Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,804
- 134,593
Naunga mkono hoja na hiki ndicho nilicho shauri , Polepole ajitoe ndani ya CCM awe huru kukosoa.Kumpinga Dr. Samia ni haki ya kila anayejisikia kufanya hivyo, kwasababu kila mtanzania anayo haki ya kumchagua mgombea anayemtaka.
Lakini mtanzania unapojinasibisha kuwa mwana CCM unapoteza haki ya kumpinga mgombea wa CCM badala yake unakuwa na wajibu wa kumtetea. Kumpinga mgombea wa CCM, ukiwa umevaa sare za CCM ni USALITI.
Ushauri wangu, kama mwana CCM, hukubaliani na mgombea aliyeteuliwa, mambo ya kufanya ni mawili. Moja, baki ndani ya chama ukiwa umenyamaza, Mbili, Ondoka kwenye chama ufanye kazi ya upinzani. Lakini kufanya upinzani ndani ya chama, hizo ni vurugu.
P