Ndugai: Mkitumia lugha hizo tutagawa mbao hapa, shauri yenu...

Ndugai: Mkitumia lugha hizo tutagawa mbao hapa, shauri yenu...

Hata kama kwa katiba hii muungano utanusurika, tujue tu kuwa hautadumu.
 
Ndugai yuko sahihi kama ulikuwa unafuatila mjadala. Kuna mjumbe toka zanzibar kaongea kwa vitisho sana. Ndipo ndugai ktk kumjibu akasema hayo.
 
Ngungai ameongea kitanganyika na kizalendo zaidi Bora lawama kuliko fedheha. Wagawane mbao kieleweke
Nani hajui wewe pia ni sehemu ya watanzania ambao CCM imeweeka wakfu km bidhaa inayoweza uzw amara nyingi na kwa watu wengi km viwanja vya migogoro ktk halamashauri na vijiji vyetu. Huwezi kuwa tofauti wewe..utaishia jiua km mkwawa kuliko kukombolewa kifikra.
 
Kwa hili ndugai yupo sahihi.
Wznz ni walalmishi tu hawaonyeshi wapi wanakandamizwa.
Wzn wamekariri maneno ambayo hawawezi kuyaweka katika hesabu.

Wamekuja Dodoma wenyewe sasa malalamiko ya nini.
Kama wangejua wanakandamizwa wasingetokea Dodoma kabisa ili TUGAWANE MBAO.

Ndugai ni mwana JF hasa, hii kauli ni maarufu hapa JF 'Tuvunje jahazi tugawane mbao'.
Ndugai at least ameonyesha uchungu na Tanganyika inayolipa gharama kubwa ya muungano na kupata mgao wa faida ya mitusi na kashfa zisizo na kichwa wala miguu kutoka kwa wznz.

Narudia, wamekuja Dodoma bila police au kufungwa kamba, sasa wanalalamika nini.
Wangetaka kujikomboa tulishawaambia siku nyingi sana wasije, maana yake wangepata mamlaka kamili na wala wasingekandamizwa.
Midhali wapo Dodoma wamekubali na sasa wafunge vinywa vyao

Wabebwe halafu wacheze msewe kwenye migongo ya watu! ebo! alaah
 
kwa hili ndugai hoja anayo. ndugu zetu wa zanzibar wanaona kuwa wao wako sahihi kwa walisemalo wasikilizwe na wabembelezwe mi nimeipenda kauli ya dugai kama hawautaki muungano hapo ndio mahali pake ikishindikana tugawane mbao .lugha kali ila ndio ukweli wenyewe malalamiko ya tanganyika kuikoloni zanzibar bunge hili ndio mahala pake
 
Samahani kiongozi,MBILIMBI ndiyo nini? Maana nimecheka sana na huku sikijui,ila nimecheka the way ulivyo-present.
Kaka, mbilimbi ni matunda ambayo watengeneza chachandu/siki huchanganya ili kuweza kuleta ladha. Sijui kama ntakuwa nimeeleza vizuri, kama sivyo tunaweza kusaidiwa na wenye kujua zaidi.

Sasa tunda hilo likiwa bovu, ngozi yake ni laini mno na likiguswa tu linatumbuka. Ndo kafananishwa mtu hyuo.

Hii hapa picha yake:
90px-Averrhoa_bilimbi_fruit_by_Sugeesh.jpg

Mbilimbi Mbichi

120px-Averrhoa_bilimbi_ripe.JPG

Mbilimbi Mbivu


Mti wake.
 
Kasema kuwa kama Wazanzibar WATAENDELEA kudai uhuru wa Zanzibar basi wanagawanywa mbao, kama kwamba Zanzibar haina haki ya kudai uhuru wao na hajui kuwa katiba ya Zanzibar ilishaitangazia uhuru tangu huko siku zilizopita ......sasa huyu nafikiri anawatishia watu wa Zanzibar na wakati shiksa nitawashangaa sana maana watakuwa nao ni wapiga domo tu.......

kwanini unaweka maneno yako?ni kweli amesema ''kuwa kama Wazanzibar WATAENDELEA kudai uhuru wa Zanzibar basi wanagawanywa mbao'', ?​kusema uongo ni alama ya mnafiki.
 
Nakuunga mkono kuwa msikubali kuburuzwa lakini sio kwa sababu ya ukubwa na udogo wa nchi mbili hizi bali usawa kwa nchi husika.
Niruhusu na mimi niseme ZANZIBAR KWANZA MUUNGANO BAADAYE.

Ukiuangalia kiundani huu muungano unawabeba zaidi wanyiabaharini kuliko Tanganyika lakini kinachonishangaza hao wanyiabaharini ndiyo wamekuwa na kimbelembele cha kutaka maslahi na mamlaka zaidi kuliko upande pili, mtambue kwamba hilo halitakubalika kamwe.
 
Mkisema mnaitaka Tanganyika sitaki tena kusikia mnataka muungano...! Tumesema ama serikali mbili huru (Tanzania Bara na Zanzibar) ama serikali moja ya muungano.

Eh Tanzania Bara, wale ndugu zenu wa Mafya, Kisarawe mtawapeleka wapi....?
 
He! wandugu mbona mmemtolea sana macho Ndugai kwa kauli yake ya kishujaa aliyoitoa?? Ndugai yuko sahihi kabisa, haiwezekan kabisa nchi kubwa yenye watu mil.45 ikubali kuburuzwa na kisiwa chenye wakaz wasiozidi mil.2 tu, kitakuwa kichekesho kikubwa endapo wajumbe wa upande wa Tanganyika watakuwa wapole na kushindwa kuwadhibiti hao wanyiabaharini. Mimi namuunga mkono Ndugai, kama vp tupoteane tu kwani kitu gani bwana na huu ndiyo wkt mwafaka kabisa kwetu TANGANYIKA KWANZA MUUNGANO BAADAYE.

hata Tembo huangushwa na Chura mtoni....!!! pumbavvzzz!!!
 
hata watanganyika wanamengi ya kuongea ila hawana pa kuyasemea, tunataka serikal 3, nasie tupate pa kuongelea zanj n tone ndan ya bahar wakitaka waondoke hatunatym nao; wasepe tu
 
Hata kama kwa katiba hii muungano utanusurika, tujue tu kuwa hautadumu.



Kwa hali inavyoonekana naungana nawe kabisa, hii ni kama kukwepa kusinzia wakati usingizi unakunyemelea, ila muda wake ukifika utasinzia tu iwe isiwe.
 
anaweza akawa amesema sawa ila bila hekima..... hiyo sentensi inaonyesha pride na kudharau upande mwingine...
 
Back
Top Bottom