Ndugai: Mataifa ya wenzetu huchukua vijana wenye ufaulu class A+ wana negotiate mikataba sisi tunapeleka maprof wazee waliochoka!

Ndugai: Mataifa ya wenzetu huchukua vijana wenye ufaulu class A+ wana negotiate mikataba sisi tunapeleka maprof wazee waliochoka!

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Katika moja ya comment zilizowahi kunishtua ni hii ya jobu aliyoitoa akiwa spika.

Alidai kwamba wenzetu baadhi ya mataifa linapohusika suala la mikataba, hawana masihara hata kidogo huchukua vijana smart class A wenye uwezo mkubwa wa kusoma kuelewa na kufikiri kwa upana juu ya mikataba tunayoingia kama taifa ni kwa namna gani itanufaisha umma. Akasema kwetu Tanzania hali ni tofauti kabisa kwani sisi huwatumia maprof wetu.

Ni kweli wana elimu nzuri lakini wamechoka kiakili kwa namna ambayo ni rahisi sana kutuingiza chaka. Alisema hii mikataba inaandikwa kijanja sana na ni mabook makubwa makubwa hiyo yanahitaji akili fresh ili kuyasoma kuyaelewa na kufanya maamuzi sahihi.

Mada ya mikataba ya nchi ni nzito sana haikupaswa kabisa kufanyika kizembe.
 
Watu wako serious kufuatilia kesi ya ngono ya binti wa yombo na kudadavua vipengele husika vya hiyo kesi utafikiri wote mawakili. Utasikia kosa la mtandao la kusambaza ngono, kumuingilia kinyume na maumbile, n.k. lakini kwenye mikataba mibovu ya kuuza ardhi na rasilimali za nchi au kusoma katiba akhaaaa! Tunahitaji deliverance! Watu wanapenda na kufuatilia ngono kuliko hata Mungu
 
Ndugai alikuwa mbele ya muda!

Nilishangaa sana watz kuungana na chura kiziwi kumzodoa Ndugai eti ili kumkomoa marehemu Magu!

Kauli zile zilipaswa zitushtue watz maana zimetolewa na spika wa bunge ambae anajua karibu kila kitu kwenye nchi. Badala yake tukaungana na chura kiziwi kumtukana Ndugai.

Pale ndio nikaona watz ni wapumbavu sana.
Hii nchi ukipata nafasi piga ondoka, maana watu hawajielewi.

Sisi watz tunachoweza ni
. Ngono
. Uchawi
. Na Majungu tu basi
 
Ndugai bhana!!
Haya ilibidi ayafanye yeye na wenzie akiwa kiongozi wa muhimili unaojitegemea.
Sasa sahivi hata akisema, nani atamuelewa? Hivi kumbe viongozi wa nchi hii akili zao zinarudi wakishakua nje ya madaraka. Lol
 
cocastic hayo aliyasema akiwa spika wa bunge na ndiyo kauli iliyomuondoa hapo! Kwahiyo anastaili pongezi
 
Ndugai bhana!!
Haya ilibidi ayafanye yeye na wenzie akiwa kiongozi wa muhimili unaojitegemea.
Sasa sahivi hata akisema, nani atamuelewa? Hivi kumbe viongozi wa nchi hii akili zao zinarudi wakishakua nje ya madaraka. Lol
Kwa kiasi alianza kama kukemea na ndio Hilo ndio lililo mfanya akaachia ngazi
 
Katika moja ya comment zilizowahi kunishtua ni hii ya jobu aliyoitoa akiwa spika.

Alidai kwamba wenzetu baadhi ya mataifa linapohusika suala la mikataba, hawana masihara hata kidogo huchukua vijana smart class A wenye uwezo mkubwa wa kusoma kuelewa na kufikiri kwa upana juu ya mikataba tunayoingia kama taifa ni kwa namna gani itanufaisha umma. Akasema kwetu Tanzania hali ni tofauti kabisa kwani sisi huwatumia maprof wetu.

Ni kweli wana elimu nzuri lakini wamechoka kiakili kwa namna ambayo ni rahisi sana kutuingiza chaka. Alisema hii mikataba inaandikwa kijanja sana na ni mabook makubwa makubwa hiyo yanahitaji akili fresh ili kuyasoma kuyaelewa na kufanya maamuzi sahihi.

