Ndugu naomba ushauri akili imestack

Ndugu naomba ushauri akili imestack

Ebu tulia kwanza, Yan8 tangu 2014 na watoto wa4 unaita Mahusiano?

Eeh Mungu watazame watu wako..........πŸ™„πŸ™„πŸ™„πŸ™„πŸ™„
 
Huyo bint ni kibaka na kwao ndo wamemlea hivyo hutoboi, Nenda kawachukuewatoto wa Umri wa shule hao wadogo mwachie utakua unawatumia mahitaji yao muhim tu. Ya nini upoteze roho mwanaJF mwenzetu aibu kitu gani bwana...?
 
Mimi Nina umri Miaka 38 sasa Nina mahusiano na mwanamke tangu mwaka 2014 na tumezaa watoto 4 kati ya hao 1 Mungu amemchukua na sasa Hivi tuna ambaye mwezi wa 10 atatimiza mwaka na wawili wapo shule darasa la 3 na 2.

Sijawahi kufika kwao tangu 2014 mpaka mwaka 2022 pale aliponiibia vitu vya ndani TV,pasi ya umeme, laptop,redio,baadhi ya vitambulisho vyangu,simu,blenda,Kadi ya benki,,,shs.477000 Kaitoa benki mana Anajua password.Kaondoka na watot pia!

Sababu za kutofika kwao

1.Umbali kikazi ulichangia mana
nilikuwa busy na uhamisho na mim pia kwetu sijaenda tangu 2017 Hadi 2021 kwa ajil ya Mazish

2.Huwa hatuelewani kwa Muda mrefu Katika mahusiano yetu mana Ana kiburi,madharau,akinikosea hajawahi kuomba msamah mpaka nitakapojirudi mwenyewe,,,hivyo nikawa na hofu kwamba itakuwaje Kama tutafunga ndoa Kama ktk Hali ya sasa yupo hivyo??

3. Hata akinikera hawezi kujishusha yupo tayari kupigana na tulishapigana akanipeleka ofisi ya kata tukashauriwa Lakini hakuna mabadiliko

4.Ana Tabia ya kunipekua,,,kuna siku nilitegesha pesa chini ya meza akaichukua afu nikamwambia kuna pesa nimeangusha chumban Kama aliiona akakataaa katu Lakini mwishow amekubali

5.Huwa tunakosana Sana mpaka nikaanza kunywa pombe,,,Mara pengin nashinda nje usiku Lakini Naona haimugusi wala ushaur hakuna

6.Siku aliponiibia pesa benki akajitetea nyumban kwao kuwa hakuna matumizi Jambo ambalo Halina ukwel,,,na wazazi wake wanamuunga mkono Hata nijieleze vipi

KILICHOTOKA SASA HIVI
1.Amekuwa akichukua kila pesa anayoiona kwangu,,,ndani Hata kweny akaunti ya mitandao yangu ya simu na kucheza nayo kamari

2.Amekuwa na madeni mengi ya nje hiyo pesa amepeka kweny kamari

3.Nimemshirikisha baba yake juu ya kuchukua pesa zangu kwa siri na madeni ya nje Lakini baba yake katulia tu

4.Tareh 10 kuchukua pesa iliyo ndani nilipomuuliza lawama hajui baadaye kakubali,,tarehe 11 kachukua pesa
nyingin nikaumia Sana nikampigia usiku baba yake akaniambia nimpandishe kwenye gari na watot wake,,,mim nikaenda kunywa pombe asubuh nikamtaka aondoka na Arudishe pesa zangu,,,,,tukalumbana Sana mpaka nikachukua kisu mwishowe ameondoka na watot.

