#COVID19 Ndugai: Chanjo ni hiyari ila hauna hiyari kuambukiza wenzako

#COVID19 Ndugai: Chanjo ni hiyari ila hauna hiyari kuambukiza wenzako

Wakuu soon tamko la katibu wa bunge kwenda kwa wabunge wote wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwa lazima wachanjwe la sivyo hawataruhusiwa kuingia bungeni mwenzi ujao .

Wabunge watatakiwa kuwasilisha kadi za chanjo kwa walinzi ili kuruhusiwa kuingia bungeni.

Wabunge wanatakiwa kuwa mifano ya jamii na chama Cha mapinduzi na kumuunga mkono mh. Rais ambaye tayari amesha chanjwa.

MY TAKE. Msimamamo wa gwajiboy na poleople utaonekana hasa wakigoma kuingia bungeni

USS

Nchi hii imelaaniwa

Wenzetu waliozitengeneza hizo chanjo hawalazimishani Bali wananchi wao wanaelimishwa na wanakubali kwa hiari yao

Sasa ukija kwa hawa viongozi wetu mbumbumbu hawajui chochote kuhusu Uhuru wa mtu na faragha yya
Halafu wanawatishia hawa jamaa vichwa ngumu.
Hili ndiyo anguko la rais linaanzia hapa.

Hawa jamaa wamejibanza kwenye hoja za Mwendazake kuhusiana na chanjo.Wananchi wengi ndo wanasimamia hicho.Kuwatimua Bungeni kisa chanjo ndo watatengeneza upinzani ambao haujapata kutokea.
 
Umejuaje kama hawajachanjwa? Wewe unawaamini wanasiasa hawa wa Tanzania? Ambao juzi walisema tusali halafu wakaja tujifukize na leo wanasema tuchanje na kesho hatujui watasema nini

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Halafu wanawatishia hawa jamaa vichwa ngumu.
Hili ndiyo anguko la rais linaanzia hapa.

Hawa jamaa wamejibanza kwenye hoja za Mwendazake kuhusiana na chanjo.Wananchi wengi ndo wanasimamia hicho.Kuwatimua Bungeni kisa chanjo ndo watatengeneza upinzani ambao haujapata kutokea.
Wabunge wengi Tena naweza sema wote watachanja.Hakuna upinzani wowote utatokea kwa kuzuia chanjo
 
Wakuu soon tamko la katibu wa bunge kwenda kwa wabunge wote wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwa lazima wachanjwe la sivyo hawataruhusiwa kuingia bungeni mwezi ujao.

Wabunge watatakiwa kuwasilisha kadi za chanjo kwa walinzi ili kuruhusiwa kuingia bungeni.

Wabunge wanatakiwa kuwa mifano ya jamii na chama Cha mapinduzi na kumuunga mkono mh. Rais ambaye tayari amesha chanjwa.

MY TAKE. Msimamamo wa Gwajima na poleople utaonekana hasa wakigoma kuingia bungeni

USSR
Unajuwa kwamba ww ni popomarism?
 
Ila Gwaji akiacha ubunge kupinga chanjo graph yake itapanda mara 100000

Kanjanja yule tapeli hawezi, nakuhakikishia sasa hivi utasikia wote wameunga mkono na wamechanja. Wanasiasa karibu wote ni wanafiki tu, haswa wakiona maslahi yao yanaguswa ndio utaujua unafiki wao.
 
Mabunge yote yanayofuata taratibu za Westminster wabunge wake lazima wachanjwe ,acha mbumbavu wako hapa

USSR
Kudadadeq walahi mafisiem mnaparurana
IMG-20191216-WA0001.jpg
 
Halafu wanawatishia hawa jamaa vichwa ngumu.
Hili ndiyo anguko la rais linaanzia hapa.

Hawa jamaa wamejibanza kwenye hoja za Mwendazake kuhusiana na chanjo.Wananchi wengi ndo wanasimamia hicho.Kuwatimua Bungeni kisa chanjo ndo watatengeneza upinzani ambao haujapata kutokea.
Katika kitu mwanasiasa mbunge ambaye tayari Ni mbunge hapendi Ni kurudi katika uchaguzi
 
Wakuu soon tamko la katibu wa bunge kwenda kwa wabunge wote wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwa lazima wachanjwe la sivyo hawataruhusiwa kuingia bungeni mwezi ujao.