Mada ya mikataba ya nchi ni nzito sana haikupaswa kabisa kufanyika kizembe.
Hatuchukui ma Prof. Bali huwa tunapeleka wakuu wa idara au wakurugenzi wa idara husika ambao wamepanda vyeo kwa experience na siyo ubobevu wa eneo husika
 
Kuwa na A ni jambo moja, imepatikanaje na inatumikaje ni jambo jingine. Jambo la msingi, kama taifa yatupasa tuwe na timu nzuri ya mawakili wazalendo, wenye uzoefu na wenye weledi katika mambo ya sheria.
 
Tatizo la nchi hii watu ni wabinafsi sana ,wanajifanya wanauchungu wakiwa nje ya mfumo .Haya yangekuwa na Maana kama angeyasema kipindi ni speaker wa bunge , vinginevyo tunaweza sema ni wivu tu ,yeye mbona amen'gan'gania ubunge miaka na miaka kwani huko chemba hakuna vijana damu changa wanaoweza kuliwakilisha hili jimbo mpaka yeye tu au kwanini yeye amekuwa akipinga vyama vingine vya siasa vyenye mawazo mapya mpaka visishike nafasi yeyote ya uongozi nchini mpakaimepelekea CCM imekuwa kama empire watu wote wenye ideas zakuongoza nchi Kwa kukata tamaa wameamua kujiunga na chama hicho ili tu ndoto zao zitimie. Kama ana Manisha alicho kisema tu isiwe Kwa makataba kupewa vijana wenye uelewa Mpana bali hata katika nafasi za uongozi ndani ya chama chake awe anatoa matamko kama haya ,na yeye akiachia nafasi Kwa vijana itakuwa mfamo mzuri.
 
Alidai kwamba wenzetu baadhi ya mataifa linapohusika suala la mikataba, hawana masihara hata kidogo huchukua vijana smart class A wenye uwezo mkubwa wa kusoma kuelewa na kufikiri kwa upana juu ya mikataba tunayoingia kama taifa ni kwa namna gani itanufaisha umma. Akasema kwetu Tanzania hali ni tofauti kabisa kwani sisi huwatumia maprof wetu.
tena wa "majalalani" 😡
 
Kuwa na A ni jambo moja, imepatikanaje na inatumikaje ni jambo jingine. Jambo la msingi, kama taifa yatupasa tuwe na timu nzuri ya mawakili wazalendo, wenye uzoefu na wenye weledi katika mambo ya sheria.
walikuwa akina chenge, ambae tumbo lake na ubinafsi uliomjaa alituingiza ktk mikataba hovyo kabisa hasa awamu ya 4
 
Tatizo sio A+ tatizo nchi ya Tanzania haiendeshwi kama taasisi bali tuna mfumo kama timu za mpira , yaani si unoana Kocha akipewa timu basi anataka kubadili aje na mbinu mpya , hata wachezaji atasajili anaowataka .

Mkiwa na taasisi basi mtakuwa na watu smart endelevu kila sio kuwatumia wanasiasa .Nakupa mfano Wizara na mawaziri walitakiwa wawe wanajitegemea wasifungamane na siasa yaani wasitokane na wabunge , hii ingesaidia kupata watu wenye weledi tena wenye uzoefu kama wakuu wa mashiriki ..Waziri wa sekta fulani alitakiwa awe anachangulia kwa uwezo sio kwa vile ni mbunge . Je, kama wabunge wote kama hawana uwezo ? Ndio hapo wanapeana tu wanasiasa hizo nafasi kumbe kuna watu baki wako nje na uwezo mkubwa.

Mikataba itaendelea kuvunjwa kutokana kila raisi anakuja na mawazo yake na kundi lake la kufanya pamoja .Jengeni taasisi mikataba mingi itakuwa endelevu kwa maslahi mapana ya nchi . Raisi huyu kavunja baadhi ya taasi za umma alizoweka Magufuli sasa huoni kama tunarudi nyuma baada ya kwenda mbele ?​
 
Back
Top Bottom