KESI HUKO KWAO
Ninahitajika kwenda KWAO nikajieleze na kuomba msamah kuwa nimemfukuza pamoja na watot,,,kumbuk watot wanatakiwa kwenda shule kesho

Naombeni ushaur jaman,,,,akili haifanyi Kazi mana Nataka tuachane Lakini nafsi inakataa Sababu Nina watot Naye,,,nyumbani wanajua nimeoa hata kazin pia,,,,,,NAONA AIBU
Achana nae huyo,uzuri wa mwanamke haukusaidii chochote,hilo ni tatizo na siyo dogo... mwanamke anajua mpaka gg,3+!!
 
Mungu fundi, vijokoleo havibaguani kamwe ni gusa unase ila linapokuja swala la kuoa ndo unagundua uligusisha mahala sipo afu ushatia mchanga sasa tabia zinakushinda ila bao aaah.
 
2.Huwa hatuelewani kwa Muda mrefu Katika mahusiano yetu mana Ana kiburi,madharau,akinikosea hajawahi kuomba msamah mpaka nitakapojirudi mwenyewe,,,hivyo nikawa na hofu kwamba itakuwaje Kama tutafunga ndoa Kama ktk Hali ya sasa yupo hivyo??
Lakini mkazaa Wakwanza, wapili, hadi watatu.....acha hizi Lame Excuses brother hazitakufikisha popote
 
Ninahitajika kwenda KWAO nikajieleze na kuomba msamah kuwa nimemfukuza pamoja na watot,,,kumbuk watot wanatakiwa kwenda shule kesho
Mkuu wewe ni Kabila la Msukuma? Na Huyo Mwanamke ni Mweupe sana?

Samahani lakini maana nataka tukishauri basi Ushauri wetu uwe Relavant.
 
Visanga vyote hivyo Bado tu Halmashauri ya kichwa chako unaomba ushauri!?? .... Huyo mwanamke ni kiboko ..ndio alikutoa ujana wako au kakuroga!?? Visa vyote hivyo bado unataka kwenda kuomba msamaha!??..... La msingi ni elimu ya watoto tu .... Na ole wako umuachie hao watoto hutoamini....
Usicheze na Nyapu.....yaani ukiwa mtu wa nyapu sana utamuona mwanamke ndio kila kitu kwako no.matter what.

Hizo ni akili za mtu anayewekeza maisha yake kwa mwanamke...

Natafuta ajira kila siku anawafundisha mnakaza vichwa maji.
 
Mimi Nina umri Miaka 38 sasa Nina mahusiano na mwanamke tangu mwaka 2014 na tumezaa watoto 4 kati ya hao 1 Mungu amemchukua na sasa Hivi tuna ambaye mwezi wa 10 atatimiza mwaka na wawili wapo shule darasa la 3 na 2.

Sijawahi kufika kwao tangu 2014 mpaka mwaka 2022 pale aliponiibia vitu vya ndani TV,pasi ya umeme, laptop,redio,baadhi ya vitambulisho vyangu,simu,blenda,Kadi ya benki,,,shs.477000 Kaitoa benki mana Anajua password.Kaondoka na watot pia!

Sababu za kutofika kwao

1.Umbali kikazi ulichangia mana
nilikuwa busy na uhamisho na mim pia kwetu sijaenda tangu 2017 Hadi 2021 kwa ajil ya Mazish

2.Huwa hatuelewani kwa Muda mrefu Katika mahusiano yetu mana Ana kiburi,madharau,akinikosea hajawahi kuomba msamah mpaka nitakapojirudi mwenyewe,,,hivyo nikawa na hofu kwamba itakuwaje Kama tutafunga ndoa Kama ktk Hali ya sasa yupo hivyo??

