa copy, ila 'orijino' alipewa katibu mkuu wa CCM[emoji848]
Kachemka tuseme tu ukweli badala ya ushabiki usio na maana; Bunge lipelekewa copy for what? "KWA TAARIFA"; so, lina taarifa na ndivyo utaratibu unavyotaka.Mbatia kapaniki.
Kipi ni Bora , kuendelea katika makosa au kuanzia upya bila makosa , au mtu akikosea njia huko nyuma hatakiwi kurudi kwenye njia sahihi , Bali aendelee katika makosa ? Hakuna mtu sahihi duniani kote, hata mbinguni wapo wa kuhesabuMbatia anatembelea matukio kutafuta kiki,
Katiba imekanyagwa mara nyingi sana huko nyuma,hakuwahi kujitokeza kufungua kesi,
Leo hii ameona Nini?
Toa taarifa na si nakala ya taarifa, sijui unatumia kiswahili cha wapi!Kumekuwa na mjadala kutoka baadhi ya watu mbalimbali mtandaoni juu ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Spika Mh Job Ndugai.
Ulianza mjadala kwamba kwanini ktk barua yake ameandika herufi kubwa pekee? KIMSINGI kilichosambaa mtandaoni siyo barua bali ni TAARIFA KATIKA VYOMBO VYA HABARI ambayo ni sawasawa tu na TANGAZO. Katika uandishi TANGAZO/TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NI KAWAIDA SANA KUANDIKWA KWA HERUFI KUBWA PEKEE. Barua za kujiuzulu zimewasilishwa katika bunge na katika Chama cha Mapinduzi.
Jambo la Pili nimeona Ndg James Mbatia amesema anakusudia kupeleka kesi mahakamani kupinga utaratibu uliotumika ktk kujiuzulu kwa spika. Kwamba kwa maelezo ya Mbatia ni kiwa Spika alitakiwa aende bungeni kujiuzulu kupitia ktk kamati ya bunge na bunge lenyewe.
Kimsingi hoja yake siyo sahihi. Kwa maoni yangu Mh Spika amefuata utaratibu wa kikatiba na ametimiza matakwa ya kisheria katika mchakato wa kujiuzulu.
Ukisoma katiba ya JMT sura ya 11 ibara ya 149(1)(c) imeeleza wazi kuwa endapo Spika au Naibu spika anataka kujiuzulu anatakiwa kuwasilisha taarifa hiyo katika bunge. Katiba haijatoa masharti kuwa taarifa hiyo iwe ktk mkutano, kamati au kwa barua original au nakala ya barua? Katiba imetaka tu kuwa Spika atoe taarifa katika Bunge.
Mh Spika Job Ndugai katika kujiuzulu ametoa taarifa katika bunge na chama cha mapinduzi na kwamba KWA KUWA BUNGE LIMEKIRI KUPOKEA TAARIFA YA KUJIUZULU KWA SPIKA (KAMA TAARIFA YA KATIBU WA BUNGE INAVYOJIELEZA) Basi tuhitimishe kwa kusema Spika amewasilisha taarifa yake ktk bunge na amefuata taratibu za kisheria za kujiuzulu kwa spika.
Kwa lugha rahisi Spika amejiuzulu kisheria na uchaguzi wa Spika mwingine utafanyika mwezi Februari kama ilivyotangazwa na BUNGE katika taarifa yake ya vyombo vya Habari.
View attachment 2072949
Sorry uliwahi kuishi Mbinguni?Kipi ni Bora , kuendelea katika makosa au kuanzia upya bila makosa , au mtu akikosea njia huko nyuma hatakiwi kurudi kwenye njia sahihi , Bali aendelee katika makosa ? Hakuna mtu sahihi duniani kote, hata mbinguni wapo wa kuhesabu
Ni kweli kabisa.Ndugai amenajisi katiba kwa kuwakumbatia wabunge 19 walio jichagua bila ridhaa ya chama Chao.Mbatia atuambie kama taratibu zimefuatwa,kama Sheria, kanuni na taratibu hazikufuatwa, nadhani hapa ndiyo angeshitaki kwa kutofuata Sheria.Kinyume Cha hapo ni usanii tu.Mbatia anatembelea matukio kutafuta kiki,
Katiba imekanyagwa mara nyingi sana huko nyuma,hakuwahi kujitokeza kufungua kesi,
Leo hii ameona Nini?
Asante Sana Mkuu. Umefunga kaziYawezekana unajua kusoma na kuandika vizuri ila umekosa analytical thinking.
Kwa fikra zako, na kwa uelewa tu wa kawaida, hivi tuseme umeajiriwa na kampuni fulani, kabla ya kuajiriwa ulidhaminiwa na Baba yako, unaweza kujiuzulu kazi kwa kumwandikia barua baba yako, na anakala ukampelrkra mwajiri wako?
Katiba ipo wazi, spika akitaka kujiuzulu anapeleka taarifa Bungeni, huko kwenye chama chake, hakuna mahali popote katiba imetamka. Unaacha kitu kilichotamkwa kikatiba, unaenda kufanya upuuzi halafu unasema katiba imefuatwa!
Alimwandikia Chongolo lakini pia alimpa nakala katibu wa bunge, kwanini? Kwasababu alitaka pia katibu wa bunge ajue.Watu wanasema lile sio bunge la CCM ni bunge la wananchi sasa kwanini Ndugai amwandikie Chongolo.
Umeelewa au bado?
Soma vizuri hiyo ibara ya 149 kifungu kifungu kidogo cha kwanza tangu mwanzo kisha soma hiuo 1(c) na uunganishe. Msharti yaliyoainishwa ya kujiuzulu kwanza ni kuandika barua ya kujiuzulu na kuitilia saini kwa mkono wake, kisha kuipeleka hiyo taarifa / barua kwa bunge. Maana yake ni kuliandikia bunge (barua zote zinazoelekea bungeni huandikwa kwa katibu wa bunge), na si vinginevyo!!Kikubwa ni Bunge kupata taarifa ya kujiuzulu kwake.
Suala la kukitaarifu chama kilichomdhamini ni hiyari yake na wala siyo kosa na haiathiri ukweli kuwa bunge limepewa taarifa ya kujiuzulu kwa spika na bunge lenyewe limekiri
Anachekesha na anasikitisha.Mbatia anatembelea matukio kutafuta kiki,
Katiba imekanyagwa mara nyingi sana huko nyuma,hakuwahi kujitokeza kufungua kesi,
Leo hii ameona Nini?
Punguza hasira. Spika ametoa taarifa katika bunge na bunge limekiri kupewa taarifa hiyo; hivyo spika amezingatia matakwa ya kisheria ktk kujiuzuluTukisema vyuo vya Tanzania vinatoa Premature mnakasirika. Kwa akili yako Ndugai angeweza kupiga Simu tu ikawa taarifa?
Kwa hiyo asubiri hadi kikao ndipo ajiuzulu? We uliona wapi?149(1)(c) Mimi nimeelewa kwamba taarifa ya kujiuzulu inatokewa iwasilishwe bungeni, yaani kwenye mkutano/kikao cha Bunge
Wewe ndiye umekurupuka.
Soma barua ya Ndugai kwanza.rua
Ungeongea kiswahili tu bado tungekuelewa