Ndugu J. Gwajima, ushahidi wa Mpina haujathibitishwa popote, hivyo huna HAKI ya kusema amedanganya

Ndugu J. Gwajima, ushahidi wa Mpina haujathibitishwa popote, hivyo huna HAKI ya kusema amedanganya

Salaam, Shalom!!

Leo naongea na Ndugu Gwajima kama kiongozi wa wananchi, na SI kama Askofu madhabahuni.

Nimekusikia ukidai na kumtuhumu Ndugu Mpina kuwa mwongo bila kuthibitisha UONGO huo Kwa data na ushahidi kama alioutoa ndugu Mpina hadharani.

Umeenda mbali zaidi na Kutoa LAANA Kwa Ndugu Mpina ukiquote maandiko kuwa " Amelaaniwa mtu ampigaye ndugu yake Kwa Siri" Sasa Mpina na Bashe Wana undugu Gani? Nani aliyepaswa kuitwa kamati ya maadili kati ya Mpina na Bashe? Giza na Nuru lini vimewahi kuchangamana?

Leo umeungwa mkono na mtu aina ya chiembe, hiyo ni dhahiri kuwa umetoka kwenye line ya HAKI.

Ndugu Gwajima, ndugu zako ni wananchi maskini, ndugu zako ni wote wanaamini juu ya HAKI kutawala juu ya nchi,

Ndugu Gwajima huna ndugu CCM, wewe unatambulika una Damu ya Upinzani, na record Bado zipo wazi juu ya uhusika wako wa wazi kumleta Lowwassa CDM, hivyo ninakukumbusha kuwa huna mizizi CCM.

Nikupe taarifa kuwa Wananchi tumekielewa alichokisema ndugu Mpina, na ameyasema hayo Kwa Uzalendo wake Kwa nchi na hakuongozwa na chuki binafsi juu ya Waziri Bashe kama unavyodai.

HOJA zijibiwe Kwa HOJA,

Evidence ipingwe Kwa EVIDENCE SI porojo za kisiasa.

USHAURI: Ndugu Gwajima ,BUSARA ni kunyamaza, ulinyamaza kwenye sakata la DP world na ulieleweka kuliko sasa unavyofungua kinywa kumkemea NABII MPINA.

Amebarikiwa sana NABII MPINA Kwa kuwa amesimama upande wa KWELI na HAKI.

Mungu ibariki nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿, Amen

Source: Uhondo Tv.

Karibuni 🙏
Mchungaji uchwara
 
Mchungaji kanjanja
Tujifunze kujadili issue not personalities.

HOJA hapo ni Mpina ameleta HOJA za maandishi zenye evidence,

Hakuna Tume au uchunguzi wowote uliofanywa kuthibitisha HOJA za Mpina ni UONGO,

Mpina amepigwa stop kuhudhuria vikao SI Kwa Sababu ya HOJA alizotoa, Bali Kwa kutumia eneo la Bunge.

Na wabunge wanamtuhumu kudanganya bila kusema ukweli ni upi.

Tujadili hayo, SI kujadili watu, Bali HOJA wasemazo.🙏
 
"The world will not be destroyed by those who do evil, but by those who watch them without doing anything" - Albert Einstein
Ahsante kwa Mpina kwa kukataa hili.
 
Hapana SI Mimi.
kumbe kuna Rabbon wawili huku ndio
maana, sorry sana nimeshampata yeye in single R wewe ni double R

 
kumbe kuna Rabbon wawili huku ndio
maana, sorry sana nimeshampata yeye in single R wewe ni double R

Wako watatu Rabonn ,Rabbon na Rabboni
 
Na kale kakiosk ka kuuza simu pale Ilala
Michango mingi ya wabunge kuhusu Tume ya Spika juu ya Mpina, ilikuwa maelekezo baada ya kupata party corcas,

Yaani waliamini, CCM ingeruhusu HOJA za Mpina zijadiliwe, zingeangusha chama na Serikali.

Bunge la Spika Sitta, linabaki kuwa Bunge la kihistoria lililosimama kama Muhimili mkuu wa pili.

Hivi sasa Spika anatoka na kuipongeza Serikali Kwa u umilivu wa kuhusu alichoongea Mpina 🤔
 
Michango mingi ya wabunge kuhusu Tume ya Spika juu ya Mpina, ilikuwa maelekezo baada ya kupata party corcas,

Yaani waliamini, CCM ingeruhusu HOJA za Mpina zijadiliwe, zingeangusha chama na Serikali.

Bunge la Spika Sitta, linabaki kuwa Bunge la kihistoria lililosimama kama Muhimili mkuu wa pili.

Hivi sasa Spika anatoka na kuipongeza Serikali Kwa u umilivu wa kuhusu alichoongea Mpina 🤔
Maana yake yale yote aliyoleta Mpina yamezikwa rasmi. Laiti tungekuwa na uchaguzi huru na haki tusingeshuhudia ujinga huu kwani tungetoa hukumu kwenye sanduku la kura, lakini kwa kile kilichofanyika 2020 ni dhahiri kamwe watawala hawatakaa waweheshimu wananchi tena kwani wanajua hatuna cha kuwafanya.
 
Back
Top Bottom