3. Hata akinikera hawezi kujishusha yupo tayari kupigana na tulishapigana akanipeleka ofisi ya kata tukashauriwa Lakini hakuna mabadiliko

4.Ana Tabia ya kunipekua,,,kuna siku nilitegesha pesa chini ya meza akaichukua afu nikamwambia kuna pesa nimeangusha chumban Kama aliiona akakataaa katu Lakini mwishow amekubali

5.Huwa tunakosana Sana mpaka nikaanza kunywa pombe,,,Mara pengin nashinda nje usiku Lakini Naona haimugusi wala ushaur hakuna

6.Siku aliponiibia pesa benki akajitetea nyumban kwao kuwa hakuna matumizi Jambo ambalo Halina ukwel,,,na wazazi wake wanamuunga mkono Hata nijieleze vipi

KILICHOTOKA SASA HIVI
1.Amekuwa akichukua kila pesa anayoiona kwangu,,,ndani Hata kweny akaunti ya mitandao yangu ya simu na kucheza nayo kamari

2.Amekuwa na madeni mengi ya nje hiyo pesa amepeka kweny kamari

3.Nimemshirikisha baba yake juu ya kuchukua pesa zangu kwa siri na madeni ya nje Lakini baba yake katulia tu

4.Tareh 10 kuchukua pesa iliyo ndani nilipomuuliza lawama hajui baadaye kakubali,,tarehe 11 kachukua pesa
nyingin nikaumia Sana nikampigia usiku baba yake akaniambia nimpandishe kwenye gari na watot wake,,,mim nikaenda kunywa pombe asubuh nikamtaka aondoka na Arudishe pesa zangu,,,,,tukalumbana Sana mpaka nikachukua kisu mwishowe ameondoka na watot.

KESI HUKO KWAO
Ninahitajika kwenda KWAO nikajieleze na kuomba msamah kuwa nimemfukuza pamoja na watot,,,kumbuk watot wanatakiwa kwenda shule kesho

Naombeni ushaur jaman,,,,akili haifanyi Kazi mana Nataka tuachane Lakini nafsi inakataa Sababu Nina watot Naye,,,nyumbani wanajua nimeoa hata kazin pia,,,,,,NAONA AIBU
Pole sana mkuu, usijaribu kutumia nguvu kwenye jambo linaloweza kutatuliwa kwa upendo. Nguvu ni kwa ajili ya uhalifu tu.

Kwa maelezo yako, mkeo anahitaji kupendwa, kusikilizwa na kupata muda wa kutosha na wewe, lakini wewe ukitoa hela ya kula unaona umemaliza.

Kwanza, yatambue makosa yako kabla ya hujaanza kutafuta makosa ya mwenzi wako, kisha shirikiana na mwenzi wao kuyatatua.

Mfuate mkeo, kwani yeye na watoto wamekumiss pia, hawana mwingine aliye baba yao mzazi, ni wewe. Nenda ukawaone, mrudi nyumbani.

Nenda ukaweke ahadi ya kuhalalisha uhusiano wenu, wazazi wake hawataki binti yao aishi kihuni huni tu, na tayari ashakuzalia.

Mkirejea nyumbani, sikiliza mahitaji ya mkeo na uwe unayatatua, sio lazima kila siku awe akikuomba hela kwa ajili ya mahitaji yake.

Usirudie kumpiga wala kupigana na mkeo, mpende sana na ongeza muda wa kuwa karibu naye, ongeza zaidi mawasiliano mkiwa mbali.

Mjulishe yeye mkeo kuwa unaenda kuwafuata. Mwambie umewamiss yeye na watoto wenu. Anzeni upya.

Ova
 
Nilimkuta bikra boss
Huyo sio mkeo umeoa mke wa mtu
Red flag uliona mapema ukapuuzia
Utakufa kabla ya siku zako
Ushazaa nae vumilia usibiri muda wako wa kufa basi
 
Achana naye na usirudi nyuma, watoto watasoma huko huko walipo, hawezi atakurishia.
 
Mibumunda kama wewe mtaendelea kupigwa sana mpaka akili ikae sawa.
 
Inapotokea unaachana na mama wa mtoto/ watoto na wapo chini ya miaka 7 utawaacha na mama na utatakiwa kua unawatumia pesa ya matumizi pamoja na kuwaunga na mfuko wa bima.

