#COVID19 Ndugai: Chanjo ni hiyari ila hauna hiyari kuambukiza wenzako

#COVID19 Ndugai: Chanjo ni hiyari ila hauna hiyari kuambukiza wenzako

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Wakati kukiwa na mjadala wa baadhi ya wabunge kuhusu chanjo ya corona inayoendelea kutolewa nchini, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema pamoja na chanjo kuwa hiari, haimfanyi mtu kuwa na hiari ya kuambukiza wengine.

Kauli hiyo imekuja kukiwa tayari kuna wabunge walioonyesha wazi kupingana na mpango huo wa chanjo wakieleza kuhofia usalama wake kwa afya ya anayechanjwa.

Hata hivyo, juzi katika mahojiano yake na BBC, Rais Samia Suluhu Hassan aliendelea kuwahakikishia Watanzania kuwa chanjo hiyo ni salama, kinyume na hapo yeye asingehatarisha maisha yake kwa kuwa wa kwanza kuchanjwa

“Nashukuru sasa hivi Watanzania wengi wameelewa na wanaulizia chanjo, nalazimika kutuma maombi kwa nchi wahisani wanaosaidia chanjo waiangalie Tanzania wakati na sisi tukiendelea na mpango wa kununua chanjo kupitia nchi za Umoja wa Afrika (AU),” alisema Rais.

Pamoja na kauli hiyo ya Samia na uthibitisho wa wataalamu wa nchini na kimataifa, baadhi ya watu, wakiwemo wabunge kadhaa, wanaeleza waziwazi wasiwasi wao dhidi ya chanjo hiyo.

Akinukuliwa na kituo kimoja cha runinga, Spika Ndugai ambaye amekwishachanja, alisema, “tuna mabanda tayari yameshajengwa, wapo wataalamu na chanjo za kutosha zipo, kwa hiyo kila atakayekuja kwenye Bunge lijalo…(hakumalizia).

Aliongeza, “Ni hiari. “Ni hiari” alisema huku akionyesha ishara ya alama za funga usemi kwa vidole.

Kisha, Ndugai akasema, “...lakini hiari hii haikufanyi uwe na hiari ya kuchukua risk ya kuambukiza wengine.”

Mwananchi lilimtafuta Spika Ndugai jana ili aeleze alichokuwa anamaanisha, ambapo alifafanua zaidi kuwa vikao vya Bunge lijalo litakaloketi Agosti 30, ofisi yake itatoa mwelekeo huku akiwasisitiza wabunge wote kuchanja.

“Kuanzia Jumatatu (Agosti 16), wabunge wote watakuwepo (Dodoma) na uchanjaji utakuwa mkubwa. Tunaanza kwa kuhakikisha huduma zinakuwepo maana hata ukisema unachukua hatua, lazima huduma zipatikane, wenyewe ndiyo washindwe kwenda kuzipata. Natoa wito kwa wabunge wote kuchanja,” alisema Ndugai.

Miongoni mwa wabunge walioonyesha msimamo dhidi ya chanjo hiyo ni pamoja na aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, ambaye kwa sasa ni mbunge wa Kuteuliwa, Humprey Polepole.

“Ni muhimu sana watu wetu wakumbushwe tena na tena namna ya kujenga kinga ya mwili, ikiwemo elimu ya chakula na lishe bora kama hatua ya msingi ya kukabiliana na magonjwa na maambukizo yanayoweza kuzuiwa na kinga imara ya mwili. Kuchanja ni hiari lakini si kila kitu, mimi nitaimarisha kinga ya mwili na chanjo kwangu hapana,” aliandika Polepole kwenye ukurasa wake wa Instagram na kupongezwa na baadhi wafuasi wake, huku wengine wakimshukia.

Naye mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima mara kadhaa ametamka hadharani kuwa hatachanjwa chanjo hiyo kwa kuwa hana uhakika na usalama wake.

“Chanjo ni hiari anayependa aende, ila hapa hachanjwi mtu, lazima kondoo wangu niwalinde kwa namna yoyote ile, siko tayari kondoo wangu hata mmoja aangamie. Wajibu wa kulinda afya yako ni wako, huwezi kuwekewa kitu mwilini bila kutaka. Sichanjwi na sitachanjwa,” alisema Gwajima, ambaye ni askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.