Wabunge watatakiwa kuwasilisha kadi za chanjo kwa walinzi ili kuruhusiwa kuingia bungeni.

Wabunge wanatakiwa kuwa mifano ya jamii na chama Cha mapinduzi na kumuunga mkono mh. Rais ambaye tayari amesha chanjwa.

MY TAKE. Msimamamo wa Gwajima na poleople utaonekana hasa wakigoma kuingia bungeni

USSR
Jamani lazima tuelewe.Kuchanja ni hiari.Kama ingekuwa lazima andiko lako lingekuwa na thamani.Lakini ni hiari.
 
Hii niliandika kwenye post moja juzi iliyokua ikimuhusu kitibu mkuu wa ccm na polepole na gwajima,nikasema itatengenezwa kama sheria asiye na cheti chakudhibitisha amechanjwa aingii bungeni,,kuna mtu alinijibu tofauti sasa ndio hivyo
 
Si vizuri kutisha bunge madhara yake ni makubwa kwa serikali

Ni.kuwa serikali inatishia bunge au wabunge kupitia vikao vyao ndio wameamua hivyo

Mleta mada hii habari uzushi bunge Lina taratibu zake za kikanuni za kuamua wafanye Nini

Katibu wa bunge Hana ubavu was kuliburuza bunge kwenye lolote

Bunge ndio hukaa na kuweka kanuni zake hawapabgiwi na katibu wa bunge, serikali Wala mahakama

Hii chanjo wapiga debe wa Chanjo mwende taratibu Kuna maeneo huwezi tu ku enforce kienyeji hivyo

Katibu wa bunge Ni mtu mdogo Sana kwenye bunge Hana huo ubavu.Ila wabunge wenyewe wakiweka hiyo kuwa kanuni happy sawa

Umeandika kishari na bila kuangalia sheria na kanuni za bunge zinasenaje
Sazani kama ameandika bali nikuwa spika mwenyewe amelizunvumzia juzi au Jana jambo hili
 
Kwani ukichanja unakuwa huwezi kuambukiza? Halafu kwanini waliochanjwa wanawaogopa ambao hawajachanjwa wakati inatakiwa iwe vice versa..
'Wanawaona kuwa ni watu hatari' inabidi uelimishaji ufanyike na wala sio kuwashangaa!
 
Ana matatizo Ndugai ukichwanjwa bado unaweza kuambukiza wengine.
 
Spika wa Bunge la Tanzania amesema kuanzia Agosti 16, 2021 Wabunge watakuwepo Dodoma ambapo wametakiwa kuchanjwa Chanjo ya COVID-19. Katika maelezo yake Spika Ndugai amesema Chanjo ni Hiyari lakini hakuna Hiyari ya kuwaambukiza wenzako.

Kwa kauli hiyo ni dhahiri kuwa kundi la wabunge litachanjwa kwa nguvu vinginevyo hawataweza kushiriki Shughuli za Kibunge. Kauli hii itakuwa mwiba Kwa wale wabunge waliojitikeza hadharani na kuonyesha Msimamo wao kuwa hawakubaliani na chanjo ya covid19 inayotolewa nchini

"Maendeleo hayana vyama"

----
Wakati kukiwa na mjadala wa baadhi ya wabunge kuhusu chanjo ya corona inayoendelea kutolewa nchini, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema pamoja na chanjo kuwa hiari, haimfanyi mtu kuwa na hiari ya kuambukiza wengine.

Kauli hiyo imekuja kukiwa tayari kuna wabunge walioonyesha wazi kupingana na mpango huo wa chanjo wakieleza kuhofia usalama wake kwa afya ya anayechanjwa.

Hata hivyo, juzi katika mahojiano yake na BBC, Rais Samia Suluhu Hassan aliendelea kuwahakikishia Watanzania kuwa chanjo hiyo ni salama, kinyume na hapo yeye asingehatarisha maisha yake kwa kuwa wa kwanza kuchanjwa.

“Nashukuru sasa hivi Watanzania wengi wameelewa na wanaulizia chanjo, nalazimika kutuma maombi kwa nchi wahisani wanaosaidia chanjo waiangalie Tanzania wakati na sisi tukiendelea na mpango wa kununua chanjo kupitia nchi za Umoja wa Afrika (AU),” alisema Rais.

