Ndugu Harrison Mwakyembe tafadhali tukutane Monduli kwenye mazishi ya shujaa Edward Lowassa!


Sasa huoni kama huyo Bwana mkubwa ni mwamba, watu wote wakususie uchaguzi eti TISS wabaki peke yao na wewe halafu ushinde uchaguzi, 2010 huyo jamaa alishinda kihalali kabisa.

Huyo Bwana mkubwa unayemsema ndiye Bwana mipango mwenyewe refer 1995 pale chimwaga umri Ile na ujasiri wa kuutaka Urais na Ile speech iliyomfanya JK Nyerere asimame kumpa mkono na kumkumbatia.

Kifupi tumuombee Marehemu kwenye safari yake mpya, huku kwenye mtifuano wa Urais hakuwa na nguvu kumdhidi yule jamaa wa Saigon.
 
Kweli duniani kuna mambo ya ajabu. Harrison Mwakyembe aliteuliwa auchunguze mkataba wa Richmond na TANESCO akafanya hivyo. Je alitakiwa akatae kazi aliyopewa na bunge? Akatoa ripoti ya Uchunguzi kuonyesha alichogundua. Nakumbuka wajumbe wa Tume waliapa kuwa ikiwa mtu yeyote ndani au nje ya bunge angegundua jambo lolote la uongo ndani ya ripoti basi wajumbe wote wangejiuzulu nafasi zao zote za uongozi ndani ya bunge serikali chama. Sasa baada ya ripoti kujadiliwa yakatokea yaliyotokea. Sasa kosa la Mwakyembe ni lipi? Kuongoza tume? Au alitakiwa asiandike vilivyogunduliwa?
 
Kwa maelezo hayo, nimeamini kweli Dk. Mwakyembe ni Mwamba!
 
Jamaa alinibowa pale kwenye kampeni za uchaguzi mwaka 2020 alipomuambia mtu wa darasa la Saba kuwa yeye ana degree 4.

Huyu Mwakyembe alisoma shule lakini HAKUELIMIKA
 
CCM kuwa na minyukano ni jambo la kawaida hata Lowassa kuna watu/kundi la watu alikuwa anawanyuka na ndio maana akawa na mafanikio CCM
Minyukano ya ccm ndio uhai wao...jamaa niliwakubali walipotuzuga na vua gamba ..ni km wanagombana kumbe ndio wanawekana sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…