Uchaguzi 2020 Ndugai: "Ikulu haiachwi ni “mwiko”, huwezi kuuza ‘mama mkwe’, tuliachiwa na Mwl Nyerere na Karume na chama chetu CCM hatuwezi iachia Ikulu

Chadema husema wakishika madaraka Nchi haitakalika

Wengine tuna ndugu wazee na wagonjwa hatuna pa kuwapeleka Chadema wakianzisha vita
Lini na wapi walisema kuwa wakishika nchi haitakalika?
Nataka ni ushahidi ukiwa na supportive evidence wa kauli unayodai walitoa chadema.
 
"Ikulu haiachwi ni “mwiko”, huwezi kuuza ‘mama mkwe’, tuliachiwa na Mwalimu Nyerere na Abeid Amani Karume na chama chetu @ccm_tanzania hatuwezi waachia watu hawaeleweki" -Job Ndugai View attachment 1568612
Kuna mwenzake Zanzibar alisema hawatoi nchi kwa makaratasi. Sasa hivi amewaachia watoto wake laana tu maana ardhi imeshammeza hizi jeuri na viburi sijui wanadamu wanavipata wapi!.Sote tutalala tuache viburi vya uzima
 
Inaachwa mbona, tuliuza mama yangu kwa jogoo
 
kwani huyu Ndugai na Al Bashir nani mbabe? nani ana maguvu?
 
Hii ni ishara ya kukiri kuwa hawawezi kushinda kupitia sanduku la kura.

Kwa kifupi,wanakiri kushindwa na sasa wanajipanga kutumia dola kubaki madarakani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…