Ikatokea mama anaishi maisha ambayo hatoweza kuwalea watoto katika misingi inayotakiwa mfano anafanya kazi bar, mzururaji n.k. na watoto hawajafikisha hiyo miaka 7 baba anaweza kuwachukua watoto na atawakabidhi kwa bibi (mama wa baba) kwa ajili ya malezi.

Pesa ya matumizi itakoma watoto/ mtoto wakifikisha miaka 18.

Hata hivyo kwa sifa ulizotaja za huyu mwanamke ninashindwa kuelewa ilikuaje mkafikisha watoto 4. Pia kumbuka ofisi ya kata haiachanishi wanandoa. Wanandoa watatafuta talaka mahakamani kwa yeyote atakayeona haoni haja ya huo muungano.

Una sehemu yako ya makosa haujaisema, umemshikia kisu mama wa watoto wako hili ni kubwa. Umesema sana kuhusu kuongea na wazazi wake ila hakuna sehemu umeongea na wazazi wako.
 
Kabla ya yote nikulize una pesa ? Au upo zako Na mishahara ya Tamisemi , kama unayo pesa achana naye haraka sana , tafta mwanamke mwingine usichukue chochote mlichochuma naye , anzisha familia nyingine mimi huyu mzazi mwenzangu hazingui kivile , ila nakwambia nimeanzisha familia yingine yaani huko napewa Mahaba ya ajabu na single mother wa sasa nilichompatia ni kanyumba ka kuishi na mtaji kidogo tu ili ahudumie mtoto niliyezaa naye hakika linapokuja suala la mapenzi naenjoy sana ntaacha kuoa if I will be blessed to live longer huku duniani na nikifika miaka 70, niumize kichwa kuhusu pesa na mapenzi eti yaniendeshe hapana, huyu mwenzangu baada ya kujua nimejiweka mahali na single mother aisee amebadilika sana mtiifu na msikivu maana nimemuahidi kuongeza mke ramsi akileta mbwembwe na Mali zangu mimi Nina tofauti ndogo Sana na hakim yule chezaji ya psg nandika watoto na nawajulisha ndugu so Huwa anasikia tu mumeo huko kanzisha mradi fulani
Eti unaandika watoto huo mali ni zenu wote akienda kwenye sheria anakushinda mapema. Hkuna mtoto anayemiliki mali. Kazitoa wapi... kma unataka kumzidi ujanja?? Mwandike mama ako lkn je ndgu wakigundua jua hio mali itakuwa si ya kwako tena kma mama yenu.akifariki.
 
Kwao usiende, kwanza unaenda kama nani wakati hujaoa wala kuchumbia huko kwao. Wazazi wa binti nao ni wahuni tu kama nyie watoto wao.

Wewe chakufanya andika barua kwenda kwa mkuu wa shule wanaposoma watoto, ipitie kwa mtendaji wa kata na kwa afisa elimu kata na wilaya pia ngazi ya elimu ya msingi.

Watoto awapo kwako, wamechukuliwa na kwenda kufichwa kwa babu na bibi yao mzaa mama na mama yao hivyo watake hao maafisa watumie nguvu yao kisheria kuwataka hao watu watatu kuwarejesha watoto ili waendelee na shule. Usisahau kuwa CC: Afisa ustawi wa jamii pamoja na Mkuu wa dawati la kijinsia polisi na Ofisi ya Mkuu wa wilaya

Wewe kaa kwako tulia acha wapambane na serikali, nakuhakikishia hawatakaa wathubutu tena ila wanaweza kukuloga kiongozi πŸ˜‚πŸ˜‚.

Kuna mambo.wewe tumia mifumo tu maana ukisema utumie nguvu zako ni kujichosha wakati kuna watu wanalipwa mishahara kwa kodi yako ili wafanye hizo kazi.

Ukitaka kuandikiwa hiyo barua sema pia.
 
Back
Top Bottom