Ndugai asisahau, kadi yake ya CCM ndio inampa uspika, CCM wanaweza kuiondoa muda wowote na akawa raia wa kawaida tu

Ndugai asisahau, kadi yake ya CCM ndio inampa uspika, CCM wanaweza kuiondoa muda wowote na akawa raia wa kawaida tu

Ule ushauri wake ndio unawafanya muanze kuona anyang'anywe kadi?
Hivi hii nchi akili tumezipeleka wapi?
Mbona hatuna uwezo wa tafakuri?
Kwanini tusitafakari ushauri wake?
Kwanini kila kauli itolewayo ionekane ni hujuma?
Kwani hata huyo Rais kinachompa sio kadi ya CCM?
Au Katibu Mkuu wa CCM, kinachompa cheo sio kadi?
Yaani hatutaki kupewa ushauri wa tahadhari juu ya mikopo?
Kwani nchi ngapi maskini zimeshazidiwa na mikopo?
Tunaangalia motive,, yale matamshi yalikua na ulterior motive nyuma yake[emoji2955]

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
84.(7) Spika atakoma kuwa spika na ataacha kiti cha spika litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:-
a) iwapo mtu huyo alichaguliwa kutoka miongoni mwa wabunge, basi ikiwa atakoma kuwa mbunge kwasababu yoyote ambayo haihusiki na kuvunjwa bunge.

Ndugai akiondolewa uanachama wa ccm anakosa sifa ya kuwa mbunge and therefore hawi sifa ya kuwa spika kwasabau amechaguliwa miongoni mwa wabunge...

Umeelewa sasa nilichokuwa namaanisha, maana watu wengine mpaka muandikiwe kwa kirefu.
Yaani wewe ndo umesolve equation,, case closed [emoji28][emoji28]

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Nani atamruhusu , hivi wewe unaijua nguvu ya Rais.. Huyo speaker wako si anapigwa House Arrest anachaguliwa mwingine maisha yanaendelea.. watakwambia kwa ajili ya maslahi ya Taifa. Utasema nini?

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Wamesahau kilichomtokea Aboud Jumbe,,,, [emoji134][emoji134]

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Kama wana ubavu Ccm wamvue ubunge spika, tatizo vichawa ndio vinapiga kelele, lkn chama kama chama wala hakijajitokeza chini ya msemaji wake kuongea lolote, zaidi zaidi mama kamjibu spika kama rais tu na sio kwa kofia ya uenyekiti wa chama. Bunge ni mhimili unaojitegemea ndio maana hata Magu aliweka mahusiano mazuri na mkuu wa mhimili huo, hiyo CCM ikianza kushindana na Spika ujue pia itakuwa inashindana na wabungu wanaomuunga mkono spika, sasa sidhani kama CCM ipo tayari kuwafuta uanachama wabunge wake, kwahyo msimchukulie poa poa Ndugai
 
Ndungai ataendelea kuwa spika Hata bila chama kama wale wabunge wa Covid 19😲
 
Ibara ya 84(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema:

Kutakuwa na Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na Wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni Wabunge au wenye sifa za kuwa Wabunge; atakuwa ndiye kiongozi wa Bunge na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje ya Bunge.

Je, mna maswali zaidi?! Naweka mkazo: mtu halazimiki kuwa mbunge ili kuwa spika wa bunge! Anayelazimika kuwa mbunge ni Naibu Spika!
Spika anaweza asiwe mbunge ila AWE NA SIFA ZA KUA MBUNGE,
Mojawapo ya sifa za kuwa mbunge, LAZIMA UWE MWANACHAMA WA CHAMA CHA SIASA,, [emoji16][emoji16]
hujaelewa bado?

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Ninyi haya mmeyajua leo kuwa kuna mawazo mbadala, mbona upinzani wakitoa mawazo mbadala zengwe linakuwa kubwa sanaa
Mi nadhani tatizo la upinzani ni kulazimisha mawazo yao, yawe ndo sahihi,, wakati democracy inataka pande mbili zenye mawazo tofauti, lazima kura ihusike, mawazo yatayopita kwa kura, haijalishi yawe mazuri au mabaya , maadamu yamepita upande mwingine hauna budi kuwa wapole,, hiyo inafanyika dunia nzima kuliko na demokrasia,
Huwezi ukashindwa kupitisha agenda yako kidemokrasia bado ukawa una PUSH AGENDA KWA LAZIMA, hiyo sasa siyo siasa ni FUJO. [emoji1745]

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Ule ushauri wake ndio unawafanya muanze kuona anyang'anywe kadi?
Hivi hii nchi akili tumezipeleka wapi?
Mbona hatuna uwezo wa tafakuri?
Kwanini tusitafakari ushauri wake?
Kwanini kila kauli itolewayo ionekane ni hujuma?
Kwani hata huyo Rais kinachompa sio kadi ya CCM?
Au Katibu Mkuu wa CCM, kinachompa cheo sio kadi?
Yaani hatutaki kupewa ushauri wa tahadhari juu ya mikopo?
Kwani nchi ngapi maskini zimeshazidiwa na mikopo?
Kwanini hakushauri haya kipindi cha awamu ya 5?
 
Spika ni lazima awe Mwanachama wa Chama cha Siasa ila si lazima awe Mbunge
Sio kweli. Speaker sio lazima awe mwanachama. Mtu yeyote mwenye sifa ya kuwa mbunge anaweza kuwa speaker. Sasa mbunge sio lazima awe mwanachama. Mtu yeyote anaweza kuwa mbunge, either kupitia chama au kuteuliwa
 
Spika anaweza asiwe mbunge ila AWE NA SIFA ZA KUA MBUNGE,
Mojawapo ya sifa za kuwa mbunge, LAZIMA UWE MWANACHAMA WA CHAMA CHA SIASA,, [emoji16][emoji16]
hujaelewa bado?

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Sio lazima, sifa za kuwa mbunge ni panoja hujawahi kutiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi sita kwa mfano. Hakuna mahali popote kuwa lazima uwe member wa chama cha siasa.
 
Kudhaminiwa na chama sio hoja, hoja ni matakwa ya mtu kuwa spika!! Kudhaminiwa na chama ndo hiyo backup ninayoisema lakini unaweza kugombea uspika hata kama huna chama!!
Aligombea uspika kama mgombea asiye na chama ama mgombea kupitia chama fulani?

Mbona sheria iko wazi kwamba kama aligombea kupitia chama basi uanachama wake ukikoma basi mamlaka aliyonayo nayo yanakoma kama yalipatikana kupitia udhamini wa chama cha siasa.
 
Back
Top Bottom