Pamoja na kauli hiyo ya Samia na uthibitisho wa wataalamu wa nchini na kimataifa, baadhi ya watu, wakiwemo wabunge kadhaa, wanaeleza waziwazi wasiwasi wao dhidi ya chanjo hiyo.

Akinukuliwa na kituo kimoja cha runinga, Spika Ndugai ambaye amekwishachanja, alisema, “tuna mabanda tayari yameshajengwa, wapo wataalamu na chanjo za kutosha zipo, kwa hiyo kila atakayekuja kwenye Bunge lijalo…(hakumalizia).

Aliongeza, “Ni hiari. “Ni hiari” alisema huku akionyesha ishara ya alama za funga usemi kwa vidole.

Kisha, Ndugai akasema, “...lakini hiari hii haikufanyi uwe na hiari ya kuchukua risk ya kuambukiza wengine.”

Mwananchi lilimtafuta Spika Ndugai jana ili aeleze alichokuwa anamaanisha, ambapo alifafanua zaidi kuwa vikao vya Bunge lijalo litakaloketi Agosti 30, ofisi yake itatoa mwelekeo huku akiwasisitiza wabunge wote kuchanja.

“Kuanzia Jumatatu (Agosti 16), wabunge wote watakuwepo (Dodoma) na uchanjaji utakuwa mkubwa. Tunaanza kwa kuhakikisha huduma zinakuwepo maana hata ukisema unachukua hatua, lazima huduma zipatikane, wenyewe ndiyo washindwe kwenda kuzipata. Natoa wito kwa wabunge wote kuchanja,” alisema Ndugai.

Miongoni mwa wabunge walioonyesha msimamo dhidi ya chanjo hiyo ni pamoja na aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, ambaye kwa sasa ni mbunge wa Kuteuliwa, Humprey Polepole.

“Ni muhimu sana watu wetu wakumbushwe tena na tena namna ya kujenga kinga ya mwili, ikiwemo elimu ya chakula na lishe bora kama hatua ya msingi ya kukabiliana na magonjwa na maambukizo yanayoweza kuzuiwa na kinga imara ya mwili. Kuchanja ni hiari lakini si kila kitu, mimi nitaimarisha kinga ya mwili na chanjo kwangu hapana,” aliandika Polepole kwenye ukurasa wake wa Instagram na kupongezwa na baadhi wafuasi wake, huku wengine wakimshukia.

Naye mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima mara kadhaa ametamka hadharani kuwa hatachanjwa chanjo hiyo kwa kuwa hana uhakika na usalama wake.

“Chanjo ni hiari anayependa aende, ila hapa hachanjwi mtu, lazima kondoo wangu niwalinde kwa namna yoyote ile, siko tayari kondoo wangu hata mmoja aangamie. Wajibu wa kulinda afya yako ni wako, huwezi kuwekewa kitu mwilini bila kutaka. Sichanjwi na sitachanjwa,” alisema Gwajima, ambaye ni askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.

Mbunge huyo, kinyume na kauli za kitaalamu, alisisitiza kuwa hadi sasa hakuna tafiti za kutosha zilizofanywa na wataalamu wa ndani kuhusu chanjo hiyo inayotolewa nchini na kuwataka wataalamu kuweka wazi kemikali zilizomo kwenye chanjo hiyo.

Matamshi hayo yamemwibua Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka akisema msimamo wa chama hicho unaweka wazi kuwa chanjo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani yao kwenye kipengele cha utoaji wa huduma za afya kwa Watanzania.

“Kwa hiyo sisi ukituuliza CCM msimamo wetu, tunasimama na Rais kwamba lazima tuwakinge Watanzania dhidi ya maradhi ya mlipuko, ikiwemo Uviko-19... tuna kanuni ya maadili, hii inawamulika viongozi wote ambao mienendo yao haiendi vizuri, ikionekana kuna mtu amekiuka kanuni, misingi ya chama ipo na haibagui, hatua zinaweza kuchukuliwa kwa yeyote,” alisema Shaka.

Chanzo: Mwananchi
 
Itakuwa heri kwao wakisimamia misimamo yao yasni;
Gwajima
Polepole pole
Ikiwa watashikilia misimamo yao nitawaheshimu japo sipingi chanjo hata kidogo.
Point yangu ni heri kufa ukitetea unachokiamini kuliko kuishi ukiwa bendera fuata upepo.
 
Back
Top Bottom