Mbunge huyo, kinyume na kauli za kitaalamu, alisisitiza kuwa hadi sasa hakuna tafiti za kutosha zilizofanywa na wataalamu wa ndani kuhusu chanjo hiyo inayotolewa nchini na kuwataka wataalamu kuweka wazi kemikali zilizomo kwenye chanjo hiyo.

Matamshi hayo yamemwibua Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka akisema msimamo wa chama hicho unaweka wazi kuwa chanjo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani yao kwenye kipengele cha utoaji wa huduma za afya kwa Watanzania.

“Kwa hiyo sisi ukituuliza CCM msimamo wetu, tunasimama na Rais kwamba lazima tuwakinge Watanzania dhidi ya maradhi ya mlipuko, ikiwemo Uviko-19... tuna kanuni ya maadili, hii inawamulika viongozi wote ambao mienendo yao haiendi vizuri, ikionekana kuna mtu amekiuka kanuni, misingi ya chama ipo na haibagui, hatua zinaweza kuchukuliwa kwa yeyote,” alisema Shaka.
 
Kwa lugha nyepesi ni kwamba Job analazimisha wabunge wachanje. Na kama patatokea Mbunge ambae hajachanja, basi Mbunge huyo hato ruhusiwa kushiriki ndani ya mbunge kwa kisingizio cha atawaambikiza wengine.
Anyway..... Wakubwa tumemuelewa vyema Mh 🔉 Job
 
Kwa lugha nyepesi ni kwamba Job analazimisha wabunge wachanje. Na kama patatokea Mbunge ambae hajachanja, basi Mbunge huyo hato ruhusiwa kushiriki ndani ya mbunge kwa kisingizio cha atawaambikiza wengine.
Anyway..... Wakubwa tumemuelewa vyema Mh 🔉
Kenyan civil servants have until late August to get vaccinated against Covid-19 or risk disciplinary action, according to a government document made public this week.

The order comes as parliament is due to consider a motion to bar unvaccinated people or those without negative Covid certificates from certain public and private spaces.

Kenya is witnessing a surge in coronavirus cases but the vaccine rollout remains slow, with less than three percent of the 47 million population having had shots.


"Some public servants have deliberately avoided getting vaccinated so that they can stay away from work under the guise of working from home," public service head Joseph Kinyua said in a memo to government ministries.

"This is against a background of access to vaccines having greatly improved."

He said there had been a low uptake of vaccines among public servants particularly in the security sector, teachers and core civil service workers -- designated as essential workers by the government.

Those who have not had a first jab by August 23 will be "treated as discipline cases and appropriate action taken against them", Kinyua said, without elaborating on what the penalties may be.

The country aims to have inoculated at least 26 million people by the end of next year.

MPs are also due to debate on Thursday a motion to deny people access to private and public spaces if they are not fully vaccinated or do not possess a negative Covid-19 certificate.

It was not immediately clear where the proposed restrictions would apply.

At the end of last month the government extended until further notice a nighttime curfew across the country and banned public gatherings, warning that hospitals were becoming overwhelmed.

In total the East African country has registered more than 213,000 coronavirus infections of which 4,211 have been fatal, and recently the daily caseload has often topped 1,000.

Weekly positivity rates have risen from averages of seven percent in early June to nearly 15 percent now.
 
Wakuu soon tamko la katibu wa bunge kwenda kwa wabunge wote wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwa lazima wachanjwe la sivyo hawataruhusiwa kuingia bungeni mwezi ujao.

Wabunge watatakiwa kuwasilisha kadi za chanjo kwa walinzi ili kuruhusiwa kuingia bungeni.

Wabunge wanatakiwa kuwa mifano ya jamii na chama Cha mapinduzi na kumuunga mkono mh. Rais ambaye tayari amesha chanjwa.

MY TAKE. Msimamamo wa Gwajima na poleople utaonekana hasa wakigoma kuingia bungeni

USSR
 
Wachague posho au misimamo, mtego mchungu kweli, ukiacha kuchanjwa na ukaacha posho bado chama kitakushughulikia kwa nini unaenda kinyume na maazimio ya chama.

Hapo ni lazima wote wachanje ili wawe na hivyo vyeti.
 
Kwani bakora boy naye ameshajitokeza kupata chanjo? Mbona yamewekwa masharti magumu hivyo, ilhali wapinga chanjo na uviko wamejaamo.
 
Back
Top Bottom