Al Watani
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 21,237
- 31,811
Aliyesababisha serikali na rais wafanye wanavyotaka ni Ndugai mwenyewe baada ya bunge na speaker kuanza kupokea maigizo ya rais badala ya join kuisimamia serikali, serikali ndiyo ikaanza kulisimamia na kuliagiza bunge.Ndugai naona mitazamo yake ya kiuchumi ni kama ya Samia Suluhu. Yule jamaa aliyekuwa anaua sekta binafsi alikuwa anaturudisha miaka 40 nyuma na wala hashauriki. Mashirika binafsi ya ndege alifanya juhudi yafe wakati ATCL ni hasara, PPP ilikuwa imeshakufa.
Watu mnalumu tu kwa nini hawakuongea Magufuli akiwa madarakani, pengine mlikuwa hamumjui Magufuli. Pengine waliona anaharibu sana na haambiliki wakaamua wamtangulize tu kama baadhi ya watu wanavyodai.
Spika Ndugai ndiye aliyesababisha serikali iwe ya udikteta baada ya Ndugai kupokea maigizo kutoka kwa rais ya kuwashughulikia wabunge bungeni naye akayatekeleza.
Kama Spika Ndugai angekuwa na akili walau kidogo tu angewaomba radhi watanzania ndipo afanye hizi uturn zake.
Nje ya hapo Ndugai alikuwa mnufaika wa uhalifu wa serikali ya awamu ya tano kama si mshirika muhimu katika uhalifu huo.