Hiki kilio ni wazi ww ama nyinyi ndio mna matatizo, kwanini usipuuze uendelee na mijadala mingine maana ipo mingi?! Nyie mliofaidika na ulevi wake wa madaraka ndio mnatushangaa baadhi yetu tuliona hayuko sahihi na hakustahili kuwa rais, haswa kwa katiba inayomfanya rais kuwa Mungu mtu kama yetu.
Nitafute attention kupitia Magu kwani alikuwa rais wa Marekani? Au kwakuwa nyie mlikuwa mnamuona Mungu basi kila mtu anamsujudia? Hili suala la vyeti ni bora hata mkae kimya, maana yeye alikuwa na PhD yenye utata mtupu, na hili liko wazi. Isitoshe kama ni vyeti fake bado hakuliendesha kwa haki kwani lilijaa double standard ya ajabu, maana aliiacha taasisi nyingi hasa za ulinzi na usalama bila kuwapigia, na huko vyeti fake viko kibao. Ifahamike haya kuhusu aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar alikuwa na tuhuma ya vyeti fake, na alikuwa anajibu kwa kejeli kuhusu suala hilo. Kwahiyo hakukuwa na suala la vyeti fake bali uonevu. Isitoshe mimi hata ningekuwa na cheti fake isingekuwa tatizo maana sio mtumwa wa ajira za serikali kama ww. Sauti inatosha au niongeze?