Ndugu naomba ushauri akili imestack

Bora hata huyu kuna mmoja kafungiwa na mlango kalala nje leo yupo kumuomba msamaha mwanamke ila wanaume kuna mda tunajitakia hizi shida
Na bado! nani aliwaambia watu kila binadamu anafaa kuoa/kuolewa? kumzalia/kumzalisha?

Wanatesa watoto.

Kuna watu tunawaona huku mitaani, wamenyooka kama rula, familia ni familia wanapiga hatua.. watoto wanasoma darasa moja, darasa la kumi mwisho wanajitegemea, hakuna vurugu wala heka heka. Na kuna hawa wengine kutwa vita kama gaza, Hatujiulizi kitu? kuna mahali tunakosea na hatuko tayari kwa huu mjadala kama jamii.
 
Sasa Fazaa kwa matukio hayo yote na matendo aliokufanyia bado tu una moyo wa kurudiana nae?

Mimi wa 2000 nina miaka 24 nitajifunza nini kwako wewe wa miaka 35+?

Anakiburi, hajijushi, dharau, ugomvi na MWIZI wa pesa zako za ndani hadi kwenye account za benki na mitandao ya sim bado unataka kurudiana nae tu?

Kama ameondoka huoni ndio tikeki nzuri sasa ya wewe kuishi maishi mazuri? Muache aende ila kama unaweza. Kama huwezi nenda ukweni kapige magoti na kuomba msamaha maana ni kawaida yako hujaanza leo kumpigia magoti
 
We nenda kwa lengo la watoto wako tu, huyo mwanamke hata ukielezea vipi kwao ushachafuliwa kiasi kwamba hautaeleweka. Wewe jishushe lengo likiwa ni watoto wako.

Kama anakupenda angeenda kwenu, nashangaa ameenda kwao, wewe ndio unatakiwa kumshitaki kwao na sio yeye kutangulia kukushitaki. Shituka brother wanawake sio wenzetu.
 
Watoto watoto yaani hao ndo fimbo ya kukuchapia. Utakua bwege hadi lini,utaenda kuomba msamaha kwa kosa gani. Mpotezee kaa kimya. Watoto watakariri darasa mwakani. Ukizembea ukaenda omba msamaha na kujieleza utajikuta siku moja una kesi ya mauaji
 

Endelea na Maisha, achana na mambo ya wanawake
 
expand...
Ikibidi fuata hii nukuu:- "Haijalishi ni umbali gani umekwenda, lakini kama unahisi umepotea njia rudi mwanzo ukaanze tena safari yako". - Kama umetoka MBEYA kwa lengo la kwenda DAR ES SALAAM lakini kwa bahati mbaya umefika sehemu unaulizia wapi ulipo; unaambiwa upo SINGIDA, ni dhahiri kuwa umepotea njia hivyo ni vyema kurudi nyuma ili uelekee njia sahihi ya kwenda DAR ES SALAAM kuliko kuendelea kunyoosha lami ya kwenda MWANZA...Ukijifanya mvumilivu wa kuendelea kunyoosha lami utafika MWANZA halafu utaambiwa rudi nyuma, na ili kuwahi hitaji lako utalazimika tena kupanda ndege kwa gharama kubwa....KWA HUYO MWANAMKE UMEPOTEA NJIA....Kama umesoma CUBA utakuwa ushanielewa.
 
Mkuu usije thubutu kuja kuishi na huyo mwanamke ama kufikiria kumuoa, alipaswa awe mpole akijua kwamba wewe ndio mwanaume wake. Kwa matukio yote hayo hapo juu, hakuna mwanamke hapo. Nimewahi kuwa na mwanamke kama huyo, kiburi, hawezi kujishusha, neno samahani ni msamiati kwake.

Huyo wako anatokea mkoa gani?
 
jnbg kwanza pole.

Kwa ulivyoandika tu inaonekana wewe ni tatizo kubwa.
Mke anaingia madeni makubwa wewe upo tu.

Mke anaiba na kuiba wewe upo tu

Mke anapenda kwao na kurudi Tena kwa kutoroka

Unachukua kisu, ili uchinje iweje sasa? Unapigana na jitu kubwa miaka yote, unachokitafuta utakipata. Huu ni ugonjwa wa akili.

Anza upya, jirekebishe acha kuwahusisha wazazi wenu kwenye ndoa Tena. chungulia vizuri hadi umpate yule mke uliyetongozana nae. Afu mjulishe kwamba Sasa unamtaka yule nae mwambie arudi hiyo stage.

Tuzna familia yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…