Ndugai: Watanzania wanalalamikia mfumo wa elimu, wanataka majadiliano

Ndugai: Watanzania wanalalamikia mfumo wa elimu, wanataka majadiliano

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema ipo haja ya kufungua Mjadala wa Elimu, na ndiyo maana Wabunge wamekuwa wakisema washirikishwe.

Akiwa Bungeni Dodoma amemwambia Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako, "Sisi tunataka Elimu ya Tanzania tuitazame. Hayo sijui ipo Wizara gani, sisi kama Wananchi haituhusu, tunataka tuseme tunataka nini kwenye Elimu"

Ameongeza, "Tena Elimu ya Chuo Kikuu ndiyo watu wanalalamikia kuliko hata ya chini. Mliangalie vizuri ndani ya Serikali, namna gani ya kushirikishana"

Chanzo: Bunge
 
Watanzania wamepiga sana kelele juu ya bunge kuwapokea wabunge wasiyo na chama mbona hakusema chochote?

Tuanzie hapo kwanza ni kwanini anatumia fedha za walipa kodi kwa kuwalipa watu wasiyo stahili?
 
Fundisheni kwa kiingereza kuanzia msingi hadi chuo kikuu
Hii ni suluisho zuri pia naona hii advance 5 &6 ziwe zinatoa elimu ya kuajirika kwa level fulani ili mtu akishindwa kuendelea chuo miaka yote hiyo aliyosoma isiwe imepotea bure maana ata ukimaliza form six saiv wew ni kama form 4 au la saba huna fani yoyote ya kuajirika ata basic technician certifate
 
Jamaa kajigeuza mpinzani, ni kichekesho.
Ashaanza kusoma alama za nyakati na kagundua hilo baada ya kuona na kugundua kuwa watanzania wamelisusa bunge lao linalo zidi kukosa mvuto
 
Hii ni suluisho zuri pia naona hii advance 5 &6 ziwe zinatoa elimu ya kuajirika kwa level fulani ili mtu akishindwa kuendelea chuo miaka yote hiyo aliyosoma isiwe imepotea bure maana ata ukimaliza form six saiv wew ni kama form 4 au la saba huna fani yoyote ya kuajirika ata basic technician certifate
Mtu kama Ndaluchako na Ndugaye utasikia wanakwambia eti jiungeni kwenye vikundi vya uzalishaji mali na kilimo mkazalishe.
 
Mfumo Wa Elimu Ya Tanzania Mwaka 1990- 2008 Hauna shida yeyote. Hakika Niliyofundishwa yote yananiweka Mjini.
Abrianna anafahamu na ningependa afanye Research na Kuutetea Mfumo wetu wa Elimu.
 
Mtu kama Ndaluchako na Ndugaye utasikia wanakwambia eti jiungeni kwenye vikundi vya uzalishaji mali na kilimo mkazalishe.
Watuambie wenyewe tangu waseme kilimo ni utii wa mgongo wa Taifa wamepiga hatua gani au ndiyo kimekua kibiongo cha Taifa
 
Watuambie wenyewe tangu waseme kilimo ni utii wa mgongo wa Taifa wamepiga hatua gani au ndiyo kimekua kibiongo cha Taifa
Ningewapongeza sana kama wangeamua kuwachia nafasi zao ili zizibwe kwa vijana wasomi wasio kuwa na ajira.

Lakini wanayasema hayo wakati wameng'ang'ania kwenye ajira zao huo ni uzandiki.
 
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema ipo haja ya kufungua Mjadala wa Elimu, na ndiyo maana Wabunge wamekuwa wakisema washirikishwe

Akiwa Bungeni Dodoma amemwambia Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako, "Sisi tunataka Elimu ya Tanzania tuitazame. Hayo sijui ipo Wizara gani, sisi kama Wananchi haituhusu, tunataka tuseme tunataka nini kwenye Elimu"

Ameongeza, "Tena Elimu ya Chuo Kikuu ndiyo watu wanalalamikia kuliko hata ya chini. Mliangalie vizuri ndani ya Serikali, namna gani ya kushirikishana"

Chanzo: Bunge
Huyu angepumzika tu sasa
 
Najaribu kuwaza hapa, mustakabali wa elimu ukajadiliwe na form four failure, sijui nini kitatoka hapo, lakini pia sina uhakika hata kama wabunge wameelewa muktadha wa spika wao katika hili suala.

Mi naona bunge liunde kamati itakayohusisha wasomi na baadhi ya wabunge (ambao pia wana exposure juu ya mifumo ya elimu)

Lakini bunge likijichukulia huu mjadala lenyewe tuu, nawaza yule mbunge aliyesema magufuli aongezewe miaka hata kwa kumlazimisha atachangia nini
 
Huyu anakoenda, bado kidogo kuwa kichaa.

Hivi wananchi wanacholalamikia ni elimu pekee?

1) katiba mbaya wananchi hawajalalamikia?
2) tozo hawajalalamikia?
3) kutokuwepo ongezeko la mishahara kwa wafanyakazi wa umma, hawajalalamikia?
4) polisi kubambikia watu kesi na kuua mahabusu,wananchi hawajawahi kulalamikia?
5) kukosekana tume huru ya uchaguzi, wananchi hawajalalamikia?
6) wabunge kutolipa kodi stahiki, wananchi hawajalalamikia?
7) nchi kuwa na bunge bandia na kimeo, wananchi hawajalalamikia?
 
Back
Top Bottom